Hivi Laana ni nini?

Haogopwi mtu yoyote yule ila nimeona hata nikianza kufunguka hapa itakusaidia nn wakati huijui hata mistari ya biblia?
Si bora uingie chimbo kwanza ujiweke sawa halafu tusonge...
Huku tunataka msaada kujua Laana ni nini?! Dini bado natafuta, kwanini umetanguliza biblia hata sijachagua dini?! Mungu yupo kila mahali, dini ni sehemu ya kusalia si ndiyo au nakosea?! Kwasasa sijachagua.
 
karma ni vuno la matendo Yako.
Ukitenda Wema utavuna mema,Ukitenda ubaya utavuna ubaya.Mavuno huwa makubwa kuliko mbegu.

Sasa Laana navojua ni vuno baya kutokana na matendo yako mabaya kwa watu ambao hawakustahili ubaya wako hasa wazazi au ndugu wa karibu,rafiki au mpenzi(mwenye mashiko)

sasa hilo vuno baya linaweza kukupiga kama hali,tabia au Gonjwa.

Kujijua kama una laana ni kujitathmini na mabaya au tabia mbaya ulonayo.
laana inapiga kizazi mpaka kizazi.
Waweza kupatwa na changamoto isio kikomo,gonjwa au hasara...jitafakari mapito yako.Tubu anza upya
kwa wale wasio amini mungu watende mema mengi kuliko mabaya kufuta madeni yao yanayoleta laana.
mfano wa laana ni ulevi uliotukuka wa kuleta hasara au umalaya usio mfano ambao utakupa majibu mazuri Tu yq kupendeza siku za Usoni.

mkuu umeenda skuli kulingana na maelezo yako -hongera
 
Kuna mtu kaniambia eti Albadir ni Laana, nani anaweza kuthibitisha hili.
Aliongeza mtu kama Nabii Titto ni mfano wa mtu aliyelaanika, akidai eti matendo yake yanathibitisha hilo, hakutaka kusikia taarifa kwamba ni mgonjwa wa kichaa. Je ugonjwa ndio laana?!
 
Leo nimesikia kutoka Kinondoni eti ccm chama na tawi lao polisi na viongozi wote wa serikali awamu ya tano wamelaaniwa. Nani kawalaani?!
 
Jamani eti laana ni nini?! Ni maombi au ni ni uchawi?! Huwa nasikia fulani kalaaniwa yule, usifanye hivyo utalaaniwa, usifanye hivyo utapata laana, utawala huu umelaanika, nakadharika. Laana ni nini?! Mtu aliyelaanika yukoje?! Nani hutoa au anauwezo wa kulaani?! Je laana ni ulizi/uchawi au maombi/dua mbaya kwa mtu, na je hizi laana pia hutolewa na mungu au ni mashetani au mizimu?! Nami naweza kumlaani mtu au nini vigezo vya kulaani na kulaaniwa?!
IJUE LAANA KWA KINA.

MUNGU atukuzwe ndugu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.
Laana ni nini?

Laana ni ukosefu wa radhi za MUNGU katika jambo fulani.
Radhi ni nini?
Radhi ni msamaha.
Hivyo laana ni ukosefu wa msamaha wa MUNGU katika jambo fulani.
Hiyo ni maana ya kwanza ya laana.

Maana nyingine ya laana ni.
Laana ni apizo alitoalo mtu kwa mtu mwingine ili afikwe na mabaya?


Zipo laana nyingi lakini leo ningependa kuzungumzia laana zifuatazo:-

Ukoo/familia:- laana zinazojiendeleza kwenye ukoo hutokana na matokeo ama matunda ya dhambi. Kwa mfano unakuta katika familia husika kuna wengine wana laana za magonjwa sugu kama kansa, kwenye hiyo hiyo familia wengine hawaolewi, wengine wameolewa lakini ndoa hazidumu, wengine hawapati mimba. Familia nyingine utakuta kuna vifo vya ghafla, wanaanza maisha na kufanikiwa na kuwa na mali na biashara kubwa au kazi lakini mwisho wao wanaishia kufilisika na kufa kwa mateso makali.Unatakiwa kuomba maombi ya rehema na toba na lazima utamke kilichofanyika na matokeo yake. Kwa sababu kila dhambi iliyofanyika ni kutokana na kuwa na miungu mingine. Dhambi inatokea pale mtu anapomwacha Mungu wa kweli na kusikiliza miungu mingine. Sasa unapokosa msaada wa Mungu wa kweli unapata misaada ya miungu inayokusababisha wewe kutenda kinyume na Mungu. “Usiwe na miungu mingine ila Mimi- Kumbukumbu la torati 5:7”

Laana za kulaaniwa na mtu mwingine:- Yawezekana ulikosana na rafiki yako ama mtu mwingine pengine mwalimu wako wa shule akakuchukia na kukulaani. Anaweza kukulaani kuwa na kamwe hutakaa uendelee kwa kila utakalofanya usifanikiwe.

Laana za kujilaani mwenyewe:- Kuna watu hawaridhiki na jinsi walivyo ama niseme viungo vya miili yao, yaani kwa ufupi hawajikubali ama kujiamini. Utakuta mtu analalamika na kusema “aah mimi kwa ufupi huu sidhani kama nitakaa nipate mwanamke mrefu atakaenipenda, ama mwingine atajilaani kwa kusema kamwe hawezi kuwa mtu wa kwanza darasani kwa sababu tu ya mtu fulani nyumbani kwao hajawahi kuwa” Siku zote maneno huumba na kujiumba, kwa maana hiyo yale uyatamkayo mdomoni kwako vivyo hivyo yanafanyika.

Laana ya vitu visivyoisha: Kuna watu wamelaaniwa kwa kila wakigusacho kisiendelee na matokeo yake hujikuta wameanzisha vitu mbali mbali bila hata kimojawapo kukamilika. Mfano mtu anataka kujenga lakini anaishia nusu na kuanza kitu kingine ambacho nacho hakifiki mbali. Nataka kuanzisha biashara ya nguo, atanunua sehemu ya kuuzia nguo lakini hakuna kitakachoendelea. Watu kama hawa ni wale wanaonena kwa midomo lakini hawatekelezi.

Laana ya kufanya tendo la ndoa na dada yako au kaka yako, baba yako au mama yako
Kuna mambo mengine sio rahisi hata kuelezea lakini yapo na yanafanyika mtu amelala na Dada yake, mwingine na kaka yake, laana ya Mungu imeagizwa juu yao “Kumb 27:22 Na alaaniwe alalaye na umbu lake, binti ya babaye au Binti ya *****. Na watu wote waseme Amina”



Haya yote yanatokana na UPOFU wa mawazo. Akili ikifungwa mtu hawezi kufanya maamuzi yoyote. Pia akili ikifungwa mtu haoni ugumu wa dhambi. “2Wakorintho 3:14 ila fikira zao zilitiwa uzito. Kwa maana hata leo hivi wakati lisomwapo Agano la kale, utaji uo huo wakaa, yaani haikufunuliwa kwamba huondolewa katika Kristo”. Soma pia Waefeso 4:18

Wa wengi hujitanganya kwamba hawana laana kwa sababu wamewakombolewa kutoka kwenye laana ya torati.
Wagalatia 3:13-14 '' alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti; ili kwamba baraka ya Ibrahimu iwafikilie Mataifa katika MUNGU , tupate kupokea ahadi ya ROHO kwa njia ya imani.''

Hiyo haina maana kwamba tufanye maovu yanayoleta laana tukijifariji kwamba tumekombelewa kutoka laana ya torati.
Aliyekuambia kwamba torati kazi yake ni kulaani ni nani?
Biblia hapo imeweka wazi kwamba tumekombolewa na laana ya torati ILI BARAKA YA IBRAHIMU AMBAYO MWANZO ILIKUWA NI YA WAISRAELI PEKEYAO, SASA KWA NJIA YA MUNGU BARAKA HIYO INAHUSU WATU WOTE WALIOKOMBOLEWA KWA NGUVU YA MUNGU .
Jambo la kujua ni kwamba tumekombolewa kutoka laana ya kutengwa na MUNGU na sasa kwa njia ya tunatambuliwa na MUNGU kama warithi sawasawa na ahadi aliyopewa Ibrahimu kwa wanaye.
Wagalatia 3:26-29 '' Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa MUNGU kwa njia ya imani katika MUNGU . Maana ninyi nyote mliobatizwa katika mmemvaa . Hapana Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu mke. Maana ninyi nyote mmekuwa mmoja katika . Na kama ninyi ni wa , basi, mmekuwa uzao wa Ibrahimu, na warithi sawasawa na ahadi.''

Kumbe kabla ya MUNGU kutuokoa hatukuwa uzao wa Ibrahimu na hiyo ilikuwa ni laana lakini wana MUNGU ametufanya sisi kuwa uzao wa Ibrahimu warithi sawasawa na ahadi aliyoapiwa Ibrahimu na MUNGU.
Laana ilipofutika tulihesabiwa haki kama Ibrahimu alivyohesabiwa haki kwa kumwamini MUNGU.
Leo andiko la Wagalatia 3:13 wa wengi hulitumia kuonyesha kwamba hawana laana lakini wakati mwingine maisha yao yana laana.
Kuna laana ambazo hutolewa na wanadamu kama maapizo, ndio maana ya pili ya laana na laana hizo zimewakamata wengi kwa sababu hawaombi na hawajui haki zao kwa MUNGU, Wameteswa sana na laana hizo huku wakijifariji kwamba wamekombolewa kutoka laana.
Ndugu zangu ni muhimu kujua kwamba MUNGU anaweza kukutenga na laana lakini hadi ukiamua wewe kumwita, usipomwita utabaki na laana yako.
Kuna mambo umeyaona kwenye ndoto au maono yakionyesha wachawi au wakuu wa giza wanakulaani, Usipoomba hakika laana hiyo itakupata huku wewe ukibaki kujifariji kwamba umekombolewa kutoka laana.
MUNGU alisemea ''Akawaambia mfano, ya kwamba imewapasa kumwomba Mungu sikuzote, wala wasikate tamaa-Luka 18:1''
Kama huombi hakika laana inaweza kukupata na kukutesa huku ukiendelea kujifariji.
Ndugu mmoja alilaaniwa kwamba hataolewa, ilipita miaka mingi hadi alipojua kuombea kufuta laana hiyo ndipo aliolewa.
Watumishi wengi kwa sababu labda hawajawahi kupitia laana ndio maana hufundisha kwamba hakuna laana.
Wengine husema kwamba agano jipya halijazungumzia laana lakini wanasahau kwamba MUNGU alisema kwamba wenye laana ya MUNGU wataenda jehanamu.
Mathayo 25:41 '' Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake;''

=Laana kutoka kwa MUNGU inatengenezwa na dhambi usizotubia hadi kifo chako.
Kumb 28:20 '' atakuletea laana na mashaka, na kukemewa, katika yote utakayotia mkono wako kuyafanya, hata uangamie na kupotea kwa upesi; kwa ule uovu wa matendo yako, uliyoniacha kwayo.''
= Laana ya MUNGU pia unaweza ukaipata kwa sababu ya kutokutoa fungu la kumi.
Malaki 3:9 '' Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote.''
Kutokutoa zaka kamili ni kumwibia MUNGU na jambo hilo hutengeneza laana.
Wengi hawatoi fungu la kumi wakisingizia kwamba wamekombolewa kutoka laana ya torati wakati Fungu la kumi lipo kabla ya torati. Akina Ibarahimu walitoa Fungu la kumi kwa akina Melkizedeki kipindi ambacho hata torati hajapewa Musa.
Akina Yakobo walitoa Fungu la kumi kabla hata Waisraeli hawajaenda utumwani Misri.
Nikisoma andiko la Mathayo 25:41 kwamba waliolaaniwa na MUNGU watakwenda jehanamu huwa naogopa sana.
Njia ya mbinguni ni nyembamba ndio maana hata kwa zaka tu watu hupishana na njia hiyo ya uzima.

Laana za wanadamu au majini au wakuu wa giza haziwezi kumfanya mtu asiende uzima wa milele lakini laana kutoka kwa MUNGU inaweza kumfanya mtu asiende uzima wa milele.
Laana kutoka kwa wanadamu na mawakala wa shetani zinaweza kusababisha ukateseka katika maisha ya duniani, hivyo ukihisi kuna laana inakufuatilia iwe ni kutoka kwa babu au bibi au mama au baba au mjomba au shangazi au kaka au dada au mtoto wako hakikisha tu unatubu kwa sababu ya kisababishi cha laana hiyo kisha ifute laana hiyo kwa maombi katika uwezo wa Mungu .
Laana ni jambo baya sana.


Hata makosa ya akina adamu hayakumfanya MUNGU awalaani bali aliilaani ardhi na sio wao.
Je ni lini uliiombea ardhi yao iliyolaaniwa ili laana iondoke kwa nguvu ya MUNGU na ufaidike na mazao yanayotokana na ardhi yako?
MUNGU analifundisha kanisa lake kupitia Mtume Paulo akisema tusiwe watu wa kulaani watu wengine, ni heri tuwabariki na sio kuwalaani, kuna madhara makubwa yanayotokana na laana hivyo ni heri kubariki tu.


Warumi 12:14-17 '' Wabarikini wanaowaudhi; barikini, wala msilaani. Furahini pamoja nao wafurahio; lieni pamoja nao waliao. Mpatane nia zenu ninyi kwa ninyi. Msinie yaliyo makuu, lakini mkubali kushughulishwa na mambo manyonge. Msiwe watu wa kujivunia akili.Msimlipe mtu ovu kwa ovu. Angalieni yaliyo mema machoni pa watu wote.''

Laana ni kitu kinachokukamata ili usifanikiwe kwenye jambo fulani maishani mwako.
Hakikisha laana inaondoka maishani mwako.
Kama ni laana kutoka kwa MUNGU tubu na acha uovu huo kwa kuanza kutenda mema ayatakayo MUNGU.
Zingatia hiyo itakusaidia.
Biblia inasema mtu akilaani mjini basi hata mashambani yaani kijijini atakuwa amelaani.
Kama unasumbuliwa na laana unaweza ukajaribu kufanya biashara mjini lakini hufanikiwi. Baadaea unaweza ukajaribu kwenda kijijini labda huko utafanikiwa, kwa sababu ya laana iliyo juu yako hakika hata kijijini hutafanikiwa.

Kuna watu hukimbilia mijini labda wakidhani huko watafanikiwa lakini kama laana inawasumbua hakika hata waende wapi hawatafanikiwa.
Kumb 28:16 ''Utalaaniwa mjini, utalaaniwa na mashambani.''
Dawa ya kuondoa laana sio kuhama eneo bali ni kutubu na kutengeneza kwa MUNGU Mfalme wa uzima.
Unataka kujijua kama una laana?
Kumb 28 itatujibu.
Mtu mwenye laana yuko hivi;
1. Hata ahamie eneo jingine lolote hatafanikiwa.
Kumbu 28:16 ''Utalaaniwa mjini, utalaaniwa na mashambani. ''

2. Chanzo chake cha kipato hakimpi faida yeyote.
Kumbu 28:17 '' Litalaaniwa kapu lako na chombo chako cha kukandia.''

3. Uzao wake unakuwa chini ya laana na pia Biashara au mradi anaoanzisha hafanikiwi kwa sababu viko chini ya laana
Kumb 28:18 ''Utalaaniwa uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, maongeo ya ng'ombe wako, na wadogo wa kondoo zako. ''

4. Kwa kosa la kumkosea MUNGU basi mtu huyo atakuwa mtu wa kuwa na mashaka mashaka, hukemewa, Kudhalilishwa na kutishwa bila kosa kwa sababu ya laana aliyonayo.


Kumbu 28:19-20 '' Utalaaniwa uingiapo, utalaaniwa na utokapo, atakuletea laana na mashaka, na kukemewa, katika yote utakayotia mkono wako kuyafanya, hata uangamie na kupotea kwa upesi; kwa ule uovu wa matendo yako, uliyoniacha kwayo.''

5. Kwa Kumkosea MUNGU basi Laana yake inaweza kutengeneza magonjwa mabaya.
Kumbu 28:22 ''atakupiga kwa kifua kikuu, na kwa homa, na kwa kuwashwa, na kwa hari ya moto, na kwa upanga, na kwa ukaufu, na kwa koga; navyo vitakufukuza hata uangamie.''

6. Kufungwa kwa baraka kutoka kwa MUNGU.
Kumb 28:23 ''Na mbingu zako zilizo juu ya kichwa chako zitakuwa shaba, na nchi iliyo chini yako itakuwa chuma.''

7. Kwa kumkosea MUNGU basi Mazuri anayoyatarajia yatageuka kuwa mabaya
Kumbu 28:24 '' atafanya mvua ya nchi yako iwe vumbi na mchanga; itakujilia juu yako kutoka mbinguni hata uangamie.''

8. Kwa Kumkosea MUNGU basi Adui kwenye ulimwengu wa roho watampiga.
Kumbu 28:25 '' atakufanya upigwe mbele ya adui zako; utawatokea juu yao kwa njia moja, lakini utakimbia mbele yao kwa njia saba; nawe utatupwa huko na huko katika falme zote za duniani.''

9. Atakuwa mtu wa kuonewa.
Kumb 28:29 '' utakwenda kwa kupapasa-papasa mchana, kama apapasavyo kipofu gizani, wala hufanikiwi katika njia zako; nawe sikuzote utaonewa na kutekwa nyara, wala hapatakuwa na mtu wa kukuokoa.''

10. Kupata Hasara zisizoisha.
Kumb 28:38-39 '' Mbegu nyingi utazichukua nje shambani, lakini utavuna haba, kwa kuwa nzige watazila. Utapanda mizabibu na kuitengeza, wala hutakunywa katika divai yake, wala kuichuma kwani italiwa na mabuu.''

11. Wageni au watu wapya wakija wanafanikiwa lakini yeye yuko pale pale, Pia atateswa na madeni
Kumb 28:43-44 '' Mgeni aliye kati yako atazidi kupaa juu yako; nawe utazidi kushuka chini.Yeye atakukopesha, wala wewe usimkopeshe; yeye atakuwa ni kichwa, wewe utakuwa mkia. ''

12. Akipata mali au pesa wanatokea walaji ili asifanye chochote cha kimaendeleo.
Kumb 28:50-51 ''taifa lenye uso mkali, ambalo haliangalii uso wa mzee, wala halipendelei kijana; naye atakula uzao wa ng'ombe wako wa mifugo, na uzao wa nchi yako mpaka utakapokwisha kuangamizwa;''

Hizi ni alama chache tu za mtu anaMUNGUmbuliwa na laana.
Ndugu yangu ni muhimu kujua kwamba nguvu ya MUNGU inaweza kufuta laana zote lakini ni mpaka uombe na sio kujifariji tu.
Kanuni ya laana ni kwamba mkubwa anamlaani mdogo hivyo na kuondoka laana kunahitajika nguvu kubwa kuliko mtoa laana wa kidunia.
Kama laana imetoka kwa MUNGU basi dawa ni kutubu tu kwa MUNGU na kutengeneza njia zako kwa kuanza kutenda yale ayatayo MUNGU.

MUNGU ana uwezo wa kukuweka huru kweli kweli mbali na laana, lakini hadi uamue wewe kuwekwa huru.
Yohana 8:36 '' Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli.''

Ewe mteule wa MUNGU nakuomba Mche MUNGU na timiza utakatifu wako kwa kumtii MUNGU hata katika matoleo.
Pia usitumie ulimi wako kulaani watu wa MUNGU bali laani shetani na jeshi lake.
Yakobo 3:9-10 ''Kwa huo(Ulimi) twamhimidi MUNGU Baba yetu, na kwa huo twawalaani wanadamu waliofanywa kwa mfano wa MUNGU. Katika kinywa kile kile hutoka baraka na laana. Ndugu zangu, haifai mambo hayo kuwa hivyo.''
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
MUNGU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na MUNGU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee MUNGU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa MUNGU Kwako.

MUNGU AKUBARIKI.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom