Hivi Mbowe hili unalionaje?

Hivi bado kuna watu wanasoma Tanzania Daima?

Sijui siku JK akimaliza ungwe yake wataandika nini?
 
Ukisoma makala za Kibanda, Ngurumo na wachangiaji wengine utaona kwamba gazeti hili limepoteza mvuto, weledi na kuaminika kwake. Sasa hivi ukiona habari katika gazeti hili unajiuliza mara mbili mbili juu ya kuaminika kwake.

Mkuu Mbopo,
Msalimie BOLLEN NGETTI na DEODATUS BALILE
 
Mheshimiwa Mbowe ni muumini mzuri sana wa uhuru wa vyombo vya habari na hii inajidhihirisha katka namna ambavyo ameliacha gazeti lake la Tanzania Daima kufanya kazi yake bila ya kuingiliwa. Policy hii ya hands off, ni nzuri na ni nguzo muhimu sana ya uhuru wa vyombo vya habari hasa katika nchi za dunia ya tatu ambako wamiliki wana nguvu sana. Hii ililipa heshima gazeti la Tanzania Daima na nina hakika mauzo yake yaliongezeka sana.

Kwa bahati mbaya sana aina hii ya utawala imetumiwa vibaya na mawakala wa ufisadi na washabiki wa siasa za kihafidhina ambao wametanda katika news room ya gazeti hili na sasa gazeti hili limegeuka kuwa ni mdomo wa mafisadi, sauti ya ukinzani usio na tija dhidi ya serikali na hasa Rais wa nchi na upotoshaji wa kijinga sana. Ukisoma makala za Kibanda, Ngurumo na wachangiaji wengine utaona kwamba gazeti hili limepoteza mvuto, weledi na kuaminika kwake. Sasa hivi ukiona habari katika gazeti hili unajiuliza mara mbili mbili juu ya kuaminika kwake. Hali hii sasa inaonekana kuwakera hata baadhi ya watumishi wa gazeti hili, na mfano mzuri ni makala ya Happiness Katabazi ya gazeti la tarehe 3 Julai, 2012 ambayo alielezea juu ya mgomo wa madaktari. Alishutumu jinsi makala zake mbili ambazo kimsimamo zinatofautiana na 'watawala' wa news room ya gazeti walivyoziminya kiasi cha kuhisi kwamba hata hiyo nayo isingetoka.

Kama hili linamtokea mwenzao ambaye msimamo wake au fikra zake ni tofauti, vipi kwa wengine?

Swali langu ni je, Mheshimiwa Mbowe haya anayajua?

Comrade Mbopo,

Nilitaka niaanze kukuasa kwamba jaribu ku-deal na kitengo chako cha Habari hapo Foreign Affairs uongeze weledi zaidi nikaona utahamaki...nimeghairi

Wakuu wengine hapo juu baadhi yao wameacha kuwa objective.Emotions zimemwagika mno....tutulie

Hata Hivyo nirudi kwako Mbopo,Naona unataka kuturudisha kule kule tusikotaka.Kwamba unataka wamiliki wa vyombo vya habari waingilie vyombo vyao?na ofcourse bado kwa Tanzania hi ni changamoto kubwa na wakati mwingine demokrasia yetu inadumaa kwa sababu za baadhi ya wamiliki kuingilia vyombo vya habari.Niliankufurahia kuona tunatoka huko lakini mkuu kumbe wewe unataka turudi huko.Sikutegemea mtizamo huu kwa mtu wa level yako mkuu.Umeni-dissapoint leo

NB: Hebu rejea kwenye ile thread ambayo Membe ametoa majibu yenye utata kuhusu meli za Iran na Bendera ya Tanzania huku akijinadi amezingatia Resolution 920.Sijui hii Resolution na wajibu alioutaja Membe zinaingiliana vipi katika hili suala.Zanzibar inavuka mpaka na kukanyaga serikali ya Muungano katika medani za kimataifa.Naona series ya comments itafuata hapa.Someni angalao maandishi latest on 'intergrating UN-Sanctions for peace and security' iya akina David Cortright, George A. Lopez, and Linda Gerber-Stellingwerf, with Eliot Fackler and Joshua Weaver .Hii project ya Tanzania Daima haitawasaidia sana muda huu
 
Hivi kama ni kweli gazeti la Tanzania Daima linachungulia kaburi, hayo magazeti mengine anayoyasifia Mbopo ni yapi? Hayo magazeti mengine yanayopendwa zaidi ya Mwananchi na Tanzania Daima ni yapi? Hayo magazeti mengine yanayoweza kujiendesha bila ruzuku (matangazo ya serikali) zaidi ya Mwananchi na Tanzania Daima ni yapi? Binafsi kwa magazeti ya kila siku ya Kiswahili, pesa yangu ikitoka ni kununua magazeti mawili tu, Mwananchi na Tanzania Daima na kwa magazeti ya kila wiki Raia Mwema na Mwanahalisi, period. Hayo mengine sina habari nayo na hata yakifa hakuna ninachopoteza lakini kwa haya mawili niko tayari hata kuchangia, Mbopo upo?
 
Yako mambo ya kipuuzi yasiyopaswa kupuuzwa. Mafisadi anaowazungumzia huyo mpuuumbavu Hao mafisadi wanaoingilia makala za Kibanda na Ngurumo ni akina nani? Yaani anadhani Mbowe ni mpuuuzi wa kiwango chake? Yaani anataka kuuaminisha umma kwamba makala aliyoiandika Happiness Katabazi ndiyo mwelekeo wa Tanzania Daima? Hivi kwa akili yake anadhani Mbowe anaunga mkono ukatili wanaofanyiwa madaktari? Yaani anadhani Mbowe anaweza akakubaliana na makala ya Katabazi? Hebu afuatilie Bunge na aujue msimamo wa Chadema kuhusu mgomo wa madaktari na serikali.

Nasikitishwa na watu waliofikia hatua ya kumtusi hadi Mbowe kwa sababu tu ya kuwaunga mkono wapuuzi wa aina ya mwandishi wa thread hii ambaye ni miongoni mwa watu wanaotumia vibaya uhuru wa kupost thread katika jamvi hili kwa kuandika mambo ya hovyo kwa kiwango hiki.

Kwa taarifa yenu, Tanzania Daima halitakufa na halifi na kwa sasa linashika nafasi ya pili kwa mauzo baada ya gazeti la Mwananchi. Serikali ya kifisadi ambayo mwandishi wa thread anaisifia imefanya juhudi kubwa kuliua gazeti hili kwa kulinyima matangazo lakini hata hivyo ndani ya serikali hiyo wako watu waadilifu na wachapakazi ambao hawajapata kutishwa na wamekuwa wakiendelea kutangaza nasi.

Mimi ndiye Kibanda ambaye ni mhariri mtendaji wa Tanzania Daima. Niko hapa si kwa kubebwa bali kwa kujibeba kwa sifa na vigezo. Niko tayari kuondoka hapa wakati wowote iwapo mwajiri wangu ataona huo ndiyo uamuzi sahihi kwake. Viwango vyangu vinanipa fursa ya kufanya kazi katika gazeti lolote lile makini.

Ni kweli Tanzania Daima haliwezi kufa maana gharama za uendeshaji ni ndogo mno.
Hamuwalipi waandishi wenu isipokuwa wale wadada walioletwa hapo na Mbowe kwa sababu zake binafsi.
Usiwadanganye watu, hilo gazeti haliuziki.
Stori zenu ni za hewani hewani na kama huo ndio utaalam wako basi pole maana Shigongo hana vacancy iwapo utaondoka Bilicanas.
Sijali mko upande gani wa siasa, gazeti of course ni la Chadema-Machame.
Chadema-Mbulu hamuwasapoti sana.
Ila wewe Kibanda ni mfuasi mwaminifu wa Kikwete, pengine uko neutral.
 
Hivi kama ni kweli gazeti la Tanzania Daima linachungulia kaburi, hayo magazeti mengine anayoyasifia Mbopo ni yapi? Hayo magazeti mengine yanayopendwa zaidi ya Mwananchi na Tanzania Daima ni yapi? Hayo magazeti mengine yanayoweza kujiendesha bila ruzuku (matangazo ya serikali) zaidi ya Mwananchi na Tanzania Daima ni yapi? Binafsi kwa magazeti ya kila siku ya Kiswahili, pesa yangu ikitoka ni kununua magazeti mawili tu, Mwananchi na Tanzania Daima na kwa magazeti ya kila wiki Raia Mwema na Mwanahalisi, period. Hayo mengine sina habari nayo na hata yakifa hakuna ninachopoteza lakini kwa haya mawili niko tayari hata kuchangia, Mbopo upo?

Hivi wewe usingenunua Tanzania Daima ungekuwaje? that is obvious..

Tanzania Daima = Uhuru; wanunuzi wa magazeti haya wanajulikana wana mrengo gani wa kisiasa..

Daima for chadema; uhuru for ccm
 
Ruzuku ya Aga-khan na Hard Rock Cafe haziendi kwenye magazeti mengine.
Hakuna gazeti linalotegemea ruzuku ya serikali ni uvumi ulioenezwa makusudi ili uaminiwe na watu kama ninyi.
Nadhani hata Loliondo kwa babu ulienda na pia leaders kumzika Kanumba maana simple minds wote walikwenda
 
Comrade Mbopo,

Nilitaka niaanze kukuasa kwamba jaribu ku-deal na kitengo chako cha Habari hapo Foreign Affairs uongeze weledi zaidi nikaona utahamaki...nimeghairi

Wakuu wengine hapo juu baadhi yao wameacha kuwa objective.Emotions zimemwagika mno....tutulie

Hata Hivyo nirudi kwako Mbopo,Naona unataka kuturudisha kule kule tusikotaka.Kwamba unataka wamiliki wa vyombo vya habari waingilie vyombo vyao?na ofcourse bado kwa Tanzania hi ni changamoto kubwa na wakati mwingine demokrasia yetu inadumaa kwa sababu za baadhi ya wamiliki kuingilia vyombo vya habari.Niliankufurahia kuona tunatoka huko lakini mkuu kumbe wewe unataka turudi huko.Sikutegemea mtizamo huu kwa mtu wa level yako mkuu.Umeni-dissapoint leo

NB: Hebu rejea kwenye ile thread ambayo Membe ametoa majibu yenye utata kuhusu meli za Iran na Bendera ya Tanzania huku akijinadi amezingatia Resolution 920.Sijui hii Resolution na wajibu alioutaja Membe zinaingiliana vipi katika hili suala.Zanzibar inavuka mpaka na kukanyaga serikali ya Muungano katika medani za kimataifa.Naona series ya comments itafuata hapa.Someni angalao maandishi latest on 'intergrating UN-Sanctions for peace and security' iya akina David Cortright, George A. Lopez, and Linda Gerber-Stellingwerf, with Eliot Fackler and Joshua Weaver .Hii project ya Tanzania Daima haitawasaidia sana muda huu

Ben, mimi si-advocate wamiliki kuingilia kazi au uhuru wa vyombo wanavyovimiliki. Nilichomuuliza Mbowe na kikajibiwa kwa jazba kali sana na Mhariri Mtendaji ni iwapo anafahamu kwamba aina ya uandishi wa gazeti lake ni suicidal na kwa kiasi kikubwa limepunguza mvuto wake, na pengine mauzo yake? Mimi nilichukua malalamiko ya Katabazi kuwa ndiyo uthibitisho kwamba mawazo kinzani katika gazeti hili, ambayo yanakwenda kinyume na falsafa na itikadi ya wahariri na pengine na mmiliki, hayana nafasi na hayavumiliwi kamwe. Falsafa hiyo ni kusifia Chadema na wateule wachache wa CCM hata pasipostahili na kumshambulia Rais, serikali yake na CCM hata pasipostahili.

Nilichoshuhudia ni kutoka kwa Mhariri Mtendaji ni juvenile way of responding to constructive criticism na ukosefu wa uvumilivu. Hii ni kuonyesha kwamba huyu bwana ni Mungu mtu asiye tayari kukosolewa na kwake yeye, kupingana ni uadui. Nimefurahi composure iliyoonyeshwana Ngurumo japo malalamiko ya kwamba Serikali imetaka kuliua gazeti ni common feature na sababu eti haipewi matangazo as if hiyo ni kazi ya serikali. Hivi Guardian wanapata matangazo ya Barrick na kampuni nyingi binafsi kwa msaada wa serikali? Hakuna ambacho kingeizuia serikali kuua gazeti hili, kama serikali hii ingekuwa muumini wakuua vyombo vya habari. Hii ingekuwa rahisi kutokana na mwenendo wa matusi dhidi yake ulioonyeshwa na gazeti hili.

Kum-disown na kumbeza Katabazi ni kuzidi kuonyesha kwamba kuna mabaya tusiyoyajua yanayoendelea humo ndani, lakini lililo wazi ni kwamba makala ya Katabazi imekuwa mwiba hata kwa mmiliki mwenyewe.

Rai yangu ni kwamba tupingane kwa hoja na siyo matusi ya wale wanaojifanya kuwa ni vinara wa kuelimisha umma.
 
Hivi bado kuna watu wanasoma Tanzania Daima?

Sijui siku JK akimaliza ungwe yake wataandika nini?

akili yako hainishangazi! Maswali unayouliza yanaonesha akili yako ilivyo fupi! Mwanzo ulijiita Mwita25, ukajiita atiwm52, Topical. Ulipoishiwa majina ukajiita Mbwa. Huitaji hata elimu ya kata kutambua akili, mchango, na mawazo yako ni ya aina gani!?
 
Naipenda Tz Daima, hata nikiwa huku ndani ndani nikalikosa copy, internet huwa nalipata vizuri..na halina habari nusu nusu kwny internet. Mimi naona kufa si rahisi, labda CHADEMA ife..cha msingi more creativity lazima iongezwe! Mwisho, sijaridhika n ujibuji wa hoja wa Mhariri Mtendaji ambaye pia ni mwenyekiti wa wahariri tanzania..plz calm down..watu kama Mbopo wapo kuharibu tu!
 
Fortunately message imefika na kuhemuka huku ni dalili kwamba yaliyokuwa dhana sasa hivi yamethibitishwa. Kibanda upende usipende unaliua gazeti kwa kudhani kwamba hiyo ni theatre ya ku-settle scores za watu dhidi ya serikali hii. Kwanza jazba na matusi uliyoyatoa humu, ambayo ni sifa nadra na isiyo ya kujivunia ya wahariri mahiri ni ishara kwamba yaliyosemwa ni ukweli unaochoma.

Nakushukuru hata hivyo kwa kuthibitisha kwamba hata Mbowe ana-share ideals hizo zinazoelekea kulididimiza gazeti hili kwa kaburi la sahau. Itafika wakati tuathitaji kujua ile ofisi ya gazeti la Umoja ulilosaidia kuliasisi inaendeshwa kwa fedha za nani.

Mimi sijali kama kuna mhariri aliyerekebisha kazi ya Katabazi maana hiyo ndiyo kazi ya mhariri wa habari au makala katika gazeti na nina hakika kazi za waandishi wengine hupitia mchakato huo huo. Naamini hata kazi nyingine za Katabazi amekuwa akirekebishwa hivyo hivyo, kwa nini hii ionekane ni ajabu? Suala hapa ni kwamba hata yeye mwenyewe amelalamika na hakuna kanusho kwamba gazeti hili limekuwa halipokea maoni yanayotofautiana na itikadi ya mhariri mtendaji au hata mmiliki wake. Katabazi amethibitisha tulichokuwa tunakishuku.

Nahukuru sana Kibanda, pamoja na jazba na matusi yako yanayoendelea kuonyesha ukosefu wa objectivity na tolerance yako, kwa kutujulisha kwamba kumbe wewe kamwe si mwandishi mwenye maadili. Una prejudices ambazo zinakufanya sasa uwe na stereo type kwamba kila anayekupinga ni CCM na kila CCM (isipokuwa wale unaowatumikia) ni mbaya au mbumbumbu. Kwa hakika ukweli unabaki kwamba Tanzania Daima ni aina ya magazeti ya Uhuru ambayo yanazidi kupoteza heshima na mvuto. Kama unasema Mbowe anajua haya basi nampa pole!

Kwanza unapaswa kujisifu kupata bahati kubwa ya kujibiwa na Kibanda! nikilinganisha uelewa wako katika tasnia nzima ya habari ulipaswa kupuuzwa,wakati mwenzako anajibu kitaaluma wewe unajibu ki-ukereketwa.Wapi na wapi wewe mjumbe wa 10?
 
Siasa sasa ni kila kitu, ukiingia kwenye siasa inakubidi UJIKANE mwenyewe! Nanichojua mimi hakuna unachoweza fanya kikawapendeza watu wote na Magazeti haya yanaandikwa na watu na si malaika wenye mawazo na itikadi tofauti, Na mi naamini mmiliki hawezi kuwa anawapangia kila kitu cha kuwemo kwenye gazeti,
 
Comrade Mbopo,

Nilitaka niaanze kukuasa kwamba jaribu ku-deal na kitengo chako cha Habari hapo Foreign Affairs uongeze weledi zaidi nikaona utahamaki...nimeghairi

Wakuu wengine hapo juu baadhi yao wameacha kuwa objective.Emotions zimemwagika mno....tutulie

Hata Hivyo nirudi kwako Mbopo,Naona unataka kuturudisha kule kule tusikotaka.Kwamba unataka wamiliki wa vyombo vya habari waingilie vyombo vyao?na ofcourse bado kwa Tanzania hi ni changamoto kubwa na wakati mwingine demokrasia yetu inadumaa kwa sababu za baadhi ya wamiliki kuingilia vyombo vya habari.Niliankufurahia kuona tunatoka huko lakini mkuu kumbe wewe unataka turudi huko.Sikutegemea mtizamo huu kwa mtu wa level yako mkuu.Umeni-dissapoint leo

NB: Hebu rejea kwenye ile thread ambayo Membe ametoa majibu yenye utata kuhusu meli za Iran na Bendera ya Tanzania huku akijinadi amezingatia Resolution 920.Sijui hii Resolution na wajibu alioutaja Membe zinaingiliana vipi katika hili suala.Zanzibar inavuka mpaka na kukanyaga serikali ya Muungano katika medani za kimataifa.Naona series ya comments itafuata hapa.Someni angalao maandishi latest on 'intergrating UN-Sanctions for peace and security' iya akina David Cortright, George A. Lopez, and Linda Gerber-Stellingwerf, with Eliot Fackler and Joshua Weaver .Hii project ya Tanzania Daima haitawasaidia sana muda huu

Hapo ni kwa kuwa gazeti linamilikiwa na mchagga mwenzako tu.hizo mbio zenu za ikulu zitawanyofoa roho

Ben, mimi si-advocate wamiliki kuingilia kazi au uhuru wa vyombo wanavyovimiliki. Nilichomuuliza Mbowe na kikajibiwa kwa jazba kali sana na Mhariri Mtendaji ni iwapo anafahamu kwamba aina ya uandishi wa gazeti lake ni suicidal na kwa kiasi kikubwa limepunguza mvuto wake, na pengine mauzo yake? Mimi nilichukua malalamiko ya Katabazi kuwa ndiyo uthibitisho kwamba mawazo kinzani katika gazeti hili, ambayo yanakwenda kinyume na falsafa na itikadi ya wahariri na pengine na mmiliki, hayana nafasi na hayavumiliwi kamwe. Falsafa hiyo ni kusifia Chadema na wateule wachache wa CCM hata pasipostahili na kumshambulia Rais, serikali yake na CCM hata pasipostahili.

Nilichoshuhudia ni kutoka kwa Mhariri Mtendaji ni juvenile way of responding to constructive criticism na ukosefu wa uvumilivu. Hii ni kuonyesha kwamba huyu bwana ni Mungu mtu asiye tayari kukosolewa na kwake yeye, kupingana ni uadui. Nimefurahi composure iliyoonyeshwana Ngurumo japo malalamiko ya kwamba Serikali imetaka kuliua gazeti ni common feature na sababu eti haipewi matangazo as if hiyo ni kazi ya serikali. Hivi Guardian wanapata matangazo ya Barrick na kampuni nyingi binafsi kwa msaada wa serikali? Hakuna ambacho kingeizuia serikali kuua gazeti hili, kama serikali hii ingekuwa muumini wakuua vyombo vya habari. Hii ingekuwa rahisi kutokana na mwenendo wa matusi dhidi yake ulioonyeshwa na gazeti hili.

Kum-disown na kumbeza Katabazi ni kuzidi kuonyesha kwamba kuna mabaya tusiyoyajua yanayoendelea humo ndani, lakini lililo wazi ni kwamba makala ya Katabazi imekuwa mwiba hata kwa mmiliki mwenyewe.

Rai yangu ni kwamba tupingane kwa hoja na siyo matusi ya wale wanaojifanya kuwa ni vinara wa kuelimisha umma.

Gazeti hilo ni la propaganda.wachagga wanajihisi ni wamiliki wa gazeti hilo.mbona mengi hafanyi upuuzi wa hawa watu?mengi ni mchagga aliyestaarabika sana
 
Hivi wewe usingenunua Tanzania Daima ungekuwaje? that is obvious..

Tanzania Daima = Uhuru; wanunuzi wa magazeti haya wanajulikana wana mrengo gani wa kisiasa..

Daima for chadema; uhuru for ccm

Topical

Usipotoshe. Ni rahisi sana wana-CCM kununua Tz Daima kila siku, kuliko mwana-CHADEMA kununua Uhuru mara moja kwa mwezi/miezi kadhaa mbali ya kukidhi interests zao mbalimbali (kwa wale open minded people) kwa kusoma kwenye mbao za kuuzia au kusikiliza redioni/kwenye Tv.

Wapo wana CCM wengi sana wanalazimika kulipenda Tz Daima kwa sababu haliandiki propaganda kama hilo gazeti jingine unalotumia kwenye comparison yako. Nape aliwahi kuthibitisha hilo kuwa wanalinunua sana Tz Daima.

Lakini pia SI SAHIHI KABISA kulinganisha Tz Daima na hilo gazeti jingine la CCM. Vitu viwili tofauti kabisa kama mbingu na ardhi. Hasa katika umiliki ambako watu wengi wameonekana kubeba na kutembea na misconception.

Mmiliki wa Tz Daima ni kampuni binafsi. Uhuru linamilikiwa na CCM. Lenyewe pamoja na Mzalendo, yanatumika kama mouthpiece ya CCM. Mdomo wa chama hicho tawala na serikali yake. Kutetea kila aina ya madudu na hata ikibidi kuonesha uongo wa chama hicho. Hata kama hilo linawalazimisha kukiuka maadili ya taaluma nyeti ya uandishi wa habari.

Hapo ni kwa kuwa gazeti linamilikiwa na mchagga mwenzako tu.hizo mbio zenu za ikulu zitawanyofoa roho

Gazeti hilo ni la propaganda.wachagga wanajihisi ni wamiliki wa gazeti hilo.mbona mengi hafanyi upuuzi wa hawa watu?mengi ni mchagga aliyestaarabika sana

Your utterance is reprehensible.
 
Ben, mimi si-advocate wamiliki kuingilia kazi au uhuru wa vyombo wanavyovimiliki. Nilichomuuliza Mbowe na kikajibiwa kwa jazba kali sana na Mhariri Mtendaji ni iwapo anafahamu kwamba aina ya uandishi wa gazeti lake ni suicidal na kwa kiasi kikubwa limepunguza mvuto wake, na pengine mauzo yake? Mimi nilichukua malalamiko ya Katabazi kuwa ndiyo uthibitisho kwamba mawazo kinzani katika gazeti hili, ambayo yanakwenda kinyume na falsafa na itikadi ya wahariri na pengine na mmiliki, hayana nafasi na hayavumiliwi kamwe. Falsafa hiyo ni kusifia Chadema na wateule wachache wa CCM hata pasipostahili na kumshambulia Rais, serikali yake na CCM hata pasipostahili.

Nilichoshuhudia ni kutoka kwa Mhariri Mtendaji ni juvenile way of responding to constructive criticism na ukosefu wa uvumilivu. Hii ni kuonyesha kwamba huyu bwana ni Mungu mtu asiye tayari kukosolewa na kwake yeye, kupingana ni uadui. Nimefurahi composure iliyoonyeshwana Ngurumo japo malalamiko ya kwamba Serikali imetaka kuliua gazeti ni common feature na sababu eti haipewi matangazo as if hiyo ni kazi ya serikali. Hivi Guardian wanapata matangazo ya Barrick na kampuni nyingi binafsi kwa msaada wa serikali? Hakuna ambacho kingeizuia serikali kuua gazeti hili, kama serikali hii ingekuwa muumini wakuua vyombo vya habari. Hii ingekuwa rahisi kutokana na mwenendo wa matusi dhidi yake ulioonyeshwa na gazeti hili.

Kum-disown na kumbeza Katabazi ni kuzidi kuonyesha kwamba kuna mabaya tusiyoyajua yanayoendelea humo ndani, lakini lililo wazi ni kwamba makala ya Katabazi imekuwa mwiba hata kwa mmiliki mwenyewe.

Rai yangu ni kwamba tupingane kwa hoja na siyo matusi ya wale wanaojifanya kuwa ni vinara wa kuelimisha umma.
Mbopo,
Kama unampenda na kumwonea huruma sana Katabazi, muajiri basi huko kwenye kitengo chenu cha habari hapo Foreign.
Atawafanyia kazi nzuri.
 
Hivi huyu Katabazi si ndio alikuwa mbeba vibahasha flani vilivyowahi kuzua zogo humu? Au vile vilikuwa clean?
 
Hapo ni kwa kuwa gazeti linamilikiwa na mchagga mwenzako tu.hizo mbio zenu za ikulu zitawanyofoa roho

Gazeti hilo ni la propaganda.wachagga wanajihisi ni wamiliki wa gazeti hilo.mbona mengi hafanyi upuuzi wa hawa watu?mengi ni mchagga aliyestaarabika sana

Wewe ilibidi uzaliwe Kenya maana unaunadi sana ukabiala.Ukabila umeingiaje hapo?
 
Back
Top Bottom