Hivi mnataka mpendejwe?

Bishanga

JF-Expert Member
Jun 29, 2008
15,323
10,063
Kuna siku nilimwaga hapa mikero kibao ya kinamama,mimgine hii hapa:

1. Mara akwambie oh Ex wangu alikuwa hivi mara vile,ya nini yote bana? mbona mliachana sasa?

2.'We nae mpira tu kila siku',maneno gani ya kunambia hayo? Fikiria kesho Man U anakipiga na Chelsea halafu nikitaka kwenda pub nikaangalie unaniletea za kuleta,nikisema nikae mnaweka mi tamthiliya yenu,is it fair,saloon mbona sikuzuii kwenda?

3.Mara oh 'naona mapenzi yamepungua' mwanzo yalikuwa kilo ngapi na sasa kilo ngapi?yamepungua kivipi umeyapima na nini? kwa nini unanipa mastress ya kukuonyesha mapenzi,si uache ya flow tu,mwisho nitakuwa mnafiki!

4.'Sipendi marafiki zako hao'.Alllaaaa yamekuwa hayo? Enzi ya uchumba tunajirusha hadi majogoo na genge hilo hilo unalosema hulitaki,leo umeolewa ndo unawaona wabaya eti 'wataniharibu'? waniharibu nimekuwa gari au picha ya ukutani?

5.'Kwa nini unanirudia saa hizi'(with legs akimbo),embu nikuulize hii nyumba yangu yako?

.........nitaendelea ngoja nishushe munkari kwanza.........
 
Pole, hebu shusha munkari manake wife kakupatia kweli kweli. Nyumba ni yetu na utafuata vile nnavyotaka mimi. Sawa? Huna ujanja kubali tu yaishe.
 
nguvu ya mamba iko mumayi,we subiri atakapokuwa kuwa nje ya ndoa ndo atajua........
 
Umemuuliza mhusika hayo maswali??Maana yeye tu ndo mwenye majibu ya uhakika yatakayoshusha huo munkari .

Still chunguza ndoa yako ilivyo sasa tofautisha na kipindi cha uchumba....labda kumekua na mabadiliko sana.Kama unavyoona yeye kabadilika ndivyo nae anavyoona na wewe umebadilika!Tatizo hapa ni kwamba hamkubadilika pamoja alafu wote ni wale watu wasioweza/jua kuishi na kukubali mabadiliko.Mtabaki kunyoosheana vidole badala ya kila mmoja kujiangalia mwenyewe kwanza na kujirekebisha kabla ya kutaka kumrekebisha mwenzako!Kaeni chini mjadiliane matatizo ya kila mmoja wenu kiungwana ndo mtayamaliza!
 
huwa mnasikiliza nyie?si mnataka muongee wenyewe tu sisi tusikilize?
 
Kwani kuna ubaya kumsikiliza mkeo? Na kama anachokuambia kina faida kwa ndoa yenu kwa nini unakasirika? Unataka uambiwe na nani? Mke na Mume kusikilizana bana. Msikilize mwenzio, acha kiburi cha MIMI ni mwanaume WEWE ni mwanamke.
 
ungekuwa mke wangu wewe jumatatu usingeenda kazini.....juu ya nini mke kumjibu mme?
 
Hahahahahaha. Una kiburi wewe. Unataka kumkandamiza mkeo! Una bahati hujawa mume wangu, nngehakikisha unanyooka kwenye mstari. Wewe uongee tuuuuuuuuu mwenzio akae kimya! Kisa? MUME. Na yeye si MKE? Mpe nafasi mkeo, vinginevyo kama anakudharau, ila kama anakushauri kwa heshima na Upendo kwa nini usimsikilize?? Punguza munkar basi Shem.
 
Pole, hebu shusha munkari manake wife kakupatia kweli kweli. Nyumba ni yetu na utafuata vile nnavyotaka mimi. Sawa? Huna ujanja kubali tu yaishe.
Its my fu.....g house,hajaweka tofali hapo!
 
Hahahahahaha. Una kiburi wewe. Unataka kumkandamiza mkeo! Una bahati hujawa mume wangu, nngehakikisha unanyooka kwenye mstari. Wewe uongee tuuuuuuuuu mwenzio akae kimya! Kisa? MUME. Na yeye si MKE? Mpe nafasi mkeo, vinginevyo kama anakudharau, ila kama anakushauri kwa heshima na Upendo kwa nini usimsikilize?? Punguza munkar basi Shem.
tatizo too much u beijing!hela ntafute mimi,nduguzo nikutunzie,watoto full matunzo,halafu unaleta lomo!
 
Its my fu.....g house,hajaweka tofali hapo!
Hahahahaha. Hajaweka tofali lakini ni MKE. Kwa hiyo mke asipoweka tofali kwenye nyumba inabidi awe msikilizaji tu hata kama anaona mambo hayaendi sawa ndani ya nyumba?
 
Kama mwanaume hutakiwi kushindwa kumfanya mke wako akusikulize.Acha kumfokea kama mtoto badala yake ongea nae kama mke wako ambae ni mtu mzima!
utaongea saa ngapi wakati ye anachonga kaa kasuku,naenda zangu mie kuutwika ntajua huko huko.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom