SoC03 Kero yangu kwa vyombo vya habari televisheni na redio

Stories of Change - 2023 Competition

gaspern gaspal

New Member
May 12, 2023
2
1
Naandika kuhusu mambo ambayo yamekuwa yanafanyika mwenye vyombo hivi vya habari pendwa na vyenye watumiaji wengi. Katika miaka ya hivi karibuni kumekuwa na ukuaji mkubwa wa tasnia hii ya habari hapa nchini, lakini katika ukuaji huo kumekuwa na mambo ambayo yanafanyika au kufanywa ambayo yanakua kama kero Kwa sisi watumiaji/ wasikilizaji.

Mambo yamekuwa yakijitokeza karibia katika redio na televisheni hasa hizi zilizo anzishwa katika miaka ya karibuni. Mimi kama mtumiaji huwa yananikera kuona yakitokea na Nina hisi sio mimi pekee angu huwa yananikera hata watumiaji wengine.

Basi natumia hii nafasi adhimu kuyasema na kutoa mapendekezo yangu Kwa wahusika. Mambo hayo yanayotukera sisi watumiaji wa redio na televisheni ni;

1. Kurusha aina matangazo ambayo yana maudhui yasiyopendeza kama watazamaji au wasikilizaji wapo pamoja na ni wa jinsia na rika tofauti.
Kwaio mfano tangazo linatolewa kwenye televisheni lina mwonyesha mwanamke makalio yake ambayo pia ni makubwa. Tangazo kama hilo unakuta linarushwa wakati wa mapumziko ya taarifa ya habri saa 2 usiku, muda huu unakuta familia nyingi wapo mezani wanakula. Sasa apo yupo baba, mama, watoto wap wakike na wakiume na hata ndugu wengine. Kwaio mchananyko wa watu kama huu tangazo kama hili linakuwa kero kwa hawa watumiaji wote.

Mapendekezo yangu Mimi kwa kuwe na uhariri mkubwa wakuaanda haya matangazo ili kutoa hii hali kama kuzalilishana mbele ya watumiaji wa rika na jinsia tofauti tofauti. Au kuwe na tahadhali kabla ya kurushwa hewani kuwafikia walengwa.

2. Kero yangu ya pili ni matangazo ya biashara kuchukua muda mrefu.
Unakuta tangazo moja la biashara linachukua muda hadi dakika tano. Hizo dakika tano unakuta niza lenyewe kujieleza baada ya kurushwa unakuta na mtangazaji anarudia kuliongelea naye anachukua dakika hata tano tena. Unakuta tangazo moja linakuwa na kama dakika hata kumi. Kero hii imekuwa ukifanyika hasa kwenye redio, hasa hizo redio za mikoani. Kwaio tangazo moja kuchukua muda wote huo linakuwa kero kwetu sisi wasikilizaji kwa sababu na kuwa na choshwa na kusikiliza kitu kimoja Mara nyingi. Wakati malengo yangu Mimi nasilkiliza kipindi ili nipate burudani kwa mfano napo sasa nachoshwa naweza hata kuhairisha kuendelea kusikiliza.

Mapendekezo yangu Mimi matangazo ya biashara yawe yanaandaliwa kwa weredi ili yenyewe yajieleze. Ili yakimfikai msikilizaji au mtazamaji aweze kuelewa. Na Mara nyingi matangazo yanayoeleweka huwa yanakuwa na maelezo machache sana .

3. Kero ya tatu ni matangazo ya biashara kurudiwa Mara nyingi.
Unakuta tangazo linarushwa hewani pengine wakati kipindi kinaanza hata nusu saa haijaisha mtangazaji akaaliongelea alafu Akaliweka tena hewani. Apo sasa unakuta kwenye kipindi cha saa moja unasilkiliza tangazo Mara nyingi hadi unakereka na kipindi chote. Mwanzo redio na televisheni zilikuwa zinarusha tangazo ni kama Mara tatu kwa kipindi cha saa moja. Tangazo moja kipindi kinapo anza, lapili katikati ya kipindi na la tatu anapomaliza kipindi.

Napendekeza matangazo ya biashara yawe yanarushwa angalau Mara tatu ka zamani na kusiwe na maelezo mengine kutoka kwa mtangazaji kuanza kutuelezea wakati tangazo lenyewe linajieleza.

4. Kero ya nne vipindi vingi kukosa maudhui kwa watumiaji.
Hii kero ipo unakuta kipindi kinarushwa na watangazaji watatu sasa hao watangazaji muda mwingi wanatumia kutueleza mambo yao kama maisha yake , amevaaje na mambo mengine. Kipindi kinaanza wanaanza kwa kuongea mambo yao kama ni jumatatu unakuta wanaanza kwa kupiga stories za weekend walikuwa wapo na akina Mani. Mambo ambayo sisi wasikilizaji hayatusaidii chochote na wala sio malengo yetu yakuwasikiliza. Wanaweza wakatumia hata dakika kumi kuongelea mambo yao ya weekendi bila kujua kuwa sisi wasikilizaji wanatuchosha na wala hatuhitaji kujua. Au wanaongea habari za walikokwenda kunywa pombe kitu ambacho kuna wasikilizaji wengi sio habari njema kwaio kuzisikia.

Nilkua napendekeza watangazaji wawe wanakuja kwenye vipindi wakiwa wamejiandaa na maudhui ya kipindi chake kama nicha burudani aje akida na habari za burudani na sio kuja kwenye kipindi na habari sake binafsi au za watu fulani. Kwa kufanya hivyo wataweza kutupa kile sisi watumiaji wao tunataka kama burudani au kuelimishwa au kujuzwa.

5. Kero yangu ya tano ni kubadilishana watangazaji kama wachezaji wa Mpira.
Hii kitu imeibuka hivi karibuni hasa kwa rediona televisheni hizi mpya , unakuta mtangazaji alikuwa wa redio au televisheni hii unamkuta yupo kwenye redio/televisheni nyingine kitu ambacho kwa zamani mambo hayo hayakuwepo. Kwa kufanya hivyo kumekuwa ni kudumaza tasinia ya habari kwani wanakuwa wanazuia watangazaji wapya kuingia katika tasinia hii. Au pengine mtangazaji mmoja kuwa na redio au televisheni zaidi ya Moja. Huku kunakuwa unaziba nafasi kwa wanahabari wapya kupata nafasi ya kutangaza na hatimaye kurudisha nyuma tasinia ya habari na hata kufa kabisa.
Katika jambo hili Mimi nilikuwa napendekeza kuwepo na utaratibu ambao utawafanya hawa watangazaji watakuwa na redio au televisheni moja tu ndani ya nchi moja. Kama akishindwa kufanya hivyo wawe wanabadilishwa kitengo pale anapoenda kwenye redio na televisheni nyingine. Kwa mfano kama alikua mtangazaji wa redio moja anapoenda kwenye redio nyingine awe mhariri.

Hitimisho
Redio na televisheni ni moja ya vyombo vya habari vinavyotumiwa na watu wengi hapa nchini hivyo basi tunawaomba muwe na weledi katika kutimiza majukumu yenu. Maana kama mtashindwa kufanya majukumu yenu kutaleta kubwa katika jamii. Kama vile mmongonyoko wa maadili, mkakosa kuaminiwa na jamii kwenye kile mnachotupa na mengineyo.
 
Back
Top Bottom