Hivi mafia iko zanzibar au tanzania bara?

Kuna kitu kilinijia katika akili, na nikaanza kutafakari suala hili. Nchi ya Tanzania ina Tanzania Zanzibar na Tanzania Bara. Tanganyika haipo tena (Miaka 50 ya Tanzania Bara, Stuka). Sasa Mafia katika sherehe ile iliondolewa maana haipo bara. Labada sielewi maana ya bara. Lakini hii inanitia wasi kuhusu hili jina la Tanzania bara kuchukua jina ka Tanganyika. Kama mafia iko visiwani basi ipate kiti baraza la wawakilishi kule Tanzania Visiwani.

Neno Tanzania bara limeiondoa Mafia?

Bw Sanga, Mafia iko Njombe!
Tena mkoa mpya
 
Mafia ni moja ya visiwa vya Tanzania Bara, kuna visiwa vingi tu Tanzania Bara kama Ukara, Kamanga, Nansio, Katunguru, Uzinza, Kigamboni, Karumo, Kisiwa cha Juma, Nyamurutunguru, Izinga, Gana, Burubi. Muriti, Igalla, Namilembe, Kagunguli.
ritz! Kazi kweli!
 
Duh mkuu ritz hakika utakuwa unawajua wababe wa huko visiwani ambao huwa wanawazamisha watu ziwani na kujichukulia nyavu na makokoro! Sijui kama unamjua mtu mmoja aliyekuwa mbabe sana huko akiitwa Kitana. Bila shaka umewekeza huko manake bila hivyo ni vigumu kuvijua visiwa hivyo. Safi sana.
Mkuu Kimbunga huyo jamaa saizi ni tajiri mkubwa sana Mwanza (Mzungu wa Samaki) naona saizi kaacha mambo yake karudi kwa mungu, mkuu wangu na wewe sio mchezo kila nilipo gusa na wewe umegusa:yo:
 
Last edited by a moderator:
Bw Sanga, Mafia iko Njombe!
Tena mkoa mpya

Kwani njombe imo Tanzania visiwani? Tatizo langu ni pale wanaposema mafia iko Tanzania Bara badala ya Tanganyika. Najua kuna wanaofikiri sijui location ya mafia. Iko ndania ya Bahari, sasa napata tabu unaposema iko mainland (Bara)
 
Mkuu Kimbunga huyo jamaa saizi ni tajiri mkubwa sana Mwanza (Mzungu wa Samaki) naona saizi kaacha mambo yake karudi kwa mungu, mkuu wangu na wewe sio mchezo kila nilipo gusa na wewe umegusa:yo:
Lakini naona kama umechapiachapia visiwa vyenyewe - Nansio na Muriti ndio visiwa gani hivyo?. Haya bana basi Bundya na Kilwa kisiwani nazo Visiwani..
 
Mkuu Kimbunga huyo jamaa saizi ni tajiri mkubwa sana Mwanza (Mzungu wa Samaki) naona saizi kaacha mambo yake karudi kwa mungu, mkuu wangu na wewe sio mchezo kila nilipo gusa na wewe umegusa:yo:
ritz namjua jamaa ni tajiri pale MZ lakini alianzia huko visiwani. Mkuu nilipiga kambi huko kisiwa cha Lyakanyasi na mara nyingine kisiwa cha Juma! Mkuu hata mimi naona nilipokanyaga nawe umetia guu! Kuanzia mitaa ya K'oo hadi Holiday out.Tupo pamoja mkuu ila sikutegemea kabisa kwamba ungekuwa unavijua visiwani vya kule ziwani.
 
Last edited by a moderator:
Ungeenda kwa google tu ungepata jibu kua mafia iko tanzania bara - tanganyika, ni moja kati ya visiwa vingi tu kama ukara, ukerewe etc
 
definetly sio kwamba hawa mawaziri wanashindwa ..wanaweza tatizo linakuwa ni informations za kutosha kuhusu hizi sehemu hawana ...ila kusema ukweli nimeshtuka
mkuu hakuna information inayokuja bila kutafuta!
Wasisubili mezani watembee kutafuta!
 
ritz namjua jamaa ni tajiri pale MZ lakini alianzia huko visiwani. Mkuu nilipiga kambi huko kisiwa cha Lyakanyasi na mara nyingine kisiwa cha Juma! Mkuu hata mimi naona nilipokanyaga nawe umetia guu! Kuanzia mitaa ya K'oo hadi Holiday out.Tupo pamoja mkuu ila sikutegemea kabisa kwamba ungekuwa unavijua visiwani vya kule ziwani.

Mkuu Kimbunga miaka ya nyuma kidogo tumepiga kazi kule Mwanza, nadhani utakuwa hunamjua Mgiriki mmoja alikuwa na kiwanda cha Samaki kinaitwa Nile Pech.

Naona saizi kabaki yule Muhindi Murtaza wa Vicfish. Ambae wale samaki wa Magufuli walikuwa wanahifadhiwa kwenye kiwanda chake cha Bahari beach...mkuu mambo ni mengi sana.
 
Last edited by a moderator:
Embu nijuze kuhusu gharama ya kupelekwa huko na hiyo boat kwa mtu mmoja!! Kuna nn huko? Kuangalia tu jinsi sehemu ya Ardhi ilivyozungukwa na maji au?

Mkuu kule hakuna boti usafari ni mitumbwi ya engine au mtumbwi wa kasia kama una roho ndogo huwezi kuishi kule halafu kuna gharama sana miaka ile sahani ya wali elfu 2000.
 
Mkuu Kimbunga miaka ya nyuma kidogo tumepiga kazi kule Mwanza, nadhani utakuwa hunamjua Mgiriki mmoja alikuwa na kiwanda cha Samaki kinaitwa Nile Pech.

Naona saizi kabaki yule Muhindi Murtaza wa Vicfish. Ambae wale samaki wa Magufuli walikuwa wanahifadhiwa kwenye kiwanda chake cha Bahari beach...mkuu mambo ni mengi sana.

Okay Mkuu ritz nimekupata sasa. Nawajua hao watu.Ndio waanzilishi wa kuwalisha wananchi wa kanda ya ziwa vile vichwa vya samaki na mifupa maarufu kama Mapanki hadi ikaja ile picha ya Darwin's Nightmare!!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu kule hakuna boti usafari ni mitumbwi ya engine au mtumbwi wa kasia kama una roho ndogo huwezi kuishi kule halafu kuna gharama sana miaka ile sahani ya wali elfu 2000.

Mkuu ritz mbona unasahau usafiri wa ngama?
 
Last edited by a moderator:
Okay Mkuu ritz nimekupata sasa. Nawajua hao watu.Ndio waanzilishi wa kuwalisha wananchi wa kanda ya ziwa vile vichwa vya samaki na mifupa maarufu kama Mapanki hadi ikaja ile picha ya Darwin's Nightmare!!

ha haa haaa! Mkuu Kimbunga umenichekesha sana nakumbuka zamani yale mapanki yalikuwa yanatupwa kule maeneo ya Igoma kwenye dampo hali ilivyokuwa ngumu yakageuka mboga.
 
Last edited by a moderator:
ha haa haaa! Mkuu Kimbunga umenichekesha sana nakumbuka zamani yale mapanki yalikuwa yanatupwa kule maeneo ya Igoma kwenye dampo hali ilivyokuwa ngumu yakageuka mboga.

Pale karibu na tulipowahifadhi ndugu zetu waliopotea kwenye ajali ya MV Bukoba.
 
Last edited by a moderator:
Mafia ni moja ya visiwa vya Tanzania Bara, kuna visiwa vingi tu Tanzania Bara kama Ukara, Kamanga, Nansio, Katunguru, Uzinza, Kigamboni, Karumo, Kisiwa cha Juma, Nyamurutunguru, Izinga, Gana, Burubi. Muriti, Igalla, Namilembe, Kagunguli.

Mi nafikiri JF inabidi iweke vitufe viwili kimoja ''like na dislike''. Huyu jamaa kaamua kukusanya majina yooote na kuyafanya visiwa.
 
Mafia ni moja ya visiwa vya Tanzania Bara, kuna visiwa vingi tu Tanzania Bara kama Ukara, Kamanga, Nansio, Katunguru, Uzinza, Kigamboni, Karumo, Kisiwa cha Juma, Nyamurutunguru, Izinga, Gana, Burubi. Muriti, Igalla, Namilembe, Kagunguli.
Bilashaka hujui unachoandika, maana naona hujui hata maana ya kisiwa
 
Back
Top Bottom