Hivi kwanini vyombo vyetu vya habari vya runinga havina habari zilizovunjika vunjika (Breaking News)?

ibanezafrica

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,261
6,543
Yaani channel zote hadi saa hizi wanaendelea na vipindi vyao vya kawaida kana kwamba hakuna kilichotokea!

Hii si mara ya kwanza, japo kidogo clouds 360 wamerusha sauti ya Mkuu wa Mkoa Morogoro akitoa taarifa ya ajali hiyo mbaya ya moto

TBC nao hata habari hawana! Hivi hivyo vyumba vya habari si huwa mna wawakilishi Wanahabari mikoani na wana kamera sasa mnashindwa wapi? Mbona CNN, BCC huwa wepesi kujiunga na kutoa taarifa na majanga kwa jamii?

Jirekebisheni...huu ni wajibu wenu vyombo vya habari hasa TVs.

Inasemekana zaidi ya watu mia wanaweza kuwa wamepoteza maisha, nyie ndio wa kutujulisha amkeniiii.
 
Yaani hadi saa hizi bado dkk 10 kufika saa tano,Itv wana kipindi cha usafiri wako,Tbc machinga smart,Channel ten tamthiriya ya kichina,Star tv,clouds,Utv wote wameweka playlist ni video za nyimbo kwa kwenda mbele! Wakati taifa tumepatwa na msiba mkubwa karibu masaa mawili yanafika sasa!
 
Juzi hapa nilikua naangalia Live CNN tukio la al paso marekani yule kijana aliyeshambulia watu ktk mall.
Watu 20 walipoteza maisha hii nasikia huenda zaidi ya watu mia lkb vyonbo vya habari kimyaaaaaa...utasikia wanasema taarifa kamili tutawaletea saa mbili usiku kwenye taarifa ya habari!
 
Mkuu, matangazo live yanayoruhusiwa ni hotuba za Raid,Waziri Mkuu na Makamu wa Rais
 
Mkiambiwa hapa hakuna wasomi wa mambo haya ya tansinia ya habari mnabisha Tz imejawa na wambea tu na siasa uchwara sio wanahabari walio na taaluma ya kueleweka
 
Yaani channel zote hadi saa hizi wanaendelea na vipindi vyao vya kawaida kana kwamba hakuna kilichotokea!na hii si mara ya kwanza,japo kidogo clouds 360 wamerusha sauti ya mkuu wa morogoro akitoa taarifa ya ajali hiyo mbaya ya moto
Tbc nao hata habari hawana!hivi hivyo vyumba vya habari si huwa mna wawakilishi ma reporter mikoani na wana kamera sasa mnashindwa wapi?mbona cnn,bbc huwa wepesi kujiunga na kutoa taarifa na majanga kwa jamii?jirekebisheni...huu ni wajibu wenu vyombo vya habari hasa tvs.
Inasemekana zaidi ya watu miawanaweza kuwa wamepoteza maisha.nyie ndio wa kutujulisha amkeniiii.
wanaogopa watashtakiwa kwa kuleta taharuki
 
Yaani hadi saa hizi bado dkk 10 kufika saa tano,Itv wana kipindi cha usafiri wako,Tbc machinga smart,Channel ten tamthiriya ya kichina,Star tv,clouds,Utv wote wameweka playlist ni video za nyimbo kwa kwenda mbele! Wakati taifa tumepatwa na msiba mkubwa karibu masaa mawili yanafika sasa!
Itv walirusha baadae ndio wakaanza hicho kipindi cha usafiri wako
 
Tv zina hasira ya kufungiwa kwenye visimbuzi ukiwacheck kwa sasa kama vile wameishiwa pumzi.
 
Aljazeera wameripoti tukio hili vizuri sana tena chumba cha habari wamejiunga na repoter aliyepo Nairobi
 
Yaani channel zote hadi saa hizi wanaendelea na vipindi vyao vya kawaida kana kwamba hakuna kilichotokea!na hii si mara ya kwanza,japo kidogo clouds 360 wamerusha sauti ya mkuu wa morogoro akitoa taarifa ya ajali hiyo mbaya ya moto
Tbc nao hata habari hawana!hivi hivyo vyumba vya habari si huwa mna wawakilishi ma reporter mikoani na wana kamera sasa mnashindwa wapi?mbona cnn,bbc huwa wepesi kujiunga na kutoa taarifa na majanga kwa jamii?jirekebisheni...huu ni wajibu wenu vyombo vya habari hasa tvs.
Inasemekana zaidi ya watu miawanaweza kuwa wamepoteza maisha.nyie ndio wa kutujulisha amkeniiii.
Maisha ya mtu hayana thamani kubwa Tanzania.

Marekani wiki illiyopita mtu kaua watu Walmart imekuwa habari moja hiyo hiyo CNN wanaiongelea na kuichambua kutoka kila angle siku nzima.

Jumapili huwa sikosi kipindi cha Fareed Zakaria, nikaona Jumapili iliyopita kipindi kimefutwa, kwa sababu CNN waliona si sawa kuongelea siasa za mambo ya nje wakati nchi ina msiba mkubwa.

Tanzania wamefariki watu 62 kwa moto mkubwa, lakini vyombo vya habari vinaweza kuendelea kama kawaida, tena vingine vinaweza kuongeza muziki kama vinasherehekea.
 
Back
Top Bottom