Hivi kweli wanaume tumekosa confidence kiasi hiki, kwamba bila gari huwezi kung'oa vimwana wakali?

The Evil Genius

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
5,457
17,240
Habari ya muda huu wakubwa.

Jamani kizazi hiki cha sasa cha wanaume tumekosa kujiamini kiasi hiki kwamba bila pesa wala gari hatuwezi kuopoa vidosho wakali?

Je wanawake wa sasa wamebadilika kiasi hicho kwamba akili yao na mawazo yao yako kwenye gari na pesa hadi tujiaminishe kua bila gari na pesa hatuwezi kuwapata?

Mbaya zaidi bado mtu anaweza kua na hiyo gari bado akakosa kujiamini kwa mwanamke mzuri.

Kama gari ni kwa ajili ya kuwapata wanawake wasio na magari, je mwanamke mwenye gari utamuingia kwa gia gani kama akili zetu ziko kwenye magari ili tuwapate wasio na magari.

Wanaume wa kizazi hiki tumepatwa na nini hadi kupoteza confidence kiasi hiki?
 
Huo utafiti umeufanyaje na wapi umefanyia, tupo tunabeba mademu kwa chips shingo mbili za kuku. Kwa wale wanajifanya matawi basi ni sound tuuu na baby nyingi mtoto analewa na hela anatoa yeye
 
Bandiko lako limenifanya nijiulize maswali.

1. Kung'oa huko mademu ni kwa ajili ya kulala nao tu au wawe wapenzi wetu?

2. Hivi mapenzi ni lazima tu-base kwenye maamuzi ya mwanaume tu au na huyo mwanamke hana maamuzi? Hana vigezo vya kuchagua?

3. Kama wewe ungekuwa mwanamke ungetumia vigezo vipi kumkubalia mwanamke?

Wakati unabadilika, siku hizi hakuna kutongozana. Mnakuwa wapenzi bila hata kujua mmekuaje na kila mmoja akimchoka mwenzake anapotea kimyakimya.

Wanawake wa siku hizi sio wale shangazi zetu wa 'shida na raha'.
 
Babu dunia siyo static mambo yamebadilika sana.Mimi nimesota na guta lakini watoto wote nimeambulia kuwasalimia "habari za leo" yaani hata mambo hawataki kuitikia ila wenye magari hata wakijisahau kutoa kamkono tu nje wanaitikia salamu zao kwa haraka sana
 
Tatizo majority ya Dada zetu siku hizi akili zao ziko kwenye usafiri na wallet... Hlf wanaume wa siku hiz siyo kama wale wa kufuatilia jibu miez 4 hivyo wanaangalia the quickest and hustle free way ya kumpata mdada anayemtaka which is pesa na usafiri... Yani suala la sound tupu siku hizi lina changamoto
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom