CCM ni kubwa na ina Mizizi mirefu kama Chama Cha Kikomunisti cha China, itadumu sana Madarakani

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,035
142,149
Kiukweli nimeamini CCM ni Chama kikubwa tena chenye mipango mikubwa sana sioni Chama cha Upinzani cha kuiangusha CCM kwa miaka 50 ijayo

Hapa nafuatilia Mkutano mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha China hawa jamaa ni CCM kabisa yaani wamefanana kweli kweli

Nawatakia Dominica njema!
 
Ccm inaweza kutolewa madarakani lakin ni lazima tukubali kwanza kuunda chama kipya tofaut na chadema chadema pale juu wamejaa ma puppet kwaajili ya kuilinda CCM na kuendelea kuwaweka wa Tz kwenye usingizi mzito wasifikirie nje ya box na kuendelea kuitegemea chadema, hao ma puppet wa chadema kazi yao kubwa ni kucheza Sinema za kuamsha hisia ila zisizo na madhara
 
Kiukweli nimeamini CCM ni Chama kikubwa tena chenye mipango mikubwa sana sioni Chama cha Upinzani cha kuiangusha CCM kwa miaka 50 ijayo

Hapa nafuatilia Mkutano mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha China hawa jamaa ni CCM kabisa yaani wamefanana kweli kweli

Nawatakia Dominica njema!
Uko sahihi kabisa. Huku ikiendelea kutuletea Umaskini na Ujinga kama lote.
 
Hao unaowafananisha na chama cha china ndo majambaz makubwa ya taifa hli ajabu hawapewi adhabu za kunyongwa kama ilivyo kwa sheria za china ila wanapandshwa vyeo tu.
 
CCM itadumu madarakani kama itakuwa imejifunza kutomkabidhi tena nchi kwa kichaa na mshamba
 
kuna utani kuwa wakenya waliwahi kuuliza nini maana ya neno Kingunge. Yaani waliposikia Kingunge Ngombare Mwiru wakadhani Kingunge ni cheo au sifa fulani kubwa kwa mtu maarufu, Walianza kufikiria kuwa na Kingunge Kenyata, Kingunge Odinga, Kingunge Ruto, Kingunge Kibaki! nk.
Leo hii si ajabu wakaanza kufiria kuwa kila kiwanja kuanza na neno ccm kuwa ni sifa kubwa ya uwanja. Tuna sisiem Kirumba, sisiem Jamhuri, nk na baadae tunaweza kuwa na sisiem Bashungwa, sisiem Mkapa, sisiem shamba la bibi, sisiem Karume, sisiem Kaitaba, nk Kwa hiyo nao watakuwa na sisiem Kasarani.... nk.
Labda huo ndio ukubwa unaouzungumzia.
 
Kiukweli nimeamini CCM ni Chama kikubwa tena chenye mipango mikubwa sana sioni Chama cha Upinzani cha kuiangusha CCM kwa miaka 50 ijayo

Hapa nafuatilia Mkutano mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha China hawa jamaa ni CCM kabisa yaani wamefanana kweli kweli

Nawatakia Dominica njema!
CCM haina mzizi wowote, ni mfano tu wa dubwashika fulani linaloelea kwenye dimbwi la maji. Maisha likitegemea nguvu ya kamba iliyoahikiliwa na vyombo vya dola ili lisiweze kuzama ama kupotezwa kabisa na nguvu ya upepo na dhoruba nyingine.

Na vyombo hivi vya dola vinahamasika na kushinikizwa kulishikilia dubwana hili, kwa kuwa ndani ya uongozi wake kumejaa makada wake ambao wamejivika vyeo vya kijeshi na kiusalama, ili waweze kulinda maslahi na uhai wake.
 
Kikomunisti ndio nini? Kuwa hawana Kikomo au madudu gani?

Hii ni lugha moja yapo inayotumiwa na wenye Wivu na Nchi zingine, wenye wivu wa Madaraka, wenye wivu wakuona Jinsi Nchi nyingine zinavyopeta(power)

Sikubaliani na utumiaje wake pamoja na kuwa CCM imeniangusha. Inatuangusha Wananchi.

Amani ikufikie...naelewa fika ulipo.
 
Back
Top Bottom