Hivi Mbowe hili unalionaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi Mbowe hili unalionaje?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mbopo, Jul 4, 2012.

 1. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #1
  Jul 4, 2012
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mheshimiwa Mbowe ni muumini mzuri sana wa uhuru wa vyombo vya habari na hii inajidhihirisha katka namna ambavyo ameliacha gazeti lake la Tanzania Daima kufanya kazi yake bila ya kuingiliwa. Policy hii ya hands off, ni nzuri na ni nguzo muhimu sana ya uhuru wa vyombo vya habari hasa katika nchi za dunia ya tatu ambako wamiliki wana nguvu sana. Hii ililipa heshima gazeti la Tanzania Daima na nina hakika mauzo yake yaliongezeka sana.

  Kwa bahati mbaya sana aina hii ya utawala imetumiwa vibaya na mawakala wa ufisadi na washabiki wa siasa za kihafidhina ambao wametanda katika news room ya gazeti hili na sasa gazeti hili limegeuka kuwa ni mdomo wa mafisadi, sauti ya ukinzani usio na tija dhidi ya serikali na hasa Rais wa nchi na upotoshaji wa kijinga sana. Ukisoma makala za Kibanda, Ngurumo na wachangiaji wengine utaona kwamba gazeti hili limepoteza mvuto, weledi na kuaminika kwake. Sasa hivi ukiona habari katika gazeti hili unajiuliza mara mbili mbili juu ya kuaminika kwake. Hali hii sasa inaonekana kuwakera hata baadhi ya watumishi wa gazeti hili, na mfano mzuri ni makala ya Happiness Katabazi ya gazeti la tarehe 3 Julai, 2012 ambayo alielezea juu ya mgomo wa madaktari. Alishutumu jinsi makala zake mbili ambazo kimsimamo zinatofautiana na 'watawala' wa news room ya gazeti walivyoziminya kiasi cha kuhisi kwamba hata hiyo nayo isingetoka.

  Kama hili linamtokea mwenzao ambaye msimamo wake au fikra zake ni tofauti, vipi kwa wengine?

  Swali langu ni je, Mheshimiwa Mbowe haya anayajua?
   
 2. n

  ndutu Member

  #2
  Jul 4, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 90
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hili gazeti na lile la Mwanahalisi sasa yanachungulia kaburi. Walilewa sifa na tamaa za wahariri wao sasa zinayatafuna magazeti haya. Mbowe ajue kwamba gazeti likifa hao wanaoliua watahamia gazeti lingine na kumuacha yeye akishangaa.
   
 3. T

  Tiote Senior Member

  #3
  Jul 4, 2012
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 139
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sijui madhumuni ya kuanzishwa kwa gazeti hili. Maana kama lengo lingekuwa ni kulifanya listawi, wale wanaojiiypta wahariri walitakiwa kufukuzwa siku nyingi.
   
 4. b

  banyimwa Senior Member

  #4
  Jul 4, 2012
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 117
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Afanye nini naye amelegezwa kwa rushwaya mafisadi?
   
 5. Ndumbayeye

  Ndumbayeye JF-Expert Member

  #5
  Jul 4, 2012
  Joined: Jan 31, 2009
  Messages: 4,784
  Likes Received: 1,038
  Trophy Points: 280
  hilo tumeliacha kitambo tunafungia samaki ferry
   
 6. m

  mudavadi Member

  #6
  Jul 4, 2012
  Joined: Apr 19, 2011
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hata kufungia samaki ni kulipa hadhi. Halifai hata kusokotea tumbaku.
   
 7. w

  watenda Member

  #7
  Jul 4, 2012
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 73
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Lilikuwa mahsusi kwa ajili ya kumpigia debe kwenye urais wake wa 2005. Baada ya kubwagwa ameamua kuliacha lijifie kifo cha taratibu. Vinginevyo ni uchochoro wa kupokelea hela za mafisadi. Si nasikia mmoja wa wale ampacha watatu wanalipia gharama za uendeshaji?
   
 8. c

  chama JF-Expert Member

  #8
  Jul 4, 2012
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 8,006
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mbowe naye ni fisadi tatizo yupo upande wa pili anaongea lugha ile ile

  Chama
  Gongo la Mboto DSM
   
 9. Asa'rile

  Asa'rile JF-Expert Member

  #9
  Jul 4, 2012
  Joined: Jun 29, 2012
  Messages: 426
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  ...........loading............
   
 10. M

  Mghaka JF-Expert Member

  #10
  Jul 4, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 320
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mimi ninatofauti kabisa na wengine lakini hili ni gazeti ambalo nisipolikuta kwa wauzaji wengine basi hapati na hela za magazeti mengine
   
 11. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #11
  Jul 4, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  hilo gazeti mbona mi naliona fresh tu, kumbe ni la mbowe nilikua hata sijui:wacko:
   
 12. Kibanda

  Kibanda Verified User

  #12
  Jul 4, 2012
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 87
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Yako mambo ya kipuuzi yasiyopaswa kupuuzwa. Mafisadi anaowazungumzia huyo mpuuumbavu Hao mafisadi wanaoingilia makala za Kibanda na Ngurumo ni akina nani? Yaani anadhani Mbowe ni mpuuuzi wa kiwango chake? Yaani anataka kuuaminisha umma kwamba makala aliyoiandika Happiness Katabazi ndiyo mwelekeo wa Tanzania Daima? Hivi kwa akili yake anadhani Mbowe anaunga mkono ukatili wanaofanyiwa madaktari? Yaani anadhani Mbowe anaweza akakubaliana na makala ya Katabazi? Hebu afuatilie Bunge na aujue msimamo wa Chadema kuhusu mgomo wa madaktari na serikali.

  Nasikitishwa na watu waliofikia hatua ya kumtusi hadi Mbowe kwa sababu tu ya kuwaunga mkono wapuuzi wa aina ya mwandishi wa thread hii ambaye ni miongoni mwa watu wanaotumia vibaya uhuru wa kupost thread katika jamvi hili kwa kuandika mambo ya hovyo kwa kiwango hiki.

  Kwa taarifa yenu, Tanzania Daima halitakufa na halifi na kwa sasa linashika nafasi ya pili kwa mauzo baada ya gazeti la Mwananchi. Serikali ya kifisadi ambayo mwandishi wa thread anaisifia imefanya juhudi kubwa kuliua gazeti hili kwa kulinyima matangazo lakini hata hivyo ndani ya serikali hiyo wako watu waadilifu na wachapakazi ambao hawajapata kutishwa na wamekuwa wakiendelea kutangaza nasi.

  Mimi ndiye Kibanda ambaye ni mhariri mtendaji wa Tanzania Daima. Niko hapa si kwa kubebwa bali kwa kujibeba kwa sifa na vigezo. Niko tayari kuondoka hapa wakati wowote iwapo mwajiri wangu ataona huo ndiyo uamuzi sahihi kwake. Viwango vyangu vinanipa fursa ya kufanya kazi katika gazeti lolote lile makini.
   
 13. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #13
  Jul 4, 2012
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,200
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  mambo meng yanayoandikwa humu yanafikirsha ...panueni fikra zenu na shughulisheni akili zenu....mmezoea jambo leo na uhuru
   
 14. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #14
  Jul 4, 2012
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,200
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280

  wengi hawaelewi humu...wamejaa ubishi usio na mantiki
   
 15. Kibanda

  Kibanda Verified User

  #15
  Jul 4, 2012
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 87
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Gazeti la Tanzania Daima ni gazeti huru. Tuko tayari kupokea mawazo na maoni tofauti na ya msingi. hawa wapotoshaji wa aina Mbopo walio tayari kupotosha, kupindisha ukweli na kutunga mambo kwa nia mbaya hawapaswi kuvumiliwa kwa hoja. Hatuwezi kujenga taifa imara kwa kuendekeza mawazo ya kipuuzi ya kiwango hiki cha Mbopo na wenzake.

  Eti anasikitishwa na hatua ya kumkosoa Kikwete halafu anadai eti huo ni msimamo wa karibuni. Halafu anajifanya kumshauri Mbowe ilhali akionyesha bayana kutojua msimamo wa Mbowe kuhusu mgogoro wa madaktari na serikali. huu ni upotoshaji uliovuka mipaka.
   
 16. Tumaini Makene

  Tumaini Makene Verified User

  #16
  Jul 4, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 2,617
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180

  [FONT=&amp]Hawa jamaa wanahangaika kweli kutafuta wa kufa naye. Hawataki kufa wenyewe peke yao. Wanajaribu kushika kila tawi, bahati mbaya si tu matawi yanateleza, bali yanakatika. CCM na serikali hii, itakufa yenyewe na vibaraka wake. Haitakwenda na wengine wasiojihusisha nayo, hasa katika matendo yake.

  Nawiwa kuchangia hapa kama mdau na mshirika mkubwa wa habari, kitaaluma na kazi za kila siku. Na pia nikiwa muumini wa hoja mbalimbali, zikiwemo za ukosoaji, ilimuradi ukosoaji usiwe kwa ajili/usilenge kupotosha!
  [/FONT]
  Kamanda mwanzisha thread unaonekana wazi hupatani na ukweli mkuu. Hata kama ulilenga kukosoa, basi ni vyema ungefanya hivyo bila kuonekana una dhamira ya kupotosha.

  Mtu makini akikusoma maeneo haya mawili pekee, anaweza ku-conclude na akaondoka;

  Unatarajia nani anaweza kukuamini hapa, bila kuonesha hilo kwa kinagaubaga?

  Unaijua vyema dhana ya "mouthpiece of...", unaijua vyema maana ya siasa za kihafidhina...au mwenzetu umejiandikia tu. Tanzania Daima na siasa za Kihafidhina!!! Du, are u serious kaka?

  "Ukinzani usio na tija dhidi ya serikali, hasa rais wa nchi na upotoshaji wa kijinga". Mkuu ukiyasema hayo maneno bila mifano, unakuwa umejikatia tiketi isiyolowana, kujipatia kiti cha kudumu kwenye timu ya wapiga debe wa milele wa Serikali ya CCM na Rais Kikwete. Labda inaweza kuwa kazi inayokufaa, kwa hoja hiyo.


  Kwanza Katabazi hakusema makala mbili. Alisema makama moja haikuchapishwa. Akaitaja hata kichwa cha habari alichoipatia. Hivi umejisumbua kuitafuta makala hiyo? Itafute uisome, kisha ndiyo uje hapa ujenge hoja zako, usipotoshe. Maana inapatikana kwenye blog yake. Makala ya ajabu kabisa. Hata mwanafunzi anayetoka darasa la saba leo, aliyebarikiwa tu uwezo mdogo wa kupanga maneno, angepewa topic hiyo aliyoandikia Katabazi, mtoto huyo asingeweza kuandika makala isiyokuwa na mtiririko wa hoja na mantiki hata kidogo kama ile...

  Mbali ya kuonekana unaendelea kuwa mpiga debe wa serikali ya Kikwete hata kwa kupotosha ukweli, lakini pia unaonekana hujui hata maana ya baadhi ya maneno uliyoyatumia "mvuto, kuaminika na weledi".

  Maana kama utaisoma makala aliyolalamika Katabazi kuwa haikuchapishwa, ungelazimika kufikiria mara mbili kuweza kuchukua kompyuta na kuthubutu kuisapoti huku ukisema ati anabaniwa na sasa Tanzania Daima inaonekana kupoteza mvuto, kuaminika na weledi kwa sababu ya makala za watu kama Ngurumo (Maswali Magumu) na Kibanda (Tuendako). Unless hujui maana ya maneno hayo.

  Tena bila shaka mhariri wa makala wa gazeti hilo alimsaidia sana Katabazi, maana kama makala ile ingetoka watu wangesema sasa Tanzania Daima sasa nalo limegeuka kuwa ni gazeti la watu wanaojifunza kuweka maneno mengi pamoja (si kuandika habari), kama ilivyo kwa magazeti mengine ambayo wananchi wanayafahamu.

  Bila shaka yoyote kama mwenyewe ulivyokiri...Kamanda Mbowe ni mtu makini. Hashindwi kuyaona matatizo (kama yapo) yanayoweza kuhitaji mmiliki wa chombo cha habari kulazimika kuachana na dhana ya 'hands off' na kuingilia masuala kadha wa kadha. Lakini si haya uliyoyasema wewe hapa tena sehemu kubwa kwa upotoshaji.
   
 17. k

  kasinge JF-Expert Member

  #17
  Jul 4, 2012
  Joined: May 22, 2011
  Messages: 1,259
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Ebuu soma vizuri, nadhani Tz Daima wako makini.
   
 18. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #18
  Jul 4, 2012
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Fortunately message imefika na kuhemuka huku ni dalili kwamba yaliyokuwa dhana sasa hivi yamethibitishwa. Kibanda upende usipende unaliua gazeti kwa kudhani kwamba hiyo ni theatre ya ku-settle scores za watu dhidi ya serikali hii. Kwanza jazba na matusi uliyoyatoa humu, ambayo ni sifa nadra na isiyo ya kujivunia ya wahariri mahiri ni ishara kwamba yaliyosemwa ni ukweli unaochoma.

  Nakushukuru hata hivyo kwa kuthibitisha kwamba hata Mbowe ana-share ideals hizo zinazoelekea kulididimiza gazeti hili kwa kaburi la sahau. Itafika wakati tuathitaji kujua ile ofisi ya gazeti la Umoja ulilosaidia kuliasisi inaendeshwa kwa fedha za nani.

  Mimi sijali kama kuna mhariri aliyerekebisha kazi ya Katabazi maana hiyo ndiyo kazi ya mhariri wa habari au makala katika gazeti na nina hakika kazi za waandishi wengine hupitia mchakato huo huo. Naamini hata kazi nyingine za Katabazi amekuwa akirekebishwa hivyo hivyo, kwa nini hii ionekane ni ajabu? Suala hapa ni kwamba hata yeye mwenyewe amelalamika na hakuna kanusho kwamba gazeti hili limekuwa halipokea maoni yanayotofautiana na itikadi ya mhariri mtendaji au hata mmiliki wake. Katabazi amethibitisha tulichokuwa tunakishuku.

  Nahukuru sana Kibanda, pamoja na jazba na matusi yako yanayoendelea kuonyesha ukosefu wa objectivity na tolerance yako, kwa kutujulisha kwamba kumbe wewe kamwe si mwandishi mwenye maadili. Una prejudices ambazo zinakufanya sasa uwe na stereo type kwamba kila anayekupinga ni CCM na kila CCM (isipokuwa wale unaowatumikia) ni mbaya au mbumbumbu. Kwa hakika ukweli unabaki kwamba Tanzania Daima ni aina ya magazeti ya Uhuru ambayo yanazidi kupoteza heshima na mvuto. Kama unasema Mbowe anajua haya basi nampa pole!
   
 19. Ngurumo

  Ngurumo Verified User

  #19
  Jul 5, 2012
  Joined: May 26, 2007
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  BAADHI yetu tumezoea kukosoa wengine. Hivyo, tunapokosolewa, hatuoni shida. Tatizo ni pale watu wanapotunga uwongo na kuufanya uwe ukweli. Inawezekana kuna ups and downs katika gazeti hili, kama ilivyo kwa biashara nyingine yote ile. Lakini ukweli ni kwamba gazeti hili limevuka vihunzi vingi vya serikali kuliua. Walio nje hawajui mikikimikiki tunayopitia. Hawajui jinsi tunavyojitoa sadaka kila siku. Hawajui hatari tunazokabiliana nazo kila siku. Lakini tumeendelea kufanya kazi inayoogopwa na wengi katika mazingira dhalili na dhalimu, yasiyo na sheria zinazowapatia ulinzi waandishi wa habari. Kwa taarifa, baadhi yetu tunafanya kazi kwa kutumia vichwa na mioyo yetu - si kwa ajili ya pesa tu. Tunaamini katika kile tunachoandika; na hatuogopi kukosolewa.

  Lililo wazi ni kwamba MHARIRI halazimiki kuruhusu kila kinacholetwa mbele yake; vinginevyo hana sifa ya kuwa mhariri. Baadhi ya kazi hukatwakatwa, nyingine huandikwa upya, nyingine hunyooshwa, nyingine hukataliwa ili ziandikwe upya, na nyingine hutupwa. Wanaolalamikia uamuzi wa mhariri kutupa au kuacha makala labda hawajui kwamba hiyo ni sehemu ya mamlaka yake ya kiutendaji. Mwandishi aliyebobea au anayejifunza, anaweza kuhoji sababu za makala au stori yake kutotumika ili ajifunze kutokana na makosa yake. Akili ya kawaida, uungwana na ustaarabu wa kitaaluma havituelekezi kwamba mwandishi anaweza kukataliwa makala au habari yake, halafu badala ya kuhoji na kujifunza, akaenda kulalamika hadharani dhidi ya uamuzi wa kiongozi wake; halafu akaanika "uchafu" ule ule ambao mkuu wake wa kazi aliufagia ili kulinda heshima ya mwandishi, mhariri na gazeti husika. Kama wapo wanaomsifu Happiness Katabazi kwa alichofanya, basi nao wana matatizo mengine tusiyojua. Sana sana, kama ni waungwana kama wanavyotaka tuamini, wangepaswa kuuliza, "amechukuliwa hatua gani" za kiutawala? Au "huyo aliyeipitisha bila kuihariri vile amechukuliwa hatua gani?"

  Nasisitiza: Gazeti la Tanzania Daima halifi. Waandishi na wahariri tutafika na kupita, gazeti litabaki; na halitasahaulika kwa mchango wake wa kuleta mageuzi ya fikra nchini. Nasi hatutasita kusema kwamba tumeshiriki kwa kiwango kikubwa kuleta mageuzi hayo. Ikumbukwe kuwa, licha ya ubabe na vitisho vya serikali, Tanzania Daima ni gazeti pekee ambalo limejiendesha kwa MAUZO badala ya kutegemea matangazo yanayodhibitiwa na serikali na wapambe wake. Wanaolitabiria kifo wanaweza kufa wakaliacha juu! Na wale wasiolifahamu au wasiotufahamu vema, waendelee kufanya utafiti. ANSBERT NGURUMO +255 719 001 001
   
 20. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #20
  Jul 5, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mkuu Ngurumo,
  Wewe ndiye Ansbert Ngurumo (Naibu Mhariri wa Tanzania Daima)? Naomba kufahamu tu maana nami ni miongoni mwa wasomaji wa muda mrefu wa MASWALI MAGUMU.

  TUMBIRI (PhD, University of HULL - UK),

  tumbiri@jamiiforums.com
   
Loading...