Hivi Makonda ndio "katoswa" au kuna mchongo anatengenezewa?

Hivi Makonda ndio "katoswa" au kuna mchongo anatengenezewa?

Andie

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2011
Posts
712
Reaction score
1,643
Moja kwa moja kwenye mada, wakuu najua kuna wengi tuliwaza kua kuenguliwa kwa Bashite na kuondowea kua RC ilikua ni njia ya kumuandaa kumuweka mahala pa juu zaidi.

Kuna mpaka waliotabiri kua huenda akawa waziri mkuu baada ya uchaguzi, wengine waliwaza uwaziri, hata Paschal Mayalla alitabiri ati Bashite ndie raisi ajae baada ya Jiwe na uzi wake upo humu, wengine uspika kwakweli wengi tulitarajia kijana huyu "kipenzi cha mkuu" kutua katika cheo cha maana.

Ikumbukwe kijana huyu alikua kipenzi haswa cha bwana yule na hata yeyote aliejaribu kumgusa alikiona chamoto vipi niwakumbushe kilichompata Nape Nauye au Kabobe nk.

Makonda alikuwa mpaka anatembea na convoy ulinzi wa Rais atakavyo yeye mwenyewe binafsi, mnakumbuka alivamia mawingu fm akiwa na vikosi maalumu anaviamrisha apeavyo. Nani amesahau kijana alivyokua mpaka anawatishia mawaziri "kuwasemea" kwa mkuu na wakawa wanafyata mikia yao vizuri hiiiiii bagosha !!

Ilikua ukimgusa Makonda umemgusa mkuu, Makonda alikuwa na uwezo wa kumfanya mtu yeyote chochote atakacho. Kuna kibonzo niliona kimechorwa Bashite kabebwa mgongoni na bwana yule huku kashika SMG AK 47.

Kuna picha ya Ikulu ilipigwa jamaa akiwa kakaa siti ya jirani na mkuu siti iliyotakiwa kukaliwa na makamu wa raisi ila yeye ndo alikaa huku makamu wa raisi ikikaa mbali huko, wataalamu wa itifaki walikosoa sana ila yote kwa yote tunakumbuka "uswahiba" wa Bashite na mkuu.

Swali langu kijana wa kithembe, thatha imekuaje tena au ndo tutheme katibuana na bwana yule ?! Au ndo bado anasukiwa channel ?! Au ndo vipi wataalamu wa kubashiri mtheme jambo tafadhali.
 
Imeisha iyo. Teuzi tushamaliza mkuu.saizi Formal RC anajifariji na nyimbo ya mbosso sijui inaitwaje? Amecheza rafu nyingi zinazoonekana, saizi tunasoma namba pamoja.
 
Huo ulinzi wa Rais unauzungunzia upi jomba au umeandika kunogesha story yako
 
Wametibua nini, au kumpiga ban kuingia U.S.A ila hata kama hyo inazuiaje kuendelea kubwa kwa mbeleko ya bwana yule.
Kibwengo 👿 bado anapenda kujikosha kwa mabeberu.

Pili, ukiingia mgogoro na US automatically hata Ulaya hawakuamini. Sidhani kama Bashite anaweza kwenda Ulaya
 
Hata kama bado ila akiteuliwa kwa sasa hawezi kua waziri afu pia kipenzi cha Sizonje iweje ateuliwe utuezi wa dirisha dogo
Anaweza kumteua au asimteue anaweza fanya hivyo ili isionekane anapendelea, kumbuka kuna kumtumbua naibu waziri huko mbele akapewa, na teuz za RC bado zipo, koo huyo f4 failure bado tunae
 
Back
Top Bottom