Dharau ni tabia asilia ndgu yangu haijalishi upo bongo au nje ya bongo.Kuna baadhi ya wabeba box hapa JF wamejaa dharau sana nakuwaona kama waliopo home hamnazo ila wao washavuka maji ndio wana akili acheni tabia za kipuuzi hizo kuishi nje ya nchi sio kuwa unajua kila kitu ,
merry x mass NN,ukimwona Lizzy mpe hi.
Nadhani kiustaarabu ungeanza kwanza kujitazama wewe mwenyewe na kuona aibu kwa kuwaita wenzio wabeba box.Hiyo ni dharau kubwa sana kwa binadamu mwenzio.Utakapoacha kuwaita hivyo labda na wao wanaweza kuacha kukudharau..
Paka mweusi, hilo jina mimi nimelikuta hapa jf kwa hiyo naendeleza mila nasidhani kama mtu akikuita mbeba box ni tusi,kama hubebi haiwezi kukukwaza lolote
Now you are talking,nachoweza kukuuliza ni kuwa kama umelikuta hilo jina hapa JF,Je ulijaribu kujiuliza au kufuatilia lilitoka wapi na lina maana gani kabla ya kulitumia.Ni sawa na kwenda sehemu ambayo wewe ni mgeni na kuanza kutumia majina uliyoyakuta bila kuelewa yana madhara gani kwa waliopewa majina yao.Nitakupa mfano mdogo tu,katika wilaya ya Kahama kuna mzee mmoja anajulikana kama mzee Makonyeza kwa sababu ya jinsi anavyoangalia,lakini kwa mwenyewe endapo utamuita hivyo yuko radhi hata kukupiga risasi.Sasa kama utaweza kufika sehemu hiyo na kumkuta huyo mzee utaweza kumuita Makonyeza kwa utetezi kwamba na wewe jina hilo umelikuta....
Watakuwa wamekuudhi kweli mkuu. Pole, just ignore them!
Kwani uongo?Mbongo akiwa nje utamjua tu kwa swaga zake ,utamsikia kama unabishana nae jambo atakuambia, tatizo hujatembea wewe yaani hapo anajitambulisha yeye katembea, hiyo ni moja katika tabia za wabeba box
paka mweusi naomba nikujuze tu kuwa mzee makonyeza amefariki miezi kama 2 iliyopita, anaitwa said salum namfaham vizuri
Oh,sikuwa na taarifa nashukuru kwa taarifa hizo,apumzike kwa amani,ila nilikupa mfano wake nikijua kuwa utakuwa unamfahamu japo si kwamba kila mtu anamfahamu..Sasa tukirudi katika mada yetu nadhani si jambo jema kuwaita watu walio nje ya Nchi wabeba mabox ,tutumie ustaarabu wa kawaida tu wa kuheshimiana na hizi kashfa na dharau zote zitaisha mwishoni...
Now you are talking,nachoweza kukuuliza ni kuwa kama umelikuta hilo jina hapa JF,Je ulijaribu kujiuliza au kufuatilia lilitoka wapi na lina maana gani kabla ya kulitumia.Ni sawa na kwenda sehemu ambayo wewe ni mgeni na kuanza kutumia majina uliyoyakuta bila kuelewa yana madhara gani kwa waliopewa majina yao.Nitakupa mfano mdogo tu,katika wilaya ya Kahama kuna mzee mmoja anajulikana kama mzee Makonyeza kwa sababu ya jinsi anavyoangalia,lakini kwa mwenyewe endapo utamuita hivyo yuko radhi hata kukupiga risasi.Sasa kama utaweza kufika sehemu hiyo na kumkuta huyo mzee utaweza kumuita Makonyeza kwa utetezi kwamba na wewe jina hilo umelikuta....
Kuna baadhi ya wabeba box hapa JF wamejaa dharau sana nakuwaona kama waliopo home hamnazo ila wao washavuka maji ndio wana akili acheni tabia za kipuuzi hizo kuishi nje ya nchi sio kuwa unajua kila kitu ,
Ngongoseke, wewe pia c upo hukohuko kwa wabeba mabox, vipi tena mmepishana kauli ninyi kwa ninyi!