Hivi kuna chama ambacho kinaweza kuitoa CCM madarakani?

King Jody

JF-Expert Member
Oct 8, 2022
914
1,704
Huwa najiuliza ni chama ganii chenye uwezo wa kuitoa CCM madarakani, kwa sababu CCM ni kama Mandonga Ukimshinda ni kama amekushinda, na akishinda ameshinda.

Namuomba Mungu anijalie afya njema ili siku moja niweze kushuhudia kwa macho yangu CCM ikipigwa knockout na chama chochote cha upinzani.
 
Hakuna chama kinachoweza toa CCM madarakani! CCM ina resources zote. CCM ina resource ya waalimu wote Tz ni CCM, jeshi lote ni CCM. Sasa unaona mtu huyu kwa kura ya tiki huwezi kumtoa maana hata hizi resources nilizotaja ni ⅒.

Chama kama hichi kuondoka katika madaraka huwaga ni accident, huwa inatokea ni saa ambayo mama kajikwaa mbele ya mpizani na mpizani kumpika teke litakalofanya andondoke mazima, hapo ndio ushindi
 
Sio kweli mkuu
 
Ndio Kinaitwa UMMA.. Hawa ndio wanaweza Kuamua Nani awepo madarakani na Nani Asiwepo kwa Njia Yeyote ile..

Usitegemee Kikundi cha Watu wachache Wenye Njaa wataweza Kukiondoa , Maana Wakihongwa Hela Tu wanasaliti UMMA
 
Huwa najiuliza ni chama ganii chenye uwezo wa kuitoa CCM madarakani, kwa sababu CCM ni kama Mandonga Ukimshinda ni kama amekushinda, na akishinda ameshinda.

Namuomba Mungu anijalie afya njema ili siku moja niweze kushuhudia kwa macho yangu CCM ikipigwa knockout na chama chochote cha upinzani.
Wewe ombea kwanza tupate chama cha upinzani ndo ufikirie kama kinaweza kuitoa CCM.
 
Huwa najiuliza ni chama ganii chenye uwezo wa kuitoa CCM madarakani, kwa sababu CCM ni kama Mandonga Ukimshinda ni kama amekushinda, na akishinda ameshinda.

Namuomba Mungu anijalie afya njema ili siku moja niweze kushuhudia kwa macho yangu CCM ikipigwa knockout na chama chochote cha upinzani.
hata watoa taarifa wote wakiungana hawatafua dafu.
Yaani miongoni mwa mambo ambayo hayawezekani duniani basi ni pamoja na hiki....
 
Shida kubwa ni vyama vya upinzani vipo kwa maslahi yao binafsi sio ya nchi. Ila tungekuwa na vyama makini vyenye watu makini CCM angetolewa madarakani kitambo sana.

Ili kumtoa CCM ni lazima upinzani waanze kwa kuchukua viti vingi bungeni , kwa kilichopo sahivi wanakazi sana kurudi kwenye level waliokuwa nayo 2015 na nyuma.

Mwisho, kwa katiba iliyopo sahivi hata ipite miaka 1000 CCM hawezi toka madalakani, vyama vianze kudai katiba mpya kabla ya chochote kile .....
 
Kifo Cha CCM kitakuwa ghafula,

Na kifo hicho kitatokana na Ajali.

Tutarudi 2026 kusoma Uzi huu!!
 
Nilishahisi, kamwe CCM haiwezi kuachia madaraka kirahisi rahisi hata kama huko mbeleni ipo siku chama cha upinzani kitashinda.

Hatua ya kwanza CCM itang'ang'ania ushindi hata kama kimeshindwa, mwisho wa siku watakaa mezani na kuunda serikali ya umoja wa kitaifa.
 
Back
Top Bottom