Hivi kuna ubalozi hata mmoja umeanza kujenga ofisi za ubalozi Dodoma?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,011
144,371
Tangu serikali itangaze kuhamia Dodoma na baadae kuwagawaia bure viwanja mabozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini,kuna nchi hata moja imeonyesha ni ya kujenga ubalozi kue mkoani Dodoma?

Ni kweli kila nchi ina taratibu zake za kutekeleza jambo kama hili, ila kwa muda wote huu, nilitarajia kusikia kuna nchi wala mbili au tatu zimeanza kuonyesha dalili za kujenga ubalozi mkoani Dodoma ila pale katika Mji wa Serikali sioni dalili ya ubalozi unaojengwa.

Kwa ukimya huu,inawezekana hizi nchi haziko tayari kuhamia Dodoma ikiwemo hata kufungua ubalozi ndogo kama walivyofanya China na Ujerumani.

Baada ya Mheshimiwa kutangaza kuhamia rasimi Dodoma,labda tutaona mabadiliko/jitihada za balozi hizi nazp kuhamia Dodoma.

Serikali inatakiwa kufanya mengi ya kushawishi nchi hizi kujenga balozi zao ikiwemo kujenga na kuboresha miundombinu katika eneo husika pamoja na huduma nyingine za kijamii kama vile mahospitali ya kisasa,iweke mazingira ya kushawishi na kuvutia watu kujenga shule za kimataifa,n.k vinginevyo itachukua zaidi ya miaka 10 hili jambo kutimia.
 
Niko kwenye Shabiby naenda huko, nitafanya ukaguzi wa kina! Nitakua Itigi pale but nitarudi Dodoma
 
Usiwe na haraka. Hata wizara za serikali bado hazikalamilisha ujenzi wa majengo yao pale mji wa serikali. Miundombinu hususani za lami bado pia hazijakamilika. Haya si masuala ya kukamilika ndani ya muda mfupi, tuwe na subira. Ni suala la muda tu balozi nyingi zitafungua makao yake makuu Dodoma. Kumbuka kwa sasa Dom hata international airport bado haina.
 
Tunaanza UUUPYAAAAA.....

Ha ha hahaa....

Baada ya fununuu...
 
Tangu serikali itangaze kuhamia Dodoma na baadae kuwagawaia bure viwanja mabozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini,kuna nchi hata moja imeonyesha ni ya kujenga ubalozi kue mkoani Dodoma?

Ni kweli kila nchi ina taratibu zake za kutekeleza jambo kama hili, ila kwa muda wote huu, nilitarajia kusikia kuna nchi wala mbili au tatu zimeanza kuonyesha dalili za kujenga ubalozi mkoani Dodoma ila pale katika Mji wa Serikali sioni dalili ya ubalozi unaojengwa.

Kwa ukimya huu,inawezekana hizi nchi haziko tayari kuhamia Dodoma ikiwemo hata kufungua ubalozi ndogo kama walivyofanya China na Ujerumani.

Baada ya Mheshimiwa kutangaza kuhamia rasimi Dodoma,labda tutaona mabadiliko/jitihada za balozi hizi nazp kuhamia Dodoma.

Serikali inatakiwa kufanya mengi ya kushawishi nchi hizi kujenga balozi zao ikiwemo kujenga na kuboresha miundombinu katika eneo husika pamoja na huduma nyingine za kijamii kama vile mahospitali ya kisasa,iweke mazingira ya kushawishi na kuvutia watu kujenga shule za kimataifa,n.k vinginevyo itachukua zaidi ya miaka 10 hili jambo kutimia.
Kigogo 2014 anaemaje kwani
 
Back
Top Bottom