Kijakazi
JF-Expert Member
- Jun 26, 2007
- 6,410
- 8,911
Napenda kujua kwa anayefahamu, hivi Nchi za Kiafrika kama Kenya, Uganda, Zambia, Nigeria, Ghana Malawi n.k zinastahili kuitwa kwamba ni nchi zinazoongea Kiingereza (English Speaking Countries)?
Yaani ninachomaanisha ni kama vile kwa mfano Mtu akisema Nchi ya Australia ni English Speaking Country au Marekani ni English Speaking Country, sasa Je hawa wenzetu (Kenya, Uganda &Co.) na wao wamo kwenye hilo kundi?
Nauliza hivyo kwa maana nimesikia kwamba hawa jamaa kama Kenya na wenzake kwa mfano wakitaka kwenda kusoma Marekani ni lazima wafanye mtihani unaoitwa TOEFL (Test of English as a Foreign Language) au Mtihani wa kupima uwezo wa kuongea na kuandika kwa kutumia Lugha ya Kiingereza, lakini Raia wa Australia au Canada au sijui New Zealand hana haja ya kufanya TOEFL...sasa ni kwa nini?