Hivi kati ya Muongo, Mnafiki na Mmbea ni rafiki yupi wa Kumuogopa Zaidi?

Error 404

JF-Expert Member
Jun 21, 2022
781
799
Habari nna rafiki zangu watatu ila nimekuja kugundua mmoja ni muongo sana ,mwingine ni mnafiki na wa mwisho ni Mmbea.

Kati ya hawa ni yupi niwe nae makini sana?
 
Habari nna rafiki zangu watatu ila nimekuja kugundua mmoja ni muongo sana ,mwingine ni mnafiki na wa mwisho ni Mmbea .

Kati ya hawa ni yupi niwe nae makini sana ?
Katika dunia kitu inaitwa rafiki delete kabisa. Kuwa na watu unaofahamiana nao ( contact people and not friends) sijawahi kuwa na rafiki na sijutii. Nina watu ninaokutana nao kazini au ktk mishemishe za kawaida tunamalizana kimtaa mtaa na tunasaidiana kimtaa mtaa basi.
 
Hakuna mtu mzuri hapo maana mnafiki anaweza kuwa muongo na mmbea anytime.
Naye muongo anaweza kuwa mnafiki na mmbea anytime
Na vile vile kwa mmbea.

Kama una marafiki wa hivyo nakushauri uachane nao Mara Moja.
Habari nna rafiki zangu watatu ila nimekuja kugundua mmoja ni muongo sana ,mwingine ni mnafiki na wa mwisho ni Mmbea.

Kati ya hawa ni yupi niwe nae makini sana?
 
Mnafiki kwasababu ndani ya mnafiki kuna uongo na umbea juu. Mtu muongo anaweza danganya kwasababu zake binafsi na sio kwaajiri ya kukudhuru mfano unalazimisha kujua maisha ya mtu anakudanganya kuwa yeye yupo vema na ana mali ila si kweli huo uongo ni kwaajiri ya kukutoa wenge usimfuatilie mambo yake, nje ya hapo ni mtu poa sana.

Mbea anapenda kushare taarifa za watu na anaweza kushare na watu sahihi taarifa zake na isiwe jambo baya. Mfano jirani ambaye anamuona house girl wako akiingiza wanaume kipindi umeenda kazini na mkeo, huku nyuma watoto wako wadogo wanashuhudia mambo ya ufuska yanayofanywa na beki 3. Hauonj umbea wake utaokoa mali zako kutokana na wizi wa kuaminiwa na kuokoa watoto wako wasiharibiwe tabia na beki tatu. So umbea una faida

Ila mnafiki sio mtu mzuri sababu analengo la kufitini kama sio kuchonganisha au kurubuni. Anajificha katika sura ambayo si yake ili akupumbaze udhurike.

Imagine una mkeo ana marafiki wanatoka nae wanasema wanakwenda kanisani au vikao vya wanawake kumbe wanamsindikiza kwa wanaume ile hali wakijua mna ndoa halali ya kuheshimishwa. Halafu wanajua mwenzao anaharibu ila wanaona wamchochee aharibu ili awe nungayembe kama wao na wewe ni mtu mzuri kwao ila wanakuzeveza uingie mkenge.
 
Back
Top Bottom