Jitahidi usiwe kikwazo kwenye maisha ya watu, watu wanapambana sana kutafuta mkate

Song of Solomon

JF-Expert Member
Aug 5, 2021
2,733
5,490
Ukweli ni kwamba kila binadamu anatakiwa awe na maono, mtazamo, malengo na dhumuni lakuishi iliwa ni kama Ramani yake inayomuongoza kule ambapo yeye anapataka, kwa bahati mbaya zaidi hakuna mwenye uhakika wa kuishi milele ila uhakika wa kuishi kwa malengo, dhima na amani ya moyo itategemea wewe umejipangaje na unajionaje

Kitu cha msingi ni kwamba hatuwezi kuona kesho kitatokea nini ijapo tunaweza kutabiri tu aidha ikatokea kweli tulichotabiri au kisitokee, na ndio hivyo hivyo katika uhai hatujui kama tukilala leo kama kesho tutaamka kwasababu wapo watu ambao unaposoma nakala hii walikuwa wanauhakika leo wataamka lakini hawakufika.

Dhumuni ni nini kama unajua hakuna atakaeishi duniani milele basi usijekweze, usitumie nafasi yako kuwaumiza wengine, usitumie fedha zako kama fimbo ya kuwaonea wengine, usitumie taaluma yako kuwadidimiza wengine kwasababu IPO SIKU RAFIKI YAKO, NDUGU NA JAMAA WATAPOKEA SIMU NA KUPEWA TAARIFA YA KIFO CHAKO, hapo huna ujanja tena, kila kitu utasaidiwa kuanzia kuoga, kubebwa mpaka kulala maana yake huna nguvu na haki tena hapa DUNIANI. Ishi na watu vizuri kwa upendo, saidia watu na kama huwezi kuwa daraja kwao basi usiwe ukuta wa kukwamisha safari zao

Wapende wote usiwabague na asiyekupenda basi mtoe kwenye mfumo wako ila usimfanyie ubaya upo siku utamuhitaji kwasababu hata maji machafu hutukika kuzimia moto
Heshimu kila mtu bila ya kujali hali zao na hadhi zao, kwasababu wanaochimba kaburi, wanaobeba jeneza ni watu wa kawaida sana. Watu wakawaida ndio watakulilia kuliko hao unaoona marafiki zako
Saidia watu kama unacho kwasababu kile unachokitoa ndicho utachoongezewa na ipo siku msaada uliyotoa unaweza ukakusaidia sehemu ambayo wewe hukutarajia (hata ushauri mzuri pia ni msaada)
Kuwa "HUMBLE" , ukipata nafasi, cheo, hadhi au fedha usijilweze na ukawadharau watu, kumbuka kabla hujafika kwenye hali uliyonayo sasa hivi kuna watu walikuwa hapo na wamepita na sasa hawapo tena, ukiwa na fedha nyingi usitumie kuwanyoosha wenzio na kuwakebehi hakuna mtu asiyependa kuwa na hela ni basi tu muda huwa unatofautiana, kwasababu kuna watu wanafanya kila kitu na bado hawapati wanachotaka, na pia ukiwa na pesa usitumie kujifaharishia kwasababu pia kuna watu wanazo nyingi zaidi ya kwako halafu wako poa tu na wala hawaringi.

Ishi kwa upendo, upendo huanza na wewe mwenyewe jipende, jijali, jithamini, na jiamini,,ukianza kujipenda basi utaona utakavyokuwa na furaha na utahamisha upendo kwa wengine na kusambaza furaha kwa watu waliokata tamaa. Kumbuka upendo ni kama taa hung'arisha kwako na kwa wengine hivyo ukimuona mtu anachukia watu wengine basi ujue hata yeye mwenyewe hajipendi na anajidanganya kama anafuraha. Upendo huvuta watu wema kwako na huwabadili watu wabaya kuwa watu wema kwasababu kupitia upendo wako unawatibu maumivu yao yaliyowafanya kuwa watu wabaya.

Jitahidi usiwe kikwazo kwenye maisha ya watu, watu wanapambana sana kutafuta mkate wa familia zao, hivyo ukiwawekea kikwazo kwenye mishemishe zao utakuwa unaangamiza kundi kubwa la watu ambao hawana hati. Mtu ukikosea tafuta njia nzuri ya kumrekebisha na sio kumkomesha.Hakuna mtu mbaya ni basi tu maisha hutubadilisha kulingana na maumivu tuliyopitia.

NB: JITAHIDI SANA UKIONDOKA HAPA DUNIANI UACHE KUMBUKUMBU NZURI KWA WATU, NA HIYO ITABAKI KUWA KETE YAKO YA MWISHO YA KUKULETEA BARAKA HUKO UTAKAPOKWENDA.*
 
Sasa kama Mimi polisi ..ili nipate mkate wangu na Mimi naagizwa kuja kukumata wewe unaeuza Gongo au madawa ili upate mkate wako...
Inawezekana kweli nisiwe kikwazo Kwa mkate wako??
 
Na usidalalie bandari za Watanganyika kwa vijisent vya wajomba zako ukidhani utaishi milele
 
Sasa kama Mimi polisi ..ili nipate mkate wangu na Mimi naagizwa kuja kukumata wewe unaeuza Gongo au madawa ili upate mkate wako...
Inawezekana kweli nisiwe kikwazo Kwa mkate wako??
The Boss, biashara ya gongo ni biashara haramu huwezi kujenga hoja kwa mfano huo mkuu
 
Back
Top Bottom