Mbona una hoja za kitoto? Nani ka kwambia kuwa kutowai kuwa mwanachama wa chama kingine ni kigezo cha kutokuwa msaliti?
Haya unayo yaongea hata ndugu yako
Zitto alikuwa akiyasema kuwa yeye hakuwai kuwa mwanachama wa chama chochote zaidi ya chadema, lakini matendo yake yana mkamata! Hivi umeshawai kujiuliza kwa nini aliomba msamaha? Ndugu yako si wa kuaminika ni kigeugeu kabisa!
Alisema atakuwa wa mwisho kuwa msaliti lakini matendo na tuhuma zimemkamata!
Mwisho wa siku akawaomba msamaha hewa bila kujua mnamsamehe nini! Ulishawai kujiuliza?
Hatuna tatizo na yeye kugombea urais lakini amajitengenezea mazingira safi ya kuto aminika!
Zitto alisema walio zaliwa kabla ya uhuru muda wao umekwisha ni wakati wa vijana kuongoza taifa! Aka sahau amefanya ubaguzi tena kwa kutumia jina 'vibabu'.
Ukaletwa mjadala hapa kuhusu urais akageuka na kusema kuwa kila mtanzania ana haki ya kuchagua au kuchaguliwa na akaongeza kwa kusema ni ubaguzi kwa kuchagua urais kwa kigezo cha ujana!
Hivi mtu anaye kula matapishi yake kila leo ni mtu wa kuaminika?
Zitto hafai kuwa hata waziri mkuu kwani ameshindwa kutatua matatizo ambayo ameyaona kwenye chama chake mwisho wa siku amebaki kulalamika tuu utafikiri si muhusika kwenye chama!
Jana ililetwa makala yake hapa kuhusu chama na kukisifia chama lakini akaongelea migogoro na makundi na akabaki kulalamika na kushindwa kutuonesha mchango wake katika kutatua tatizo wakati anashiriki vikao vya chama!
Kwa nini tutafute rais wa kusema pembeni na kulalamika kwa wananchi badala ya kutatua matatizo yanayo tukabili? Kwa nini tutafute huruma za watu ili tuonekane si chanzo cha matatizo? Kwa nini tupende kutupia watu lawama tena kwa mafumbo wakati tuna nafasi ya kusema?
Hafai urais kabisaaaaaaa
............:......................................
hv kati ya zitto na huyo mnaemtaka nani wa kutilia shaka?maana zitto hajawahi kuwa na chama zaidi ya cdm lakini huyo mwingne ana uwanachama wa vyama 2