SONGOKA
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 1,843
- 1,841
Jana Mh. Rais kahudhuria mechi ya watani wa jadi, tunamshukuru sana, sababu matukio makubwa kama haya si tu ni muhimu lakini ni tija yeye kama kiongozi wa nchi kuhudhuria.
Pia aliamua kuwa neutral katika ushabiki kwa kuvaa jezi nusu Simba nusu Yanga, ingawa wambea wanasema Mh. ni Simba damu damu.
Kituko ni kuwa waliomwandalia hiyo jezi, hivi SPORPESA ni nini? Ni kweli kuwa hawakuona jezi ya Mh. inasomeka SPORPESA? Au wanamalengo yao binafsi?
Lakini pia wanajua ni makosa kufanya brand distortation? Na je, wanajua Sport Pesa wame-invest kiasi gani katika jezi hizo ili jina lao kuwa sawa?
Je, Sport Pesa wakiamua kushtaki katika mahakama za kibiashara, wanajua ukubwa wa danage yake?
Lakini kwa heshima na wadhifa wa Mh. Rais kwa nini aandaliwe jezi yenye chapa isiyoeleweka? Ni gharama kiasi gani kuchapisha jezi kama ile yenye vipimo na maandishi yaliyo sawa kulinganisha na hiki kituko walichofanya?
Ni bora kutokuvaa jezi kabisa kuliko kuvaa jezi inayoenenda kinyume na taratibu za kimichezo, lakini pia haiba kwa mvaaji.
Kwa hisani ya SPORPESA.