Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 141,793
- 284,881
Huyu Dada tangu nifahamu habari zake mara zote nimemsikia akiumwa na akiomba misaada ya matibabu.
Sina Nia mbaya na wala sina shida yoyote na kuomba kwake, Bali nauliza tu kwamba Je huyu Dada ni Yatima au ametengwa na Ndugu zake?
Mbona hata sisi tunauguliwa lakini tunajikusanya na kuchangia matibabu ya Ndugu zetu na mara kadhaa tumesafirisha ndugu kutibiwa hadi India na kwingineko, Ndugu wa huyu Wastara hawalioni hilo, mpaka ndugu yao kutwa kucha kwenye media kuomba misaada, hawaoni Aibu?
Hata kama serikali ina hela, lakini inawezekanaje msaada wake uwe kwa Wastara tu miaka yote, nani amesahau Wagonjwa waliopona lakini hawaruhusiwi kuondoka mawodini hadi ndugu zao walipe bili za matibabu, Je hao hawastahili kulipiwa na serikali?