Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 10,883
- 2,763
Heshima Mbele
Ni muda sijaanzisha Mada hapa ila kuna jambao ambalo limekuwa likinitatiza kwa muda sasa ila naamini nyie mnaweza kuwa mnajua?
Hivi kwanini Lowassa anautaka Urais? akichaguliwa atalisaidiaje Taifa? Je, Pesa hizi anazotumia kuweka watu wake kwenye Chama tawala atazirudishaje?
Nimeanza kuogopa sana na kama watanzania wakikubali kuzugwa tena 2015 na kuchagua viongozi ambao wana mvuto wa sura, mvuto wa kutawala bila kuangalia rekodi yao ya nyuma taifa litaenda kubaya sana.
Taifa linaoelekea kupata Gesi na Mafuta linahitaji viongozi makini ambao wataweza kulivusha taifa, kutuondoa kwenye lindi la umasikini na kujenga utawala bora.
We shall cross the bridge when we get there. But how far is the bridge from here and now? How do we know there is a bridge ahead? How do we know we will get there?