Hivi kwanini wasitajwe majina yao...?! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi kwanini wasitajwe majina yao...?!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Wa mmoja, Aug 10, 2009.

 1. Wa mmoja

  Wa mmoja Member

  #1
  Aug 10, 2009
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 99
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nauliza hivii kwanini hawa mafisadi wasitajwe kwa majina?Yani majina yao yaanikwe hadharani halafu waadabishwe,labda kidogo inaweza ikasaidia kuwapunguza ikiwezekana kuwamaliza kabisa,maana hawa ndio wanaotunyonya sisi wa hali ya chini!
  Muheshimiwa Kikwete kama anayo LIST ya majina yao aiweke hadharani,labda itasaidia,au anaogopa 2010?!
   
 2. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #2
  Aug 10, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  mkuu kwani huwajui?
   
 3. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #3
  Aug 10, 2009
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Ingekuwa vizuri kama kina Malecela, Sitta na hata mama Maria Nyerere wataje fisadi ni fulani na fulani. Hawatusaidii pale wanaposema kuwa mafisadi watapata shida uchaguzi ujao, mafisadi wana utajiri wa kutisha, nchi inaliwa na mafisadi, mafisadi wameifikisha nchi hapa ilipo, na kadhalika.

  Kila kiongozi aliye na ujasiri wa kupigana vita dhidi ya ufisadi, awataje hao wanaoitwa mafisadi.

  Naungana na mleta hoja kwamba hili fumbo na kitendawili cha MAFISADI lifumbuliwe au kuteguliwa.

  MAFISADI NI KINA NANI ENYI MZEE MALECELA, SITTA NA MAMA MARIA.
   
 4. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #4
  Aug 10, 2009
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Mbona wanatajwa kila siku hapa ukumbini? Ulitaka viongozi wenyewe watajane wakati wao wenyewe ni mafisadi??
   
 5. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #5
  Aug 10, 2009
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Tumechoka na mafumbo, Spika Sitta aseme FISADI ni nani, Malecela awataje hao MAFISADI ni kina nani, Mama Maria awataje hao MAFISADI ni kina nani.

  Kama hawa wanaotajwa humu ndio MAFISADI, basi mwanasheria Sitta athibitishe kwa kuwataja kuwa fulani na fulani waliotajwa JF ndio hao MAFISADI WANAOIMALIZA NCHI. Sitta taja huyo mwenye majumba ni nani? Kwa nini unamuogopa mheshimiwa wa Speed na Standard? Tunakuaminia Mheshimiwa Sitta, huogopi kitu, taja usiogope taja.
   
 6. Mchaga

  Mchaga JF-Expert Member

  #6
  Aug 10, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,371
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  kwani kuna wapya?
   
 7. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #7
  Aug 10, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Jamani hamjui kwamba CCM wanatufanyia mchezo wa kuigiza hapa?

  CCM wana kale kamsemo kao ka: "HUYU NI MWENZETU". Hako ka msemo ndiko kanawatesa sana maana wana oneana aibu kutajana hadharani wakti wanajuana kabisa nani fisadi PAPA na nani fisadi NYANGUMI.

  Kwa watu tulioko nje ya CCM wote tunawajua hao mafisadi kuanzia MANYANGUMI mpaka MAPAPA. Tatizo la CCM wanafikiri bado Watanzania wako kwenye ujima wa miaka ya 47 ambako habari zilikuwa zinachujwa kwanza ndipo zinatawanywa na vyombo vya propaganda vya CCM enzi hizo TANU. Hamkumbuki kuwa enzi za Mwalimu hata kuwa na TV ilikuwa ni kosa la jinai katika Tanzania??

  Nasikia ungo wa TV ulikuwa Msasani na Mwitongo(Butiama) peke yake. Mwenyekiti wa Chama akiangalia kwenye luninga habari za nchi za nje na utabiri wa hali ya hewa anaenda RTD au anaitisha kikao cha Wazee na kujifanya anatoa utabiri wa hali ya hewa kuwa mwaka huu kutakuwa na ukame au mvua nyingi. Hapo Wadanganyika wote wanamwona kama vile ni nabii. Ndiyo maana marehemu Nyerere watu walikuwa wanamwita Mzee Kifimbo sababu ya kile kijifimbo chake alichokuwa anatembea nacho kuwa ni cha uchawi na uganga.

  CCM wanapaswa wajue enzi hizo zimepita. Dunia ya sasa imekuwa ni kijiji,habari zinaenea kwa kasi ya moto wa petroli. Huwezi kufanya madudu yako iwe ni Ikulu,Nje ya Nchi au hata kijijini ambako unadhani hakuna chombo cha habari na ujione kuwa uko salama. NEVER!

  Watanzania wote tunajua madudu aliyoyafanya BWM pale jumba jeupe. Hata watoto wadogo wanajua jinsi Mkapa alivyoiuza na kuibinafsisha Tanzania kwa wageni kwa sera za kipuuzi za Utandawizi na Ugenishaji.Tunajua alivyotengeneza ANBEM yake pamoja na utapeli wa ununuzi wa mgodi wa Makaa ya Mawe kule KIWIRA kwa kujifanya ni mwekezaji huku akilipa Tshs. 70m tu kati ya 700m na pesa yote aliyobaki akatia ndani huku akiwaacha wafanyakazi wa mgodi wakihaha mpaka kesho.

  Richmond tumesikia juzi wakati wa kuahirisha Bunge. Ulikuwa ni usanii mtupu kwenye ripoti ya serikali iliyotelewa kama utekelezaji wa maazimio ya Bunge kuhusu kuwawajibisha watuhumiwa wote wa Richmond. Ripoti ile imekuwa ni aibu na fedheha kubwa kwa Utawala wa Rais JK.

  Kama alivyosema Mbunge machachari wa CHADEMA Dk.Wilbroad Slaa kuwa kama Serikali ya CCM isipokuja na ufumbuzi wa kadhia hii kwenye kikao cha Bunge la Novemba, basi Bunge ilivunjwe na Rais aitishe uchaguzi Mkuu kabla ya 2010.

  Hapo ni patamu kweli kweli. Yaani Richmond itakuwa imeweka historia ya aina yake kwa wATANZANIA. Yetu macho na masikio yanasubiri kitakachojili hapo Jumba la Bunge mwezi wa Novemba.

  Je, CCM watakuwa na ubavu wa kuwawajibisha mafisadi wa Richmond au Watajitoa muhanga kuvunja Serikali na kuitisha uchaguzi Mkuu mwaka 2009 badala ya 2010?
   
  Last edited: Aug 10, 2009
 8. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #8
  Aug 10, 2009
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,458
  Likes Received: 1,331
  Trophy Points: 280
  itapendeza wakitajwa ili tuwajue, wanapotuambia mafisadi watapata shida uchaguzi mkuu sio kweli labda watutajie hao watu ili tusiwachague lakini kwa maneno ya kisiasa hawawezi kuwaondoa
   
 9. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #9
  Aug 10, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,312
  Likes Received: 5,600
  Trophy Points: 280
  Wanatajwa kila siku.......ila serikali inasema hawana ushahidi wa kutosha....sasa kama walienda front wakachukua....wanataka ushahidi gani????
   
 10. H

  Haika JF-Expert Member

  #10
  Aug 10, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,318
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Mimi nasema hakuna fisadi kwa ujumla, labda tupewe definition.
  kila mtu ashitakiwe kwa kosa lake la binafsi, wengine wametumia madaraka kwa uzembe, wengine wameingia mikataba mibovu, wengine wameiba au wameshiriki kuiba mali ya serikali, wengine wametoa maamuzi mabovu, wote ni adui zetu, kila mmoja anagoma kuitwa fisadi kwa kuwa tu hajaiba chash, au hajatajwa na slaa.
  basi kila mtu abebe mzigo wake kwa defn ya tendo alilolitenda.
  muuza madawa aitwe muuza madawa.
  mzembe aitwe mzembe kn, ila wote washitakiwe.
   
 11. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #11
  Aug 10, 2009
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
 12. t

  tarita Senior Member

  #12
  Aug 10, 2009
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 156
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  soma list aliyoitaja comrade Mengi
   
Loading...