Hivi kweli Watanzania ndio tumefika hapa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi kweli Watanzania ndio tumefika hapa!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ibrah, May 22, 2012.

 1. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #1
  May 22, 2012
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  MWANANCHI leo limeripoti kuwa wakazi wa Handeni wamefanyia mapokezi makubwa, Waziri wa Viwanda na Biashara Dk Kigoda na kumpongeza kwa kufanya uamuzi wa kumsimamisha kazi Bw Ekerege aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa TBS. Wiki iliyopita magazeti yaliripoti kufanyiwa mapokezi makubwa kuwapongeza Wabunge wa Mwibara wa Ludewa kwa kutetea maslahi ya nchi Bungeni.
  Tabia hii ambayo imeanza kuibuka inashangaza na kusikitisha, maana WaTz tunaanza kufikiri kuwa viongozi kutimiza wajibu ni fadhila! Hii ni aibu kubwa.
   
 2. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #2
  May 22, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,785
  Likes Received: 2,395
  Trophy Points: 280
  Huko morogoro napo wanaandaa mapokezi makubwa ya omari nundu
   
 3. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #3
  May 22, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Uongo mwingine hauna hata haya. Omar Nundu anatokea Tanga si Morogoro na jana ameingia Tanga kimya kimya hakuna mapokezi yoyote tuliyoyasikia.
   
 4. K

  Kahinda JF-Expert Member

  #4
  May 22, 2012
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 849
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 60
  Mkuu
  kama utafuatilia kamanda wa polisi aliyasitisha maandamano hayo.
   
 5. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #5
  May 22, 2012
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Lakini ni ukweli wana Tanga walikuwa wanajipanga kwa mapokezi makubwa ya Omar Nundu.
   
 6. Ralphryder

  Ralphryder JF-Expert Member

  #6
  May 22, 2012
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 4,588
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Yaani kama ulikuwa na mimi mawazoni! Ni ulimbukeni! Tena haka kamtindo kanaziiiiidi Kukua! Yaani sipendi.
   
 7. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #7
  May 22, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,185
  Trophy Points: 280
  Naamini ni George Orwell aliyesesema uozo unapozidi katika nchi, hata yule atakayefanya kazi kama kawaida na kusema ukweli tu ataonekana kafanya kitu cha ushujaa wa kimapinduzi.

  Ndicho kinachotokea hapa.
   
Loading...