Hivi kuna mtumishi wa umma anawaza kuipigia kura CCM!?

Tuseme tu ule ukweli tuache unafki na hata wanaotetea wengi wanaongea kinyume au inakuwa haiwahusu hii mada, awamu hii imekuwa mwiba kwa watumishi mshahara hujapanda wakati mkataba wa kazi unaonyesha kuwa kila mwaka wa fedha daraja lipande na mshahara uongezeke
 
Kwenye serikali hii watumishi wa umma wanapitia kipindi kigumu sana kuwahi kutokea tangu nchi yetu ipate uhuru. Wanapelekwapelekwa tu, hakuna kupanda cheo, mshahara,posho kutishwa na kukashfiwa kila siku.
Mwanafalsafa, kada hiyo unayoishangaa wala usiifikirie ndugu yangu.

Hao wameshakuwa ma-zombie (hawajielewi). Watapiga tena kwa vigelegele vyote.

Watasahau wanavyotutesa kutukopa huku mitaani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mi nadhani watakuwepo tu ingawa sina hakika , tena watakuwa wengi kama wakifanyiwa yafuatayo

wakipandishwa vyeo mwaka 2019,

wakipewa kazi ya andikisha wapiga kura katika kuhakiki taarifa za daftari la kura .
wakisifiwa na kuahdiwa neema katika awamu ijayo,
wakipewa nusu ya malimbikizo ifikapo 2019 na kuahidiwa mengine uhakiki unaendelea hivyo wavumilie kidogo.
kura zitakuwa za kumwagaaaaaa
 
Hawapigiwagi kura hawa licha ya wafanya kazi,hata na wanakijiji hakuna anayewapenda.wanaiba,wakisaidiwa na tume isiyo huru,na kutumia polisi kuua na kutishia wananchi,nakukataza hata kulinda kura mita 200,ili waingize kura feki na kujitangazia ushindi.Tangu agombee liatonga mrema bin msaliti akashinda na wakampora,ccm haijawahi shinda tena.na haitatokea ishinde kihalali mpaka mwisho wa dunia.nikwakumwaga damu,kuweka watu rumande,kuiba kura na kusaidiwa na tume,na kurudia chaguzi tu kama Zanzibar, hilo ndilo tegemeo lao.Mungu hatuhitaji tena kuwafikiria hawa watesi na adui zetu,tunapashwa tu kukushukuru kwa wanavyo dhalilika kimataifa.nasema tena Asante sana kwakua nilikuomba waumbuke mpaka nje ya mipaka na umetenda.usiwasazie ficho tena tangu waumbuke canada,naiwe hivyo kwao siku zote mpaka warudishe kura za Lowasa,Amen.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
. Kwanza rekebisha hapo 'tangu nchi ipate uhuru' mishahara ya watumishi imeimarishwa vyema juzi tu 2012 hebu tizama mishahara ya 2009 kurudi nyuma ilikuwa ni midogo kupita kiasi.

Mfano mwalimu wa diploma mshahara aloanzia kazi 2012 mwaka huu 2017 umeongezeka 205,000/

Binafsi namkubali Magufuli mambo mengi japo ntaacha kazi soon maslahi serikalini madogo nifanye mambo yangu.
 
Watumishi ni watu wa kusahau,Leo wanalizwa na CCM,uchaguzi ukikaribia wakitupiwa fupa wataichagua CCM na kusahau yote waliyofanyiwa na CCM utafikiri siyo wake waliokuwa wanailaani CCM Jana, na haohao ndio masteringi wa kuiba kura kuisaidia CCM ishinde.
 
Back
Top Bottom