Hivi Mama wa kambo wanafundisha,wanatesa,au wanaharibu watoto????

lup

JF-Expert Member
Apr 23, 2015
2,514
2,732
Nisiwachoshe na utangulizi mrefu.
Naamini humu tupo tuliolelewa na mama wa kambo kwa mazingira tofauti. Watu wengi tumekuwa na mawazo kuwa mama wa kambo huwa anakuwa na malezi ya mateso.hata anapompiga mtoto huwa anatesa,ni kama vile mama mzazi wa mtoto huyo asigempiga mwanae hata siku moja.
Ni kweli nakubaliana kuwa zipo adhabu ambazo huwa zinavuka mipaka..lakini naomba tujadili kwa mitazamo yote ya malezi kutoka kwa mama wa kambo kama yamekuletea faida ya kuishi maisha ya kijitegemea leo ukiwa MTU mzima na unaweza kusema kuwa pamoja na kwamba niliona nateseka lakini leo Yale maisha kumbe yalikuwa ni mazoezi ya kuja kukaa vizuri ukwabwani na kukabiliana na chagamoto bila kulia sana. Au Yale maisha aliyokulea, leo unaweza sema kuwa aliniharibia maisha yangu na nisigekuwa hivi nilivyo..
 
Wanafundisha upambanaji katika maisha kwa watoto pasipo kujua, wao wakidhani wanamesha ama kutumikisha.
 
Wanatesa wakidhani wanakomoa kumbe wanafundisha ila hapa inategemea na tabia asili ya mtoto wengine hubaki na visasi na wanajikuta wanarudia makosa yaleyale, wengine akaa anasahau anasamehe maisha yanaendelea.
 
Usisemee mama wa kambo tu hata baadhi ya walezi wananyanyasa sana hapo tegemea mtoto kuja kuwa na kisasi na wewe au watoto wako huko mbeleni mimi nimelelewa na walezi tu wa upande wa baba cha moto nilikiona na kuna baadhi ya mambo yaliniathiri mpaka leo hii ila nashukuru pamoja na mateso yote ilikuwa ni sawa na kumpiga chura teke
 
nachojua siku hizi mambo yamebadilika watoto wa kambo ndo wanatesa.hata ufanye nini haridhiki ,utasimangwa ,utasemwa ukimpiga mtoto ukoo mzima utajua as if wao hawapigi watoto wao kama mleta mada alivosema .yaani ukiwa mama wa kambo halafu mume awe legelege utakoma
 
Unaposema watoto wa kambo wanatesa mbona wa kwako hawakutesi mimi kuna sehemu nimekuwa nikiishi kuna familia ukifika unaweza sema wale watoto ni wa mama mmoja anawalea kwa usawa bila ubaguzi watoto wenyewe wanampenda mama yao wa kambo usipime
 
  • Thanks
Reactions: lup
Niliwahi kuwa na boyfriend, alilelewa na mama wa kambo, anajua kupika kila kitu, mpaka kukanda chapatti, ananiambia wakati huo anasoma, akitoka shule mama anamwambia hukuajiri mfanya kazi hapa, ingia jikoni na akimaliza kupika anasafisha jiko. It was tough love lakini yule mama amemsaidia sana, alivyokuwa university kila jioni alijipikia na aliserve pesa.
 
  • Thanks
Reactions: lup
Kwa hiyo kwa asilimia kubwa mama wa kambo wanatusaidia bila sisj kujua???
 
Moja ya athari kubwa ya kumfokea mtoto na kumkaripia kwa kila afanyalo ni mtoto hata atakapokua atakua kama hajiamini vile!

Yaani kila afanyalo au atakalotaka kulifanya atahisi ni kama anakosea tu!
Kifupi anakua hana "self confidence"

Ukichunguza watu wengi wasio na "self confidence" (japo sio wote) ni watu waliopitia maisha ya mateso kama hayo.
 
Kuna wengine upande wa msosipia hawatendewi haki,mwingine anakuenyesha na kazi nyingi mwisho wa siku chakula pia anakunyima hayapia ni mafundisho au?
 
Kama ilivyo ngumu kwa mwanaume kulea mtoto wa mwanaume mwenzie ndivyo ilivyo ngumu kwa mwanamke pia

Hivyo, mwanaume ndiye anapaswa kusimama kidete ili kuhakikisha kila jambo liko sawa maana Mara nyingine matatizo husababishwa na watoto wenyewe baada ya kujazwa kiburi na ndugu, majirani na makundi mengineyo...

Suala LA mateso kujenga ama kubomoa hutegemeana na asili ya mateso ama akili ya mtoto katika kuhimili mateso hayo
 
  • Thanks
Reactions: lup
Kuna wengine upande wa msosipia hawatendewi haki,mwingine anakuenyesha na kazi nyingi mwisho wa siku chakula pia anakunyima hayapia ni mafundisho au?
Ni mateso..lakini hayo hayawezi kukusaidiq kuishi vizuri ukibwani?
 
nachojua siku hizi mambo yamebadilika watoto wa kambo ndo wanatesa.hata ufanye nini haridhiki ,utasimangwa ,utasemwa ukimpiga mtoto ukoo mzima utajua as if wao hawapigi watoto wao kama mleta mada alivosema .yaani ukiwa mama wa kambo halafu mume awe legelege utakoma
Ni kweli
 
  • Thanks
Reactions: lup
ukiwa unapenda sana wa kwako utakuwa unachukia na kuwaonea wivu wa mwenzako sana..hii ipo naturally
ni kana dini, rangi, kabila, taifa n.k
ukiwa unapenda sana dini yako, kabila lako n.k utakuwa una chuki na mengine
hiyo ni case kwa wamama pia, wamama wanapenda sana watoto wao, yaani very strong emotional attachment,
so inatokea wanakuwa wanawachukia watoto ambao sio wao wakiishi nao
 
  • Thanks
Reactions: lup
Back
Top Bottom