Hivi mafia iko zanzibar au tanzania bara?

Hivi mafia iko zanzibar au tanzania bara?

Mafia ni moja ya visiwa vya Tanzania Bara, kuna visiwa vingi tu Tanzania Bara kama Ukara, Kamanga, Nansio, Katunguru, Uzinza, Kigamboni, Karumo, Kisiwa cha Juma, Nyamurutunguru, Izinga, Gana, Burubi. Muriti, Igalla, Namilembe, Kagunguli.

we ritz acha uongo, kigamboni sio kisiwa.
 
Last edited by a moderator:
Nimekubali wewe ni Great Thinker
Kuna kitu kilinijia katika akili, na nikaanza kutafakari suala hili. Nchi ya Tanzania ina Tanzania Zanzibar na Tanzania Bara. Tanganyika haipo tena (Miaka 50 ya Tanzania Bara, Stuka). Sasa Mafia katika sherehe ile iliondolewa maana haipo bara. Labada sielewi maana ya bara. Lakini hii inanitia wasi kuhusu hili jina la Tanzania bara kuchukua jina ka Tanganyika. Kama mafia iko visiwani basi ipate kiti baraza la wawakilishi kule Tanzania Visiwani.

Neno Tanzania bara limeiondoa Mafia?
 
Hilo siyo ajabu hata Treni ya kutoka London kwenda Paris inapita chini ya Bahari ( English Channel ).
Kwa maana yako hiyo tuseme duniani hakuna kisiwa kwa vile visiwa vinaweza kuunganishwa kwa underground train(chini ya bahari)?

Kwa wana Jiografia, inasemekana mabara yaliyopo (Continents) yako 7 sijui 8 yalikuwa yameungana. Dunia ilikuwa na continent moja Giant Continent lilikuwa linaitwa PANGEA kabla ya kugawanyika.
images
images
 
Mafia ni moja ya visiwa vya Tanzania Bara, kuna visiwa vingi tu Tanzania Bara kama Ukara, Kamanga, Nansio, Katunguru, Uzinza, Kigamboni, Karumo, Kisiwa cha Juma, Nyamurutunguru, Izinga, Gana, Burubi. Muriti, Igalla, Namilembe, Kagunguli.
Musila, Goziba na Bumbire vyote ni visiwa pia.
 
Mafia ni moja ya visiwa vya Tanzania Bara, kuna visiwa vingi tu Tanzania Bara kama Ukara, Kamanga, Nansio, Katunguru, Uzinza, Kigamboni, Karumo, Kisiwa cha Juma, Nyamurutunguru, Izinga, Gana, Burubi. Muriti, Igalla, Namilembe, Kagunguli.
Kigamboni ni peninsula (sehemu ya nchi kavu iliyoingia baharini)
 
Sioni tatizo kwa Tanzania Bara kuendelea kuitwa hivyo hata kama inavisiwa baharini. Kwani hii Bahari ya Hindi inamaana sisi hatuna kabisa bahari ni mali ya India? au USA inamaan Brazili, canada ni sehemu ya USA? Au kama tuna Mashariki ya kati inamaana tuna mashariki ya pembeni? ni majina tu yenye lengo la kuitambulisha maeneo.
 
Hivi wewe unajua maana ya kisiwa, toka lini Kigamboni kikawa kisiwa au kwa maana yako seheme inakuwa kisiwa unapovuka maji kwa boti au mtumbwi?, basi kama hivyo ukivuka mto upande wa pili utaita kisiwa. Kamanga siyo kisiwa, Karumo siyo kisiwa, vipi Busisi-Kigongo ferry utaviita visiwa kwa vile huvushwa kwa ferry? Kule Ifakara kuna ferry ya Kilombero sijui kama kuna kisiwa kule.

Kama Kamanga ni kisiwa basi Sengerema nayo lazima itakuwa kisiwa kwa vile Kamanga inaungana na Sengerema kwa nchi kavu. AU kama Kigamboni ni kisiwa kwa vile inaungana na Mbagala kwa nchi kavu Mbagala nayo ni kisiwa teh teh. Shule ndogo sana.

Mkuu mwenye shule kubwa naomba unifahamishe Uingereza ni kisiwa au sio kisiwa?

Halafu naomba unafahamishe kwa faida ya wana JF visiwa viwili vya Sengerema Mchangani na Zilaguza na Kome jinsi vilivyo.
 
Kisiwa cha Mafia ni sehemu ya Tanganyika, na ni Wilaya mojawapo ya Mkoa wa Pwani.
Heshima yako mkuu Edwin Mtei, naona watu wanahoji zaidi maana ya neno 'Bara' badala ya eneo la utawala wa nchi, kama tukikubaliana Tanganyika=Tanzania Bara then visiwa vya Mafia viko Tanzania Bara, lakini tukijadili kwa kuzingatia maana ya maneno 'Bara' na 'Visiwani' kunaweza kuwa na utata ingawa si mkubwa sana.
 
Last edited by a moderator:
Mafia ni moja ya visiwa vya Tanzania Bara, kuna visiwa vingi tu Tanzania Bara kama Ukara, Kamanga, Nansio, Katunguru, Uzinza, Kigamboni, Karumo, Kisiwa cha Juma, Nyamurutunguru, Izinga, Gana, Burubi. Muriti, Igalla, Namilembe, Kagunguli.

Mkuu ritz sikuwezi yaani unakijua hadi kisiwa cha Juma? Vipi kisiwa cha Mchangani nacho unakijua? Vipi kile cha Bumbire?

Hapa Dar kuna kisiwa cha Mbudya nacho kiende Zanzibar?
 
Last edited by a moderator:
Ng'wanangwa Hong Kong ni kisiwa lakini kuna treni inakwenda China.

Ritz, wewe ni wa ajabu. Kwa hiyo unataka kuhalalisha kuwa Kigamboni ni kisiwa, kufikiwa na barabara ya Kongowe - Kivukoni si hoja?

Wakati ninasoma shule ya msingi miaka hiyo, ilikuwa katka Jiografia, lazima ujue maana ya ghuba, rasi, kisiwa, ziwa, mto na bahari (ndogo na Kuu) kati ya misamiati mingi.

Bandari ya Dar ilipo ni kama namna fulani ya ghuba, ambayo mwisho wake ni Mtoni Kijichi, mashariki ikiwepo Kigamboni na Magharibi ikiwa ardha ya Kurasini.
Nafikiri utakuwa umeelewa.
 
Last edited by a moderator:
Yote yanawezekana tunaweza kufanya Campsites-Tourism kwenye hivyo visiwa sema tatizo viongozi wetu sio wabunifu mawaziri mwenyewe kina Maige wanashinda Leaders Club wanakunywa bia.

definetly sio kwamba hawa mawaziri wanashindwa ..wanaweza tatizo linakuwa ni informations za kutosha kuhusu hizi sehemu hawana ...ila kusema ukweli nimeshtuka
 
Mafia ni moja ya visiwa vya Tanzania Bara, kuna visiwa vingi tu Tanzania Bara kama Ukara, Kamanga, Nansio, Katunguru, Uzinza, Kigamboni, Karumo, Kisiwa cha Juma, Nyamurutunguru, Izinga, Gana, Burubi. Muriti, Igalla, Namilembe, Kagunguli.
ritz,

Hapo kwenye red umetuingiza chaka.

TUMBIRI wa JF
 
Ng'wanangwa Hong Kong ni kisiwa lakini kuna treni inakwenda China.
ritz,
Tafsiri ya neno Kisiwa kwa Kiswahili rahisi: "Ni sehemu ya Nchi kavu iliyozungukwa na maji (Bahari na Ziwa). Sasa Kigamboni imezungukwa na Bahari? Inawezekana hicho kisiwa unachosema kipo Hong Kong treni inakwanda lakini treni kwenda haimaanishi ni kisiwa au siyo kisiwa. Zingatia tafsiri ya neno Kisiwa.

TUMBIRI wa JF
 
Last edited by a moderator:
Ng'wanang'wa, wewe ni wa ajabu. Kwa hiyo unataka kuhalalisha kuwa Kigamboni ni kisiwa, kufikiwa na barabara ya Kongowe - Kivukoni si hoja?

Wakati ninasoma shule ya msingi miaka hiyo, ilikuwa katka Jiografia, lazima ujue maana ya ghuba, rasi, kisiwa, ziwa, mto na bahari (ndogo na Kuu) kati ya misamiati mingi.

Bandari ya Dar ilipo ni kama namna fulani ya ghuba, ambayo mwisho wake ni Mtoni Kijichi, mashariki ikiwepo Kigamboni na Magharibi ikiwa ardha ya Kurasini.
Nafikiri utakuwa umeelewa.
Mnyamahodzo aliyesema Kigamboni ni kisiwa si Ng'wanang'wa ni ritz.
 
Kuna kitu kilinijia katika akili, na nikaanza kutafakari suala hili. Nchi ya Tanzania ina Tanzania Zanzibar na Tanzania Bara. Tanganyika haipo tena (Miaka 50 ya Tanzania Bara, Stuka). Sasa Mafia katika sherehe ile iliondolewa maana haipo bara. Labada sielewi maana ya bara. Lakini hii inanitia wasi kuhusu hili jina la Tanzania bara kuchukua jina ka Tanganyika. Kama mafia iko visiwani basi ipate kiti baraza la wawakilishi kule Tanzania Visiwani.

Neno Tanzania bara limeiondoa Mafia?
hata kigamoni tutaiita znz sasa kwa dizaini hiyo,au misri na saudia ni nchi moja pia
 
Mkuu ritz sikuwezi yaani unakijua hadi kisiwa cha Juma? Vipi kisiwa cha Mchangani nacho unakijua? Vipi kile cha Bumbire?

Hapa Dar kuna kisiwa cha Mbudya nacho kiende Zanzibar?

Mkuu wangu Kimbunga maisha ndugu yangu ndio yalitufikisha huko tulikuwa na Bob Mkandara.
 
Last edited by a moderator:
Kisiwa cha Mafia ni sehemu ya Tanganyika, na ni Wilaya mojawapo ya Mkoa wa Pwani.

Nakubaliana kabisa na Mzee Mtei. Kitu ambacho nashindwa kuelewa hasa maana halisi ya bara inayotumiwa wakati tuna sema Tanzania bara na Tanzania Visiwani. Maana ukisema Tanzania visiwani, yaani Pemba, unguja, Mafia, Ukerewe na Vingine vingi tu. Afadhali kutumia neno Tanzania Zanzibar. Sasa Tanzania bara unakuwa umeondoa Ukerewe, Unguja, Pemba, Mafia NK. Bado naona jina Tanzania Bara ni Utata mtupu. Tutumie tu Tanzania Tanganyika na Tanzania Zanziba, hapo tutavitendea haki hivi visiwa. Tanganyika shall never die.
 
Feedback na TUMBIRI Uingereza iko kwenye kisiwa kikubwa cha Britania ambayo ni kisiwa kikibwa ulaya.

Kuna njia ya Barabara kutoka Holland mpaka Uingereza njia hiyo maarufu sana kipitishia watu kwa magari makubwa kuingia Uingereza.

Sasa kwa nini Uingereza inaitwa kisiwa wakati kuna barabara inayokwenda mpaka Holland nifahamisheni kwa faida ya JF.
 
Ritz Nimesikia kwamba, kumbe tanga, dar, pwani, mtwara na lindi sio Tanzania bara bali ni Tanzania pwani. Yaani hapa nazidi kupoteza maana ya jina la nchi Tanzania Bara. Heri tu turudie Jina la Tanganyika.
 
Back
Top Bottom