Hivi Watanzania ndio tumefika hapa!

Ibrah

JF-Expert Member
Mar 22, 2007
2,729
528
MWANANCHI leo limeripoti kuwa wakazi wa Handeni wamefanyia mapokezi makubwa, Waziri wa Viwanda na Biashara Dk Kigoda na kumpongeza kwa kufanya uamuzi wa kumsimamisha kazi Bw Ekerege aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa TBS. Wiki iliyopita magazeti yaliripoti kufanyiwa mapokezi makubwa kuwapongeza Wabunge wa Mwibara wa Ludewa kwa kutetea maslahi ya nchi Bungeni.
Tabia hii ambayo imeanza kuibuka inashangaza na kusikitisha, maana WaTz tunaanza kufikiri kuwa viongozi kutimiza wajibu ni fadhila! Hii ni aibu kubwa.
 
hata sisi hapa dar tunaandaa maandamano makubwa ya jk kubadilisha baraza la mawaziri,
mbona CUF walimpokea mwenyekiti wao kwa maandamano makubwa!
 
Kuwapokea kishujaa ni appreciation ya kuthubutu kwao kufanya kile ambacho mawaziri na wabunge wengine Vilaza walishindwa kutekleleza japo ulikuwa na wajibu wao! sio kulipa fadhila hata kidogo la hasha; just a pat on the back, Hukuona wachezaji wa Chelsea walivyomuangukia Drogba baada ya kupiga penalti ya ushindi!! give credit where it is due, usijichanganye; loosen your stiff neck!! thats a form of motivation to keep up doing the good job
 
Back
Top Bottom