Inatisha inaonekana anataka kwanza kulipiza kisasi na rafiki yake waliyeunda mtandao wa kumuingiza madarakani.
Haileti maana kusema kuwa alibadilisha maamuzi ya baraza la mawaziri kwa kupendekeza kupewa tenda ya utata Richmond. Atafanyaje bila ya ruhusa ya mwenyekiti wa baraza la mawaziri?
Na mrichmond mwenyewe ni swahiba mkubwa wa mzee wa ikulu,angalia hadi leo mapendekezo ya Bunge hayajatelekezwa na hayatatelekezwa na hawa viongozi wa hili bunge na serikali hii.
Kuhusu gesi watu walioweka mabilioni Uswisi zinahisiwa ni mikataba na makampuni ya kutafuta gesi,labda anataka kuja kulinda, othrewise haileti maana kutumia hela zote kwa kuutaka urais.
Hii ni matusi kwawatanzania kuona kwamba tunaweza kuja nunuliwa kama njugu ili mtu mwenye sifa za ufisadi aingie tena madarakani ili kwanza aje arudishe pesa zake alizotumia. Inawezekana kwenye chama chao kwa sababu rushwa na fedha ni kigezo cha kwanza, inatia aibu wasomi maintellectual ambao wangeweza kuwasaidia wananchi wanakimbilia kuingia kwenye chama hiki ili wapate madaraka watuibie.
Utawala bora my god, hakuna takukuru, Hosea aliitakasa Richmond hajawajibishwa na bado yupo akishuhudia rushwa kwenye chaguzi zao,hakuna ikulu na usalama wa taifa muulize Mwamboka, hakuna polisi kumbuka Iringa kijiji cha nyololo mpaka leo RPC yuko madarakani.
Bunge wasikilize spika na wenyeviti, mahakama naogopa wazee wa jumuia hadi leo hawajalipwa wanazungushwa, Idd Amin aliwalipa lakini nchi ya amani yenye viongozi wanaotarajiwa kupewa utakatatifu maji ya kuwashwa.
Kumbuka mahakama ya rufaa kesi ya katiba utafikiri kikao cha kamati kuu ya NEC ya CCM