Hivi mafia iko zanzibar au tanzania bara?

Kuna kitu kilinijia katika akili, na nikaanza kutafakari suala hili. Nchi ya Tanzania ina Tanzania Zanzibar na Tanzania Bara. Tanganyika haipo tena (Miaka 50 ya Tanzania Bara, Stuka). Sasa Mafia katika sherehe ile iliondolewa maana haipo bara. Labada sielewi maana ya bara. Lakini hii inanitia wasi kuhusu hili jina la Tanzania bara kuchukua jina ka Tanganyika. Kama mafia iko visiwani basi ipate kiti baraza la wawakilishi kule Tanzania Visiwani.

Neno Tanzania bara limeiondoa Mafia?
Mafia iko CONGO mkuu!
 
Mafia ni moja ya visiwa vya Tanzania Bara, kuna visiwa vingi tu Tanzania Bara kama Ukara, Kamanga, Nansio, Katunguru, Uzinza, Kigamboni, Karumo, Kisiwa cha Juma, Nyamurutunguru, Izinga, Gana, Burubi. Muriti, Igalla, Namilembe, Kagunguli.

Kigamboni ni Kisiwa?

dah, kumbe kuna watu humu hawajawahi kupita barabara ya Kongowe!
 
Ritz hivi visiwa vyote watu wanaishi huku? mtu unaweza kununua eneo au ni mali ya serikali i mean hifadhi?

Kuna watu wanaishi tena kuna matajiri wakubwa wa samaki visiwa vingine vina watawala wake kabisa...ngoja nikuongezee na vingine. Bukongo, Bukiko, Kakerege, Mukitundu, Namangondo, Nkilizya...najua Bob Mkandara akisoma hii itamkubusha mbali maeneo yake haya.
 
Last edited by a moderator:
Kuna kingine kinaitwa Bongoyo, hivi ni visiwa kwa ajili ya Picnic na usafiri wa kwenda uko unapatikana pale pale Slipway Masaki na Yatch club for Members only.

Shingapi mkuu na mie nikang'ae masharubu. Je, wandengereko wanaruhusiwa huko?
 
Waulize Tanganyika Law Society ni kwa nini hawajiiti Tanzania Mainland Law Society. hawa ni Wanasheria wanajuwa wanachokifanya.
Mkuu jina la kampuni au shirika kama TLS hiyo ni symbol tu huwezi kufananisha na jina la nchi. TLS wangeweza kujiita hata Kenya Law Society ndani ya Tanzania na wakasajiliwa Tanzania. Lakini Tanzania Bara (Tanganyika) kama nchi isn't just a name it is a functional name huwezi kuligeuza kirahisi rahisi.
 
Kuna watu wanaishi tena kuna matajiri wakubwa wa samaki visiwa vingine vina watawala wake kabisa...ngoja nikuongezee na vingine. Bukongo, Bukiko, Kakerege, Mukitundu, Namangondo, Nkilizya...najua Bob Mkandara akisoma hii itamkubusha mbali maeneo yake haya.

duh ..e bwanae Ritz are you serious? ..ina maana hivi visiwa hatuwezi kuvifanya vikawa kama tourist destinations? kwa sababu sijawahu kuvisikia hata siku moja au mimi ndio mzembe sijui ..aise. hii kali .
 
wewe inabidi urudi darasa la kwanza kabisa au awali though najua unatania
Nasikia hata kule CONGO kumbe ilishahama mkuu,sasa hivi MAFIA iko ZIMBABWE...
Kwi kwi kwi kwi.
Kwani hujasikia ile shifting sand ya pale Arusha?(mlima unao hama?)na mafia nayo inahama hama.
 
Kuna kitu kilinijia katika akili, na nikaanza kutafakari suala hili. Nchi ya Tanzania ina Tanzania Zanzibar na Tanzania Bara. Tanganyika haipo tena (Miaka 50 ya Tanzania Bara, Stuka). Sasa Mafia katika sherehe ile iliondolewa maana haipo bara. Labada sielewi maana ya bara. Lakini hii inanitia wasi kuhusu hili jina la Tanzania bara kuchukua jina ka Tanganyika. Kama mafia iko visiwani basi ipate kiti baraza la wawakilishi kule Tanzania Visiwani.

Neno Tanzania bara limeiondoa Mafia?

Mafia iko Tanganyika na si Tanzania bara. Tanzania ni zao la muungano.
 
Mafia iko ndani ya mkoa wa pwani Tanzania bara na ni moja kati ya wilaya sita za mkoa huu nyinginezo ni rufiji,mkuranga,kisarawe,Bagamoyo na kibaha .
 
duh ..e bwanae Ritz are you serious? ..ina maana hivi visiwa hatuwezi kuvifanya vikawa kama tourist destinations? kwa sababu sijawahu kuvisikia hata siku moja au mimi ndio mzembe sijui ..aise. hii kali .

Yote yanawezekana tunaweza kufanya Campsites-Tourism kwenye hivyo visiwa sema tatizo viongozi wetu sio wabunifu mawaziri mwenyewe kina Maige wanashinda Leaders Club wanakunywa bia.
 
Jamani wanajamvi tupunguze majibu ya kihuni. Mtu anauliza swali lake la msingi maana sote tunajua Tanzania visiwani(Zanzibar) inatengenezwa na visiwa viwili Pemba na Unguja.Tunapaswa kumwelimisha kuwa Tanzania ni muungano wa nchi mbili Tanganyika na Zanzibar. Sasa unavyosema Mafia ni Tanzania visiwani na imetengwa nashindwa kukuelewa ua unisaidie Mafia imehamishwa lini kutoka Mkoa wa Pwani? au unamaanisha imetengwa katika swala zima la maendeleo? kama ndo unachomaanisha pole we Kalakabaho huo ni ugonjwa wakila pahali labda uihamishie Mafia Kaskazini mwa Tanzania bara ndo itakumbukwa na serekali ya magamba.Kama sio ulichomaanisha basi huwezi kuzungumzia Mafia peke yake wakati imemezwa na mkoa wa Pwani labda useme na mkoa pia umetendwa.
 
Mafia ni moja ya visiwa vya Tanzania Bara, kuna visiwa vingi tu Tanzania Bara kama Ukara, Kamanga, Nansio, Katunguru, Uzinza, Kigamboni, Karumo, Kisiwa cha Juma, Nyamurutunguru, Izinga, Gana, Burubi. Muriti, Igalla, Namilembe, Kagunguli.
Hivi wewe unajua maana ya kisiwa, toka lini Kigamboni kikawa kisiwa au kwa maana yako seheme inakuwa kisiwa unapovuka maji kwa boti au mtumbwi?, basi kama hivyo ukivuka mto upande wa pili utaita kisiwa. Kamanga siyo kisiwa, Karumo siyo kisiwa, vipi Busisi-Kigongo ferry utaviita visiwa kwa vile huvushwa kwa ferry? Kule Ifakara kuna ferry ya Kilombero sijui kama kuna kisiwa kule.

Kama Kamanga ni kisiwa basi Sengerema nayo lazima itakuwa kisiwa kwa vile Kamanga inaungana na Sengerema kwa nchi kavu. AU kama Kigamboni ni kisiwa kwa vile inaungana na Mbagala kwa nchi kavu Mbagala nayo ni kisiwa teh teh. Shule ndogo sana.
 
Ng'wanangwa Hong Kong ni kisiwa lakini kuna treni inakwenda China.

Treni imejengwa na inavuka maji lkn barabara ya kongowe still ni sehemu ya mainland so as Kigamboni itself. Sikuzote nimeona ukibishana kijiiiinga hapa JF na leo umethibitisha ukomo wa akili yako kwa kutotambua kisiwa ni nini. Mwanzo nilijua unatania lkn sasa inasikitisha kuona hujui kisiwa katika umri huu.

Ndugu yangu Ritz ambaye CCM imekuharibu, kisiwa ni sehemu ili totally isolated from the mainland. Ghuba na Peninsula sio visiwa.
 
Kuna kitu kilinijia katika akili, na nikaanza kutafakari suala hili. Nchi ya Tanzania ina Tanzania Zanzibar na Tanzania Bara. Tanganyika haipo tena (Miaka 50 ya Tanzania Bara, Stuka). Sasa Mafia katika sherehe ile iliondolewa maana haipo bara. Labada sielewi maana ya bara. Lakini hii inanitia wasi kuhusu hili jina la Tanzania bara kuchukua jina ka Tanganyika. Kama mafia iko visiwani basi ipate kiti baraza la wawakilishi kule Tanzania Visiwani.

Neno Tanzania bara limeiondoa Mafia?

kamata lindi, mtwara, dar, pwani na tanga huko kote siyo tanzania bara. Huko niliko taja ni Pwani. Mimi sidanganyiki; Tanganyika yangu ndiyo mpango mzima.
 
Back
Top Bottom