Salute kwa mama yangu wa kambo

Salute kwa mama yangu wa kambo

moi wa kitaa

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2015
Posts
1,016
Reaction score
1,016
Nilipata bahati ya kulelewa na mama wa kambo kwa kipindi kifupi iv

Yule mama alikuwa mama bora tofauti na nilivyosikia kwa watu kuwa mama wa kambo si mama!! Kwangu mimi alikuwa mama! kwa maana alinifunza mambo mengi mazuri ambayo kwa kipindi kile nilihisi ananionea ananitesa

Lakin sasa nimekuwa naona kabisa yale hayakuwa mateso bali yalikuwa ni mafunzo katika dunia!!

Popote ulipo we mama leo nimegundua we Jembe kabsa
 
Mama wa kambo wanatujenga sana,nililelewa na mama wa kambo kwa upendo mkubwa,alinifundisha kazi zote kwa upendo,kupika,kufua kuosha vyombo na alikua ananambia kwa nini ananifundisha zile kazi,mgeni akifika pale nyumbani alikua anasema huyu ni mwanangu wa 2,kumbe ni mama wa kambo....huyu mama nampenda na kumheshimu kuliko hata mama yangu mzazi,amenifanya kua mwanaume nayejitambua,kuheshimu wengine na pia kufanya kazi kwa bidii...Mungu ampe maisha marefu bi Sabina.
 
Hongera sana, mshike sana, sisi wengine tumelelewa na mama wa kambo mwenye sifa ya kuitwa mama wa kambo
Hawa ni wale mama wa kambo ambao walikimbia umande! Hawana uelewa wa kutosha wa masuala mbalimbali yahusuyo malezi! Wametokea kwenye familia zilizojawa na ubinafsi, uchoyo, chuki, kisirani, nk.

Ila ukimpata mama wa kambo sahihi, basi hata mama yako mzazi wakati mwingine anaweza asitie mguu.
 
Sisi kwetu mama yetu mzazi alivyokuwa anatulea ni zaidi ya mama wa kambo kwa kifupi ni kama kambi ya mateso kumbe bana usilolijua ni usiku wa giza maisha yale yametujenga haswaa Dingi alifariki tangu 89.
 
Mama wakambo sio wote wanarohombaya hapana.mimi nimezaliwa kwenye familia kubwa Yani tupo wengi watoto wa Baba mmoja.baba yangu alikuwa na wake 4 ambao miongoni mwao mmoja hakubahatika kupata mtoto.na huyo Kati ya wote ndo alikuwa mke mkubwa wa Baba kuzidi wote na pia hata ki umri.huyo bi mkubwa kazi yake kubwa yeye ndo alikuwa akishinda nyumbani wamama wengine wakienda shambani.ivo yeye ndo anabakia na Sisi watoto Kula kuoga sisi ni kazi yake .na ikifikia umri wa kuachishwa ziwa yeye anachukua jukumu Hilo zaidi ya miaka 3 anakuhudumia Hadi kulala ni ndani mwake.mtoto ukikosea anakuchapa lakini anarudi kulia mwenyewe.mama marezi yalikuwa yazidi ya mama mrezi .Hadi tukambatiza jina la( yaya).mungu aiweke roho ya marehemu mahari salama.
 
Alivyofariki hakuacha mtoto
 
Mama wa kambo wanatujenga sana,nililelewa na mama wa kambo kwa upendo mkubwa,alinifundisha kazi zote kwa upendo,kupika,kufua kuosha vyombo na alikua ananambia kwa nini ananifundisha zile kazi,mgeni akifika pale nyumbani alikua anasema huyu ni mwanangu wa 2,kumbe ni mama wa kambo....huyu mama nampenda na kumheshimu kuliko hata mama yangu mzazi,amenifanya kua mwanaume nayejitambua,kuheshimu wengine na pia kufanya kazi kwa bidii...Mungu ampe maisha marefu bi Sabina.
Kabsa mzee wangu
 
Sisi kwetu mama yetu mzazi alivyokuwa anatulea ni zaidi ya mama wa kambo kwa kifupi ni kama kambi ya mateso kumbe bana usilolijua ni usiku wa giza maisha yale yametujenga haswaa Dingi alifariki tangu 89.
Pole bob
 
Back
Top Bottom