Hivi kuna ubalozi hata mmoja umeanza kujenga ofisi za ubalozi Dodoma?

Uamuzi wa kuufanya Dodoma kuwa mji mkuu siamini kama ulikuwa sahihi:

1) Dodoma ni kama jangwa. Kiasili, Dodoma hauna mandhari nzuri kuanzia hali ya hewa mpaka uoto wa asili, n.k.

2) Dodoma ipo ndani kabisa ya rift valley, jambo linaloufanya kuwa mji wa hatari kuishi maana ni eneo ambalo lina uwezekano mkubwa siku moja kukumbwa na tetemeko la ardhi

3) Miji mingi mikubwa Duniani ni ile yenye shughuli nyingi za kiuchumi ambazo huchangiwa na uwingi wa watu, urahisi wa usafirishaji wa mali za viwandani na mali ghafi katika kuingiza na kutoa. Sifa hizo Dodoma haina.

4) Miji mikuu mingi Duniani ilipewa tu hadhi lakini ilikuwa tayari imejengeka. Haikujengwa ili iwe miji mikuu. Dodoma haikujengeka wakati inaamliwa kuwa mji mkuu. Matokeo yake ni serikali kulazimika kuujenga.

5) Mpangilio wa mji wa Dodoma kama mji mkuu ni ovyo sana. Dar es Salaam iliyopangwa na Wajerumani miaka ya 1800 ina mpangilio mzuri kuliko Dodoma iliyopangwa na waswahili wa miaka ya 1970! Wazungu wa miaka ya 1800 walikuwa na akili na uwezo wa kupanga miji kuliko wanaotajwa wataalam waswahili wa miaka ya 2000. Kati ya kada ambazo nadhani ni hovyo kabisa na isiyo na ufanisi ni Town planners. Hawa naamini ni Town Polluters. Dodoma haina barabara hata moja katikati ya mji ambayo ni pana.

Kwa Dar, walikopanga wataalam wa mipango miji wazalendo, wote mnajua.
 
Dodoma haina mvuto,ilitakiwa tu kujenga mji mdogo wa shughuli za Bunge.
Hadi leo hawajui wanataka Didoma iwe nini?
Ila wakiweza kuweka miundo mbinu ya kisasa kuunganisha Dodoma na mikoa mingine barabara ,reli,na anga harafu wakaweza kutatua swala la maji,wakapanda miti yenye kivuli kwa wingi yenye uwezo wa kukinga vumbi.Labda baada ya miaka 20 kutokea sasa inaweza ikapata hadhi ya kuitwa mji mkuu.Lakini akija Raisi mwenye msimamo tofauti,Dodoma itabakia center ya shughuli za madini tu kama ilivyokuwa huko nyuma.

Hata ipite Miaka 100 bado sikubaliana Mkoa wa Dodoma kuwa Mji Mkuu wa Tanzania, ila Mji Mkuu uwe ni Mkoa wa Dar es Salaam tu.
 
Sio rahisi miundombinu ya mji mkuu kukamilishwa ndani ya miaka minne hata hivyo Magu anatakiwa kabla hajatoka madarakani ndani ya miaka mitano ijayo ahakikishe bwawa kubwa la maji wamelijenga,ring road ikamilike,airport iwe tayari,uwanja wa mpira uwe tayari na taasisi zote ziwe zimehamia Dodoma akiwemo yeye
Pili wajenge hospitali kubwa nyingine ya rufaa yenye hadhi ya Muhimili na ambayo itakuwa na presidential suite bila kusahau watu wa mazingira kutengeneza public gardens za kutosha na upandaji miti usisitizwe.Mwisho barabara ya Dodoma Morogoro Dar iwe dual carriage na sgr ifike Fasta hapo hakuna jinsi mabalozi watahamia tuu,private sector wao wawezeshwe tu kuweka uwekezaji unaowahusu hasa mahoteli lakini pia sio vibaya serikali ikajenga hotel japo mbili za nyota tano
 
Rais akihama nao wataanza kuhamia na hasa uwanja wa ndege mpya ukikamilika na hudymu zote nuhimu zikiwa tayari. Huko Israel mabalozi wahamia Jerusalem sasa kutoka Tel Aviv kuifuata serikali.
Unaifahamu Jerusalem au unaisikia tu. Usifananishe vitu viwili vilivyo tofauti kabisa.

Jerusalem ni mji mkubwa kuliko Tel Aviv. Wayahudi wamehamisha makao makuu ya nchi kutoka mji mkubwa wa pili kwenda mji wa kwanza kwa ukubwa. Sisi tulitoa makao makuu kutoka mji mkubwa wa kwanza kupeleka mji wa 9 kwa ukubwa.
 
Uamuzi wa kuufanya Dodoma kuwa mji mkuu siamini kama ulikuwa sahihi:

1) Dodoma ni kama jangwa. Kiasili, Dodoma hauna mandhari nzuri kuanzia hali ya hewa mpaka uoto wa asili, n.k.

2) Dodoma ipo ndani kabisa ya rift valley, jambo linaloufanya kuwa mji wa hatari kuishi maana ni eneo ambalo lina uwezekano mkubwa siku moja kukumbwa na tetemeko la ardhi

3) Miji mingi mikubwa Duniani ni ile yenye shughuli nyingi za kiuchumi ambazo huchangiwa na uwingi wa watu, urahisi wa usafirishaji wa mali za viwandani na mali ghafi katika kuingiza na kutoa. Sifa hizo Dodoma haina.

4) Miji mikuu mingi Duniani ilipewa tu hadhi lakini ilikuwa tayari imejengeka. Haikujengwa ili iwe miji mikuu. Dodoma haikujengeka wakati inaamliwa kuwa mji mkuu. Matokeo yake ni serikali kulazimika kuujenga.

5) Mpangilio wa mji wa Dodoma kama mji mkuu ni ovyo sana. Dar es Salaam iliyopangwa na Wajerumani miaka ya 1800 ina mpangilio mzuri kuliko Dodoma iliyopangwa na waswahili wa miaka ya 1970! Wazungu wa miaka ya 1800 walikuwa na akili na uwezo wa kupanga miji kuliko wanaotajwa wataalam waswahili wa miaka ya 2000. Kati ya kada ambazo nadhani ni hovyo kabisa na isiyo na ufanisi ni Town planners. Hawa naamini ni Town Polluters. Dodoma haina barabara hata moja katikati ya mji ambayo ni pana.

Kwa Dar, walikopanga wataalam wa mipango miji wazalendo, wote mnajua.
Asante,umemaliza kila kitu,
 
Hata ipite Miaka 100 bado sikubaliana Mkoa wa Dodoma kuwa Mji Mkuu wa Tanzania, ila Mji Mkuu uwe ni Mkoa wa Dar es Salaam tu.
Mkuu wanapoteza pesa za walipa kodi,Dodoma ni Idodomya.Hata physical geography yake ina utata,sababu za kuhamisha Capital kuja Dodoma kwa sasa hazipo.Mimi nilikuwepo tukahamisha hadi wizara ya Waziri Mkuu Mzee Rashid Mfaume Kawawa tena ilikuwa bidii na pilika kubwa na nia haswa.
Lakini ghafla vuuu Mwalimu Nyerere akabadirisha kibao baada ya kupewa darasa na wabobezi wa mambo.Hivi Mwalimu hakuacha Diary?Zitafute Diary zake tunaweza kupata jibu.
 
Rais Dkt. Magufuli achana na Dodoma ruhusu Mji Mkuu wa Tanzania uwe ni huu wa Dar es Salaam na ubakie hivyo Milele.
 
Huo uthubutu anautoa wapi ? Mnataka awape sababu ya ninyi kuongea ? Yaani aagize Dodoma kuwa mji mkuu zimeshatumika fedha kibao kwa ajili ya kuhamishia nguvu huko Dodoma, leo hii aje kusema walikurupuka hivyo wanarudi Dar. Simuoni huyu jamaa akifanya hivyo maana ataonekana hana msimamo na hatambui anachokifanya. Labda aje kiongozi mwingine na kuyatekeleza hayo.
 
Na Wewe unaafiki kabisa tena kwa 100% Mji Mkuu wa Tanzania kuwa ni Dodoma? Nasubiri jibu lako upesi tafadhali Mkuu.
 
Kwa upande wangu naafiki Mbeya ndio iwe mji mkuu wa Tanzania. Ili mkoa wetu nasi upate maendeleo kwa mwendo wa kasi.
 
Rais Dkt. Magufuli achana na Dodoma ruhusu Mji Mkuu wa Tanzania uwe ni huu wa Dar es Salaam na ubakie hivyo Milele.
Mjadala wa kina ulipuuziwa imekula kwetu,hizo short cut za kuuza heading bila kuangalia contents ni shida Mkuu.
 
Wengi wataweka ofisi ndogo za kibalozi
Rais akihama nao wataanza kuhamia na hasa uwanja wa ndege mpya ukikamilika na huduma zote nuhimu zikiwa tayari. Huko Israel mabalozi wanahamia Jerusalem sasa kutoka Tel Aviv kuifuata serikali.
Unaifahamu Jerusalem au unaisikia tu. Usifananishe vitu viwili vilivyo tofauti kabisa.

Jerusalem ni mji mkubwa kuliko Tel Aviv. Wayahudi wamehamisha makao makuu ya nchi kutoka mji mkubwa wa pili kwenda mji wa kwanza kwa ukubwa. Sisi tulitoa makao makuu kutoka mji mkubwa wa kwanza kupeleka mji wa 9 kwa ukubwa.
Lkn una sifa zote na uko katikati ya nchi hauna foleni ya magari, umepimwa vizuri haunuki kama Dar yenu. Wewe Kama hutaki kaa na hiyo harufu mbaya.
 
Back
Top Bottom