Mtoto wa Shule
JF-Expert Member
- Nov 16, 2014
- 11,657
- 8,592
Salary Slip kuna mambo ambayo huyajui. Uwe unaulizaGA!Tangu serikali itangaze kuhamia Dodoma na baadae kuwagawaia bure viwanja mabozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini,kuna nchi hata moja imeonyesha ni ya kujenga ubalozi kue mkoani Dodoma?
Ni kweli kila nchi ina taratibu zake za kutekeleza jambo kama hili, ila kwa muda wote huu, nilitarajia kusikia kuna nchi wala mbili au tatu zimeanza kuonyesha dalili za kujenga ubalozi mkoani Dodoma ila pale katika Mji wa Serikali sioni dalili ya ubalozi unaojengwa.
Kwa ukimya huu,inawezekana hizi nchi haziko tayari kuhamia Dodoma ikiwemo hata kufungua ubalozi ndogo kama walivyofanya China na Ujerumani.
Baada ya Mheshimiwa kutangaza kuhamia rasimi Dodoma,labda tutaona mabadiliko/jitihada za balozi hizi nazp kuhamia Dodoma.
Serikali inatakiwa kufanya mengi ya kushawishi nchi hizi kujenga balozi zao ikiwemo kujenga na kuboresha miundombinu katika eneo husika pamoja na huduma nyingine za kijamii kama vile mahospitali ya kisasa,iweke mazingira ya kushawishi na kuvutia watu kujenga shule za kimataifa,n.k vinginevyo itachukua zaidi ya miaka 10 hili jambo kutimia.
Kama kuna kitu nyumbus hawataki kusikia ni jina la KIGOGO2014!Kigogo 2014 anaemaje kwani