Hivi Mishahara ya May 2019 ilishatoka ama bado?

Hivi Mishahara ya May 2019 ilishatoka ama bado?

Mkuu utumishi kwa nchi masikini kama Tanzania ni taabu sana ona watumishi akili yote inawaza mshahara kama umetoka sipati picha siku usipotoka watumishi watakuwa na hali gani
Ulitaka asiuwaze hata ambaye amejiwekeza pia anauwaza anavitu vya kufanyia
 
Alafu mshahara wenyewe anaousubiria unaweza kuwa 231,765.00
Fanya mpango utengeneze another stream of income. Kuishi kwa kutegemea ka mshahara kiduchu tu ni risk kubwa hasa pale unapopatwa na emergency. Yaani maisha design hii ya “hand-to-mouth” bila akiba yoyote ni janga kuu
 
Wakati wa kuongelea mambo ambayo ni muhimu sana lazima mtazame na mnachokiongea je, kina maana? Unajua masuala ya mishahara ilishatolewa ufafanuzi na sasa mnachofanya baadhi yenu ni kutia doa na kuchafua tu. Naomba tuwe na nidhamu na viongozi wakubwa wa nchi yetu hata kama tunaanzisha mada lazima tutazame je, ina umuhimu gani? Mishahara pamoja na umuhimu wake ila sio jambo muhimu sana kuchafua watu na kuleta tarehe zenu mnazojipangia wenyewe kama ndio mnaojua siri ya mishahara ya wafanyakazi na utokaji wake. Tuwaachie wanaojua ambao ni viongozi wakubwa kuliko kubwatuka wakati tarehe bado hazijavukwa za kutoa mishahara. Mkumbuke mwezi wa 4 ulikuwa na "PASAKA" na angeamua Raisi kufata taratibu zake tu bila kutazama ubinadamu na umuhimu wa siku hiyo angeamua kutoa Jumanne ambayo ni tarehe 23 ama Jumatano ambayo ni tarehe 24. Pamoja na huruma zake zote na upendo wa hali ya juu sana kwa wananchi na wafanyakazi wake alitoa pesa siku ya Ijumaa kuu na ukumbuke ilikuwa siku ya mapumziko akaamua asipumzike ila atoe pesa. Hapo ndipo utajua Raisi wetu ni mtu mwema sana na anatupenda sana watu wake. Naomba tuwe na heshima na nidhamu kwake na kwa viongozi wengine huenda tukafanikiwa sana. Hata tukiwa tunasema ovyo hatujengi lolote.
Nawasilisha.
Ikiwa nimekukwaza naomba ujirekebishe.

Raisi ndo anatoa mshahara...!!! Au kujifanya una hasira ndo itabadili nini.... huijui njaa pumbavu wewe toeni hela.
 
Dah watu mna dharau aisee .. MWALIMU ndo aliyenfundisha babu yako , bibi yako, mama yako, baba yako..mke wako, watoto wako, wajomba zako, n.k leo unawadharau

Mkuu walimu wamejidharaulisha wenyewe pamoja na serikali yao, wametufundisha sawa na tunategemea wafundishe watoto wetu ila sio dhambi kusema ukweli kuwa kada ya ualimu ndio duni kuliko zote.... hata mkiwaziba mdomo bado haitobadili ukweli huo.
 
Mkuu walimu wamejidharaulisha wenyewe pamoja na serikali yao, wametufundisha sawa na tunategemea wafundishe watoto wetu ila sio dhambi kusema ukweli kuwa kada ya ualimu ndio duni kuliko zote.... hata mkiwaziba mdomo bado haitobadili ukweli huo.
Halafu unawezakuta wewe ni slay queen huna hata kazi
 
Wakuu, naomba kuuliza...Mishahara ilitoka au bado?

Now nipo shambani, sipo karibu na Bank. Naomba mnifahamishe ndugu zangu.
Kama wewe uko shambani, mshahara wa mwezi mei unalipwa na nani ?
 
Hamna hivi kati ya payroll na salary slip kipi kinatoka cha kwanza
[/QUOTE
Inaanza payroll salary slip uja badaye ndo maana unaweza maliza mwezi bila kupata salary slip ya mwezi uliopita. Ila uwezi kupata mshahara bila kuwepo payroll.
 
Back
Top Bottom