Wale watu wabaya wasiokuwa na mvuto hata ukimuangalia hapendezi machoni, sura mbaya wapo wapo tu lakini wanakuwaga wanaringa hao utasema wanamiliki dunia kumbe hamna kitu [emoji23][emoji23] mvuto hawana pesa hawana ila wanaringa hao [emoji23] wenyewe wanajikutaga wazuriiiiii. Wewe kama unajijua mbaya usiwe unaringa mkiringa ndio mnazidi kuwa wabaya [emoji23]
Kweli wanaume tumeumbwa tofauti!
Hivi unaweza ukahoji maringo ya mwanamke?
Basi uje uhoji pia kwanini mtetea unaliringia jogoo, halimpati kiurahisi hadi libake, kwanini?
Vitu vingine wameumbwa navyo ni vya asili si vya kuhoji.
Maringo sawa na pilipili kwenye mboga, ni kiungo kwa ajili ya kuchangamsha tu hakina madhara yoyote.
Mimi mwanamke mrahisi simpendi, ninamuweka kwenye group la viruka njia na kumtoa thamani.
Mwanamke mgumu, mwenye nyodo za waziwazi, ndiye kwangu mwanamke bora ninaye mpenda, bila kujali sura yake.
Nimuingie anitolee nje kwa nyodo! Dah!
Swali huwa ni moja tu linalojengeka akilini mwangu 'anaringia nini?'
Hilo swali hunisukuma kuanza kumfuatilia, kwa kutamani kukiona kwa macho kile anachokiringia.
Umeona sasa faida ya maringo?
Halafu kwa taarifa yako, hakuna mwanamke mbaya wa sura.
Unayemuona mbaya wewe, siyo chaguo lako hilo, ni chaguo la wenzako na kesho utakuta huyohuyo kachumbiwa na kaolewa, hivyo hakuna mbaya.
Ama unayesema wewe mbaya, kesho utakuta kaumiza mtu kihisia na kasababisha mtu ajinyonge kwa ajili yake.
Ndiyo maana ya msemo: wewe wasema cha nini, wenziyo wanawaza watakipata lini?