Hivi kwanini vigogo wengi wa serikali wanaosema elimu ya Tanzania ni bora hawasomeshi watoto wao shule za Serikali ??

MALCOM LUMUMBA

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
20,897
63,784
Hivi kama elimu ya Tanzania ni bora kama tunavyoisifia mbona kumekuwa na wimbi kubwa la vigogo kukwepa kupeleka watoto wao shule za serikali kama ilivyokuwa miaka ya zamani ??
Je, unahisi hawa vigogo watakuwa na maamuzi ya kizalendo na shule za umma ambazo sisi watoto wa masikini tunasoma wakati watoto wao hawasomi huko ??
 
1064621

Elimu yetu ina mapingamizi mengi sana, kuna child labour kutokana na umasikini wa familia. Watoto wanapata ajira ya u house boy/girl ili kusaidia nyumbani.
Hata wazazi wakilima mazao hayana uhakika wa soko.

Drop out, uhaba wa walimu pia huchangia watoto kuacha shule. Hata watoto wakiacha shule walimu hawafahamu. Shule ya watoto 1,000 ina walimu wanne.

Private education na English medium ni za watoto wa wagiwa kura.
 
Mkuu Malcom Lumumba

Lisemwalo lipo, na kama inasemekana kuwa elimu ya Tanzania ni bora (japo ni vigogo ndo wanaongoza kusema hayo huku wananchi wa kawaida wakipinga) basi kuna hoja

Kitu pekee ninachoamini ni kuwa sio shule zote za Tanzania zinatoa elimu bora. Na katika hili kwa sasa shule karibia zote za serikali hazitoi kabisa elimu bora, zinatoa bora Elimu huku shule binafsi zikitoa elimu bora.

Upande mwingine, baadhi ya shule za watu binafsi zinajitahidi kutoa elimu bora. Ndo maana hawa vigogo kwa sababu wana uwezo wa kulipa gharama za shule binafsi wanawapeleka vijana wao huko kwenye elimu bora na watoto wa wanyonge wakibaki kwenye shule za serikali zilizochoka.

Kitu ambacho mimi najiuliza ni kuwa, Je shule za watu binafsi ndo determinant ya ubora wa elimu hapa Tanzania?
Hivi kama elimu ya Tanzania ni bora kama tunavyoisifia mbona kumekuwa na wimbi kubwa la vigogo kukwepa kupeleka watoto wao shule za serikali kama ilivyokuwa miaka ya zamani ??
Je, unahisi hawa vigogo watakuwa na maamuzi ya kizalendo na shule za umma ambazo sisi watoto wa masikini tunasoma wakati watoto wao hawasomi huko ??
 
Hivi kama elimu ya Tanzania ni bora kama tunavyoisifia mbona kumekuwa na wimbi kubwa la vigogo kukwepa kupeleka watoto wao shule za serikali kama ilivyokuwa miaka ya zamani ??
Je, unahisi hawa vigogo watakuwa na maamuzi ya kizalendo na shule za umma ambazo sisi watoto wa masikini tunasoma wakati watoto wao hawasomi huko ??
Usimuamini mwanasiasa.
 
Elimu yetu sio bora kama tunavyoaminishwa na watawala hasa upande wa serikali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Malcom Lumumba
Lisemwalo lipo, na kama inasemekana kuwa elimu ya Tanzania ni bora (japo ni vigogo ndo wanaongoza kusema hayo huku wananchi wa kawaida wakipinga) basi kuna hoja
Kitu pekee ninachoamini ni kuwa sio shule zote za Tanzania zinatoa elimu bora. Na katika hili kwa sasa shule karibia zote za serikali hazitoi kabisa elimu bora, zinatoa bora Elimu huku shule binafsi zikitoa elimu bora.
Upande mwingine, baadhi ya shule za watu binafsi zinajitahidi kutoa elimu bora. Ndo maana hawa vigogo kwa sababu wana uwezo wa kulipa gharama za shule binafsi wanawapeleka vijana wao huko kwenye elimu bora na watoto wa wanyonge wakibaki kwenye shule za serikali zilizochoka.
Kitu ambacho mimi najiuliza ni kuwa, Je shule za watu binafsi ndo determinant ya ubora wa elimu hapa Tanzania?
Mkuu elimu ya shule za Serikali kwanini siyo bora kama shule binafsi, tulikosea wapi ?? Mbona zamani haikuwa hivyo ?? Hivi unadhani wanasiasa ambao watoto wao wanasoma shule binafsi, watakuwa na maamuzi ya kizalendo na shule za serikali ??
 
Miaka ya nyuma kidogo ulikua ukienda private school unaonekana kilaza siku hizi serikalini ndio wanaonekana vilaza.

Nadhani kuna mahala serikali iliteleza katika kusimamia ubora wa shule zake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom