Mwanamayu
JF-Expert Member
- May 7, 2010
- 11,349
- 6,476
Jana kwenye redio Ujerumani Bi. Sara Batilda Burian aliulizwa alivyomfahamu marehemu Wangari, akasema alikuwa jasiri na kuweza kupambana na "mfumo dume" uliopo duniani. Nikapata maswali mengi: hivi nje ya dunia kuna "mfumo jike"? Hivi nini maana ya dhana hii - mfumo dume? Hivi huku sio kusigina Bible? Je, ana-question kazi na maagizo ya kwenye Bible? Je, 'mfumo jike' ukoje? au mfumo 'mseto - jike+dume ukoje?