Amavubi
Nyani Ngabu
Inasikitisha mno lakini hali duni ya maisha ndio hufanya waitwe hivyo! Maisha yao ni ya kimaskini makazi yao ni kule kwenye zile nyumba zulizobanana mpaka vyoo, hakuna ramani wala mitàa.
Chakula Chao,mavazi yao, mapambo yao nyumba zao na maisha yaovyote vyote ni vya kuungaunga! Hawamiliki magari hawana elimu hawana nyumba nzuri kubwa zenye nafasi supermarket kwao ni anasa!ofa zao ni chips kuku!Inasikitisha lakini hawakuyapenda hawakuyachagua hayo maisha bali mfumo mbovu ndio tatizo.
shida yangu ni pale tunawekeana matabaka kwa sababu wa kinondoni wanawaona wa manzese waswazi, wakati wa mikocheni wanawaona wa kinondoni wa uswazi...tumeshagawanywaTafuta uswahilini ukae hata masaa mawili utagundua tofaut ikoje...japo hii ni historical issue waswahili walionwa watu wasio wastaarabu, maskini, watumwa .. Ile kasumba ikatuvaa na sisi pia
hii hata mimi nimeionaDaaaaa ndipoo ninapoishii huku uswazii yaan Dada zangu wao hawana plan b ya maisha haya waliyonayo wameridhika nayo yaan wengi wanawaza kushona sare za shughulii na kwenda kucheza vigodoro na ngoma na kwendaa kusutanaa .mungu awasaidie madada hawaa
Ni mwendelezo ule ule wa ujinga wa Mwafrika.
Ukiwa na 'mambo ya Kiswahili' (mpaka sasa sijawahi kuelewa mambo ya Kiswahili ni yepi hasa) ndo unaitwa wa Uswazi.
Ukiwa una mambo ya Kizungu (hata haya sina hakika ni yepi,labda ndo yale mambo ya yes-no nyingi na kufuatilia kwa ukaribu yajiriyo Marekani) ndo labda utakuwa si wa Uswazi?
shida yangu ni pale tunawekeana matabaka kwa sababu wa kinondoni wanawaona wa manzese waswazi, wakati wa mikocheni wanawaona wa kinondoni wa uswazi...tumeshagawanywa
mkuu hapa naakuekewa sana sababu unaishi nao kabisa hapo Mabibo Makutano