Hivi mnataka mpendejwe?

Kwa tabia hizi mnafikiri tutawataka, bora twende na vibabu vya kizungu hata vinatusikiliza kuliko nyie mnakuja usiku hamtaki kuulizwa, huko bar mnakaa kaa na vimada mkiulizwa vita, ahaha nimechoka, eti mwingine anashauri utafute nyumba ndogo imekula kwenu, ningemuona huyo mkeo ningempa dili la kupata mzungu ndio ungejua. Weka namba ya simu ya huyo mkeo alete na picha uone mambo. Acheni hizooo zimepitwa na wakati. Mke au mume kila mmoja natakiwa kupewa heshima, Acha mfumo dume. Tena endeleeni tu, tutawawekea na mazamu ya kufua kupika na kunyonyesha we ngoja. eti unampa kila kitu sijui gari watoto unatunza sijua full tank WHAT IS THAT? Alitoka kwao kwa ajili yako sio vitu. Mbona vitu tunaweza kutafuta tu. kwa kwa vile tunawaheshimu bana. KATAFUTE NJIA YA KUELEWANA NA MKEO ACHA UONEVU. NIKIMUONA TU NAMPA DILI LA MMBABU WA KIZUNGU.
khaaaa! hapa inabidi niongee kiyunani. sakramento do sokeloisa teruim liyalo asrotose. Amen!
 
Hapa inategemea. Ukileta za kuleta wanakuwa sawa na CCM. Inabidi uwe makini kijana. We si unaona Bishanga analia hovyo? Mke alimuoa mwenyewe kwa mapenzi yake wala hakutushirikisha achilia mbali kutualika, yanamshinda anakuja kutulilia, tulimtuma? Atulie hapo hapo na mke huyo huyo na tena ampende kwa moyo wake wote.
hii ni kusema wanawake ni sawasawa na CCM, kabla uongozi/ndoa ma ahadi kibao, wakishakupata uongozi/ndoa lambada linaanza. dah!
 
Hahahahahaha. Una kiburi wewe. Unataka kumkandamiza mkeo! Una bahati hujawa mume wangu, nngehakikisha unanyooka kwenye mstari. Wewe uongee tuuuuuuuuu mwenzio akae kimya! Kisa? MUME. Na yeye si MKE? Mpe nafasi mkeo, vinginevyo kama anakudharau, ila kama anakushauri kwa heshima na Upendo kwa nini usimsikilize?? Punguza munkar basi Shem.

kule kwetu ntwara inategemea ntu na ntu
 
Kuna siku nilimwaga hapa mikero kibao ya kinamama,mimgine hii hapa:

1. Mara akwambie oh Ex wangu alikuwa hivi mara vile,ya nini yote bana? mbona mliachana sasa?

2.'We nae mpira tu kila siku',maneno gani ya kunambia hayo? Fikiria kesho Man U anakipiga na Chelsea halafu nikitaka kwenda pub nikaangalie unaniletea za kuleta,nikisema nikae mnaweka mi tamthiliya yenu,is it fair,saloon mbona sikuzuii kwenda?

3.Mara oh 'naona mapenzi yamepungua' mwanzo yalikuwa kilo ngapi na sasa kilo ngapi?yamepungua kivipi umeyapima na nini? kwa nini unanipa mastress ya kukuonyesha mapenzi,si uache ya flow tu,mwisho nitakuwa mnafiki!

4.'Sipendi marafiki zako hao'.Alllaaaa yamekuwa hayo? Enzi ya uchumba tunajirusha hadi majogoo na genge hilo hilo unalosema hulitaki,leo umeolewa ndo unawaona wabaya eti 'wataniharibu'? waniharibu nimekuwa gari au picha ya ukutani?

5.'Kwa nini unanirudia saa hizi'(with legs akimbo),embu nikuulize hii nyumba yangu yako?

.........nitaendelea ngoja nishushe munkari kwanza.........

...ha ha ha, punguza munkari mkuu.
Hupo peke yako, ni 'pingu za maisha hizo!'
 
Bishanga umetoka msibani juzi tu ushaanza makeke sio? Mkeo yuko sawa unafikiri akikaa kimya bilakukuuliza hivo utasikia raha kweli? Raha ya mapenzi uulizwe ulikuwa wapi uonyeshwe kila dalili ya wivu. Respect each other na value chochote anachokuambia mwenzako. Embu fikiria unarudi saa nane unakuta mke enekuchekea tu si utaanza kuhisi ana mwanaume mwingine? Vitu vingine huwezi kuvikwepa kwenye ndoa. Na unavyosema hajaweka tofali kwenye nyumba hapo ndio ulipo niboa kabisa na kunionyesha upo mwanaume wa aina gani. Hatufanyi hivo kwenye uhusiano.
 
Kwa tabia hizi mnafikiri tutawataka, bora twende na vibabu vya kizungu hata vinatusikiliza kuliko nyie mnakuja usiku hamtaki kuulizwa, huko bar mnakaa kaa na vimada mkiulizwa vita, ahaha nimechoka, eti mwingine anashauri utafute nyumba ndogo imekula kwenu, ningemuona huyo mkeo ningempa dili la kupata mzungu ndio ungejua. Weka namba ya simu ya huyo mkeo alete na picha uone mambo. Acheni hizooo zimepitwa na wakati. Mke au mume kila mmoja natakiwa kupewa heshima, Acha mfumo dume. Tena endeleeni tu, tutawawekea na mazamu ya kufua kupika na kunyonyesha we ngoja. eti unampa kila kitu sijui gari watoto unatunza sijua full tank WHAT IS THAT? Alitoka kwao kwa ajili yako sio vitu. Mbona vitu tunaweza kutafuta tu. kwa kwa vile tunawaheshimu bana. KATAFUTE NJIA YA KUELEWANA NA MKEO ACHA UONEVU. NIKIMUONA TU NAMPA DILI LA MMBABU WA KIZUNGU.

Mimi ni mwanaume lakini siungi mkono kuongeza mke ili upate heshima. Kadhalika siungi mkono mwanamke kutafuta Kenny Rogers (Mbabu wa kithungu) ili kutafuta heshima. Ikitokea hivyo kuna tatizo kwa anayetoka nje kwenda kutafuta heshima awe mwanamke au mwanaume.
 
...ha ha ha, punguza munkari mkuu.
Hupo peke yako, ni 'pingu za maisha hizo!'
Hizi ndoa za siku hizi bana eti hajaweka tofali how can he say something like that?
 
Mimi ni mwanaume lakini siungi mkono kuongeza mke ili upate heshima. Kadhalika siungi mkono mwanamke kutafuta Kenny Rogers (Mbabu wa kithungu) ili kutafuta heshima. Ikitokea hivyo kuna tatizo kwa anayetoka nje kwenda kutafuta heshima awe mwanamke au mwanaume.
Kwa mwanamme kama huyu asiyetaka kuulizwa chochote ili mkewe anyamaze kabisa ni lazima awe na mtu pembeni hapo atanyamaza kimya
 
Its my fu.....g house,hajaweka tofali hapo!

...astaghafirullah,...taratibu bana. Mlisainishana pre nuptials?
'vuvuzela' zikizidi piga miluzi ya..." ♪ chaupele mpenzi,...♫" :whistle::whistle::whistle:...
 
Kwa mwanamme kama huyu asiyetaka kuulizwa chochote ili mkewe anyamaze kabisa ni lazima awe na mtu pembeni hapo atanyamaza kimya

Mbona hamjamuuliza anaoneshaje mapenzi kwa mke wake, au ni mwanamke tu ndiyo anatakiwa kuonesha mapenzi kwa kunyenyekea na kutokuuliza maswali
 
Yeah kuku wa kienyeji wanahusika sana Bishanga hawa wa mboga 7 mimi nilisha nyosha mikono unaletewa mapenzi ya ISIDINGO

...na kulazimishwa uangalie/usimuliwe visa vya kina María Clara, LOL!

Alafu hivi ni kwa nini nyie wanawake kabla ya kuolewa huwa mnakuwa wanyenyekevu sana mkisha fika ndani mnakuchunjua makucha yenu kwa nini hivi?
Sa tukikunjua makucha kabla ya kuolewa, tutaolewa kweli jamani?

...mnh, akheri yako sweetlady umekuwa mkweli.
 
Kwa mwanamme kama huyu asiyetaka kuulizwa chochote ili mkewe anyamaze kabisa ni lazima awe na mtu pembeni hapo atanyamaza kimya

hili swala na "nyumba yangu" limetia ndoa nyingi sana kwenye misukosuko. Bishanga anaamini kwamba kwa kuwa nyumba ni yake basi ana haki ya kurudu usiku anaoutaka na kila kiumbe kinachoishi katika nyumba yake ni furniture, including mke wake
 
Its my fu.....g house,hajaweka tofali hapo!

Mhhhh! Bishanga! Yes! it is your ****ing house, lakini kwenye ndoa kuna kitu kinaitwa COMPROMISE bila kuwepo kitu hiki ndani ya ndoa basi ndoa hiyo haina maisha marefu Mkuu. Usilalame tu atakapoamua kufunga kila kilicho chake na kukuachia "your ****ing house" ili uwe na uhuru wa kufanya lolote lile.
 
bi shanga unaonyesha huna mapenzi na huyo mke wako.huyo mke anataka attention kutoka kwako,na mapenzi ya dhati ajihisi kama na yeye anapendwa.kumjazia mafuta kwenye gari,kula vizuri watoto kupelekwa shule nzuri hiyo haitoshi.wanawake wangapi wanakuwa na kila kitu ndani,wanakosa mapenzi,mbio wanatafuita vijana wa pembeni wasio na mbele wala nyuma.ndoa zina mlolongo mrefu.mshukuru huyo mke kukwambia,badilika uone kama ataendelea kulalamika
 
Wacha niondoke zangu,kawaida huwa nakunywa ndovu,leo ntapiga konyagi iliyochanganywa na amarula kisha ntajua la kufanya. nshachoka mimi.

...Shabaashh! suluhisho lipo hapo. Piga simu wife awapeke watoto kwa shangazi na yeye asichelewa kurudi!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom