Lowassa hajakurupuka kurudi CCM, namuunga mkono 100%

Lowassa hajakurupuka kurudi CCM, namuunga mkono 100%

Rose Mayemba

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2012
Posts
721
Reaction score
1,017
Na Rose Mayemba

Jana tare 1/3/2019 Waziri Mkuu wa zamani aliyejiuzuru kwasababu ya wizi wa mabilioni ya pesa kupitia shirika fake la kufua umeme(DOWANS ) Mhe Edward Lowassa alitangaza kuondoka CHADEMA na kurudi Chama cha mapinduzi ambako aliondoka mwaka 2015 baada ya kuhujumiwa kugombea nafasi ya Urais ndani ya Chama chake

Ikumbukwe kwamba Mhe Edward Lowassa ndiye mwanasiasa pekee aliyeonekana kukubalika ndani na nje ya Chama cha Mapinduzi miaka hiyo huku wajumbe wote wa mkutano Mkuu kutoka maeneo mbalimbali ya nchi wakiamini kwamba ndiye Rais watakayemsimika baada ya swahiba wake Jakaya Mrisho Kikwete kumaliza muda wake.

Sote tulishuhudia mambo yakienda kinyume pale mjini Dodoma baada ya jina la Mhe Lowassa kuenguliwa kwenye kinyang'anyiro hicho na Ndugu John Pombe Magufuli kuibuka kidedea.

CCM walimnyang'anya Mhe Lowassa haki yake ya kupigiwa kura huku watanzania wakijionea kwa macho jambo ambalo liliua ndoto yake ya muda mrefu ya kuwa Rais wa nchi hii.

Hapa ndipo ugonjwa wa hamahama ulipozaliwa, wanaccm wengi hawakuridhishwa na hujuma zile za wazi na kuamua kwenda kujiunga na vyama ambavyo vinasimamia misingi ya haki Demokrasia.

Pamoja na wanachama wengi na viongozi mbalimbali kukihama Chama hicho kwa Sababu za uonezi Mhe Edward Lowassa alihama kwasababu aliamini kwamba wananchi walikuwa na imani nae hivyo ndoto yake ya kuwa Rais ingeweza kutimia akiwa popote, hakuamini kabisa kwamba CCM inaweza kumfanya ashindwe kuwa Rais wa nchi hii. Na ukweli ni kwamba CHADEMA hawakufanya makosa kumpitisha Mhe Lowassa wa wakati ule kuwa mgombea kwasababu hakuna asiyejua kwamba yeye ndiye aliyekuwa chaguo la wananchi, Ccm wanajua na Dunia inajua, hakuna aliyekuwa na nguvu ya kumshinda Lowassa.HAKUNA.

Baada ya Mhe Edward Lowassa kupewa ridhaa ya kugombea kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) wananchi walimpokea kwa Shangwe kubwa na kumpigia kura za kutosha.Kila alipokwenda vijana kwa wazee walionesha viparata vyao vya kupigia kura kuashiria kwamba walidhamiria kuiondoa CCM madarakani. Kimsingi Mhe Lowassa alishinda uchaguzi 2015. CCM wakishirikiana na jeshi la polisi walipoka ushindi wa Mhe Lowassa, matokeo ya uchaguzi ule nakumbuka yalitangazwa kwa mtutu wa bunduki, polisi walitapakaa kila mahali kuhakikisha hakuna kiumbe kinajaribu kufanya chochote baada ya kutangazwa kwa Matokeo yale. Kimya kilitanda nchi mzima, hakuna aliyeshangilia wala kufurahia Matokeo yale na huo ndio ukawa mwisho wa Mzee wetu EDWARD LOWASSA.

Hakuwa na nguvu tena ya kufanya jambo lolote, alipokea matokeo kwa Shingo upande huku watu wengine wakimtia moyo kwamba atashinda awamu ijayo.


Ikumbukwe pia kwamba Mhe Edward Lowassa alivumilia matusi na kejeli za kila aina wakati wa kampeni zake, wengine walisema ni Mgonjwa, wengine wakasema anajinyea hovyo Kama mtoto huku wengine wakimwita marehemu. Lakini kwasababu lengo lake lilikuwa ni kutimiza ndoto yake ta kuwa Rais alipuuza na kusonga mbele. Kimsingi alidhihakiwa sana.

KWANINI NASEMA LOWASSA AMEFANYA MAAMUZI SAHIHI KURUDI CCM?

Kila nabii na zama zake. Lengo la Mhe Lowassa kuhama Chama ilikuwa ni Urais ambao wananchi walimpa na CCM wakampora. Urais huu ninaousema hapa kwasasa hauko mikononi mwa Mhe Lowassa tena, zama zake zilishapita na hana mvuto tena kama ilivyokuwa wakati wa zama zake.

Zama zako zikishapita zimepita, huwa hazirudi japokuwa Mzee wetu alitaka kulazimisha King(wacheza bao wanajua) akijiaminisha kwamba pengine nafasi yake Bado ipo.

Vijana kwa wazee kwasasa wamebadili pambio wanaimba wimbo mwingine kabisa, kwasasa mtaani kila unapopita unasikia LISSU! LISSU!LISSU hadi kero.

Hakuna namna ya kuzuia haya ili tumsaidie Mzee wetu Lowassa, walewale waliomshangilia na kumtaka sana 2015 wamebadilika wanamshangilia na kumtaka sana Tundu Lissu. Hili CHADEMA haina mamlaka nalo na wala haiwezi kuzuia kelele za watu kumtaja Lissu. Kiufupi hizi ndo zama zake,zikipita watu watakuja na maamuzi mengine tena ambayo sisi binafsi hatuyajui.

Sasa Mzee wetu Lowassa tunataka aendelee kubaki Chadema akisubiri nini?

Kwa wakati tulionao hawezi kuja kuwa Rais tena,sio kwa kubaki Chadema wala sio kwa kurudi CCM. Ndoto yake ya Urais imekwamia hapo.


Hasara alizozikimbia CHADEMA ni kwamba utawala tulionao unawanyanyasa sana wapinzani naye hakuzoea mambo hayo. haoni sababu ya kuendelea kupambana na CCM wakati ndoto yake ya Urais imekufa. Lowassa hakuwahi kuwa na tatizo na CCM yeye shida yake kubwa ilikuwa ni Urais

Haoni faida ya kufilisiwa mali zake na kuweka rehani maisha yake wakati hakuna manufaa tena, kuwa mpinzani inahitaji kujitoa mhanga. Mhe Freeman Mbowe anajeruhiwa kila siku na Serikali ya CCM na hajabadili msimamo kwasababu ndio maisha aliyochagua tangu ameamua kuwa mwanasiasa sio Lowassa. Lowassa alitaka Urais tu na sisi tulimpa kwasababu wananchi walimtaka lakini si mwanaharakati huyu, hawezi kustahimili.


Tumuache Mzee wetu apumzike, amepigania ndoto yake imeshindikana sasa ni wakati wa yeye kupumzika na kuendelea kula mema ya nchi.

Sisi tunasonga mbele, vita hii tutashinda, usiniulize tutashinda lini wewe pambana ukiamini siku na saa isiyo na jina mnara wa Babeli utaangushwa tu.

KIZA NI KINENE KWASABABU ASUBUHI IMEKARIBIA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi Magu angeamua kukomaa nayo jamaa akaonekana ana hatia si ange fia jera ka doto akitoka yy
 
Umeandika vizuri sana. Sasa tumejua kwa nini kuna hasira sana dhidi ya chadema na CUF. kumbe ndio waliofanya mkuu ashindwe ila akatawazwa na Mzee Lubuva. Baada ya hapo akaona Mbowe akidhoofishwa sana na CUF kuuawa ndoto yake itakuwa safi 2020. Haya tusubiri ya Mkuu na Lissu!!!! 🙂 🙂!!
 
Umesema kweli.....ila tufikie hatua tujue kwamba Chama ni itikadi sera na philosophy, (Imani) hao wazee wangekua mfano wakupigania wanacho amini ili vijana wapate kujifuza.........zaidi ya hilo tutashidwa kujenga strong instutional of multpartism democracy, Lowassa is right for selfish interest but bad example for future generation, pamoja na mapungufu yake vijana wengi walikua wanamheshimu sana na kumpenda.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ninakubaliana wewe kwa 100%ukweli ni kwamba Mzee Lowasa alipotea njia kwenda upinzani yeye mwenyewe ninaamini alikuwa anajua hawezi kuwa rais kwenye hii nchi hata kama angepingiwa kura na wananchi wote kwenye hili taifa kura huwa aziamui ni nani atawale hili taifa na yeye anajua,binafsi ninampongeza kwa kurudi ccm kwa sababu hata aliyempeleka upinzani kwa sasa anashikamana na mweshimiwa sasa yeye ataendelea kupaki chadema ili iweje sasa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakumbuka huko kenya ilipamba moto sana hii siasa ya TZ and by that time the president of Tanzania amekunya kwa stage and nobody care about, most of them still believ mtu nakunya stagin inaezekana vipi akakunye ikulu na the whole nation


Siasa ni kitu iko na nguvu na siasa sio kitu ya kuchezewa kwaivo kama umedecide amia part ingine amia kwa moyo wako wote na kama hujadecid hivyo basi achana naiyo baki kwa part yako maana kuna watu wengine pale

Siasa siasa sio kitu ya mchezo mchezo kwaivo iwapo unapenda penda yote iwapo upendi bishi achana naiyo na kama ukitia mjeuri finally utaishi kusumbukaaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakubaliana nawewe. Lowasa hakuwahi kuwa mwanamageuzi wala kuwa na msimamo unaoeleweka kiitikadi nje na ndani ya ccm. Kwake yeye mwanzo na mwisho wa harakati za kisiasa ni kwa yeye kuwa raisi wa tz.
Nchi yetu inahitaji "transformational and visionary" leadership. Kiongozi atayejenga miundo mbinu ya utawala bora, demokrasia na maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Twahitaji kiongozi atakayetupatia katiba bora yenye kuimarisha uhuru wa mahakama, bunge, tume ya uchaguzi na taasisi zote muhimu za utawala wa nchi yetu bila kusahau haki za binadamu.
Siamini kama ujio wa Lowasa Chadema ulikuwa na nia ya mageuzi ya dhati kwa nchi yetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijui utasemaje kama membe atahamia huko na kupewa hiyo nafasi 2020,sijui watu watasemaje hapa
 
Back
Top Bottom