Hivi Laana ni nini?

Hivi Laana ni nini?

Asante, hii kuwashirikisha wakubwa na hawa ndio hulaani ukiwakosea, wakubwa hutoa laana?! How?!
mkuu inapotokea umemkosea mnooo baba yako ama mama yako kisha mkafikia kwenye hatua mbaya kabisaa yakutengana ...kwa mila na desturi zetu zaki Africa kama unahitaji suluhu nae yakupasa kuwatafuta watu wazima ambao ni watu wazima wenzie ..kama Shangazi mjomba au wazee wanao heshimika ktk kitongoji .kisha unawaeleza dhumuni lako ..kisha wao wtaandaa kikao kwaajili yakwenda kukuombea msamaha nawewe pia ukiwepo ktk hcho kikao ..hizo nitaratibu ambazo tumezaliwa na kuzikuta ..nayakupasa utambue kuwa kila Jamii ina desturi zake
 
Hivi hizi laana ni kwetu Waafrika tu au hata race zingine hupata haya malaana?!
 
WAKUU neno laana uslitafsiri kwa elim ulio nayo hutoweza hata kidogo, Laana nineno kubwa niongoni mwa maneno makubwa sana!" LAANA INATOKEA KWA MTU YEYOTE ALIE FANYA MABAYA MAKUU, HAIWEZEKANI UKATENDA MEMA KISHA UKA LAANIWA, MFANO umedhulumu mali ya kanisa au msikiti nilazima waumini wataumia sana nyoyo zao na nafsi pia, katka hilo pia MUNGU HAPENDI KITENDO ULICHO KIFANYA, HAPA MAJIBU YAKE WAUMINI WAMEMUACHIA MUNGU MAANA YEYE NDIE MUWEZA WA YOTE, JAPO KUTAKUWEPO MAOMBI KWA WAUMINI HAO, HAKIKA MUNGU ATAJIBU, MAANA MUNGU MWENYEWE AMEKATAZA UHALIFU KAMA WIZI NK. NI HALI KADHALIKA UKIMFANYIA UBAYA MWENNZO ALIE KUTENDEA WEMA SIKU ZOTE, MFANO MAMA KAKUBEBA TUMBONI MIEZ9 KAKULEA MIAka yote, Matokeo yake unamdharau na kumpuuza, humueshimu nk, Akichukia lazima udhurike maana hata mungu Anachukia matendo hayo, HESHIMA,HEKIMA NA BUSARA NI VITU VIKUBWA SANA,, UKIVIKOSA VYOTE HIVYO LAZIMA UWE NI MTU USIE ENDANA NA JAMII MAANA YAKE UMEINGIWA NA NA LAANA AU BALAA, NA MUTU HUYO AKIFA MAISHA YAKE NIMOTONI
 
Laana ni deni ya kisasi cha mtu kwa mtu aliemkosea against pure coincidences ya matatizo yanayompata yule mtu mkosaji..Hakuna scientific correlation kabisa!
 
Dah....usiumize kichwa...laana ni neno rahisi LA kisiasa lenye kumaananisha kutounga mkono tukio fulani....Tanzania yalaani ndoa za mashoga.....Trump alaani majaribio ya makombora ya Korea....wala hata Prof mshana jr hahitajiki pia hata kiingereza hakihitajiki ili uelewe
 
Laana ni kitisho kinachotumika na upande mmoja dhidi ya upande pinzani.
 
Jamani eti laana ni nini?! Ni maombi au ni ni uchawi?! Huwa nasikia fulani kalaaniwa yule, usifanye hivyo utalaaniwa, usifanye hivyo utapata laana, utawala huu umelaanika, nakadharika. Laana ni nini?! Mtu aliyelaanika yukoje?! Nani hutoa au anauwezo wa kulaani?! Je laana ni ulizi/uchawi au maombi/dua mbaya kwa mtu, na je hizi laana pia hutolewa na mungu au ni mashetani au mizimu?! Nami naweza kumlaani mtu au nini vigezo vya kulaani na kulaaniwa?!

Huwa siamini sana kwenye huu ' Upuuzi / Uswahili ' kwani kuna Mtu mmoja nakumbuka aliambiwa na tena akahakikishiwa kuwa ' atalaaniwa ' ili maisha yampige na awe ' hohehahe / masikini ' wa kutupwa lakini cha kushangaza hadi hivi sasa huyo Jamaa ( aliyeambiwa atalaaniwa ) ana Hela / Pesa na zinazidi tu kumtembelea na maendeleo kibao / lukuki huku Yule Yule aliyetamba ' Kumlaani ' umasikini ndiyo umemzidi hadi katika ' Kope ' zake za macho.
 
Laana ni tendo linalompata mtu linalosababisha mtu huyo kupata mikasa mbalimbali na hata akienda kutibiwa kwa waganga wa kienyeji mikasa haitoki ,akiombewa kanisani pia haitoki.

Na hii humtokea mtu aliyedharau mzazi wake baada ya mtu huyo kujua MWEMA na mabaya yeye hawatendei mema wazazi wake.

Lakini pia anakuwa na tabia ya kuwatendea mabaya watu ambao hawana uwezo wa kumlipa kisasi kwa sababu mbali mbali za kiuwezo hivyo manung' uniko,kilio na malalamiko yao hupelekea kumdhuru yule anayewatendea, wakati mwingine kizazi chake kinaweza kupatwa na madhara yaliyotikana na hayo matendo yaliyotendwa na huyo aliyejiona yeye huwezi kupata madhara.

Laana haionekani kwa macho tena ni ugonjwa hatari hauna tiba wala chanjo kwa mtu lakini una kinga tu! Na kinga Yake ni kuacha k kufanya hayo niliyoeleza hapo juu.
 
Mafwi Munda jibu lako ni very simple.
Maana ya Laana ni Mwenyezi Mungu kuondoa au kumweka mbali na rehma (huruma ) zake kwa huyo mtu. Period.
Tunaambiwa Mungu ndiye anatuumba tukiachana na biology ya baba na mama, sasa hizo rehema kwanini aziondoe au aziweke mbali?! Au ndio adhabu zake?!
 
Jamani eti laana ni nini?! Ni maombi au ni ni uchawi?! Huwa nasikia fulani kalaaniwa yule, usifanye hivyo utalaaniwa, usifanye hivyo utapata laana, utawala huu umelaanika, nakadharika. Laana ni nini?! Mtu aliyelaanika yukoje?! Nani hutoa au anauwezo wa kulaani?! Je laana ni ulizi/uchawi au maombi/dua mbaya kwa mtu, na je hizi laana pia hutolewa na mungu au ni mashetani au mizimu?! Nami naweza kumlaani mtu au nini vigezo vya kulaani na kulaaniwa?!
Laana ni mikosi
 
Huwa siamini sana kwenye huu ' Upuuzi / Uswahili ' kwani kuna Mtu mmoja nakumbuka aliambiwa na tena akahakikishiwa kuwa ' atalaaniwa ' ili maisha yampige na awe ' hohehahe / masikini ' wa kutupwa lakini cha kushangaza hadi hivi sasa huyo Jamaa ( aliyeambiwa atalaaniwa ) ana Hela / Pesa na zinazidi tu kumtembelea na maendeleo kibao / lukuki huku Yule Yule aliyetamba ' Kumlaani ' umasikini ndiyo umemzidi hadi katika ' Kope ' zake za macho.
Hivyo hii kitu Laana ni uongo tu. Maana inatumika sana kutisha huku kwetu, eti utalaaniwa wewe yani laana kama mwanga unapenya kila mahali, hadi kwenye daladala eti usiponipisha siti utallanika mimi mkubwa, nahisi wanalitumia hili neno vibaya na labda hakuna hata hizo laana zenyewe.
Yani kila mtu analaani hazina qualifications zozote sio dini wala umri kila mtu analaani mwenziye.
 
Laana ni kutokufanikiwa ktk Yale Mtu anayoyatarajia na zaidi!
Mtu anaweza kuwa kuwa na elimu kubwa, Mtu anaweza kuwa na ukwasi, fedha na Mali nyingi na bado akawa yuko chini ya Kongwa ya laana kubwa !
Ni Kukosa kuwa na Raha ya nafsi!
 
Mi sitii neno hapo maana najua alielaniwa ni shetani ( iblis) na Firaun (Farao).
 
Laana ni tendo linalompata mtu linalosababisha mtu huyo kupata mikasa mbalimbali na hata akienda kutibiwa kwa waganga wa kienyeji mikasa haitoki ,akiombewa kanisani pia haitoki.

Na hii humtokea mtu aliyedharau mzazi wake baada ya mtu huyo kujua MWEMA na mabaya yeye hawatendei mema wazazi wake.

Lakini pia anakuwa na tabia ya kuwatendea mabaya watu ambao hawana uwezo wa kumlipa kisasi kwa sababu mbali mbali za kiuwezo hivyo manung' uniko,kilio na malalamiko yao hupelekea kumdhuru yule anayewatendea, wakati mwingine kizazi chake kinaweza kupatwa na madhara yaliyotikana na hayo matendo yaliyotendwa na huyo aliyejiona yeye huwezi kupata madhara.

Laana haionekani kwa macho tena ni ugonjwa hatari hauna tiba wala chanjo kwa mtu lakini una kinga tu! Na kinga Yake ni kuacha k kufanya hayo niliyoeleza hapo juu.
Najua umeeleza sana lakini sielewi, huu ugonjwa unakuwaje na dalili au mgonjwa huonekana vipi kutofautisha mgonjwa wa typhoid, malaria na huyu wa gonjwa la laana?!
Hivyo siyo mungu anayelaani?! Huwa nasikia umelaaniwa na mungu au utalaaniwa na mungu,
 
Laana ni kutokufanikiwa ktk Yale Mtu anayoyatarajia na zaidi!
Mtu anaweza kuwa kuwa na elimu kubwa, Mtu anaweza kuwa na ukwasi, fedha na Mali nyingi na bado akawa yuko chini ya Kongwa ya laana kubwa !
Ni Kukosa kuwa na Raha ya nafsi!
Hahaha yani kwa ki hebrania mnaita Depression kukosa raha ya nafsi. Lakini hii inadawa kule hospitali huwa wana vidonge vya anti-depressants, Na ukiachilia hiyo, hili la mafanikio ni kiasi gani mtu ukifanikiwa unasema hujalaanika au hakuna limit ya juu ya mafanikio je limit ya chini au minimum success ni kiasi gani ili kusema hujalaanika?!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom