Kuwa kada wa chama cha siasa siyo tatizo. Tatizo linakuja pale mtu anayejitambulisha kama mwanataaluma, tena wa sayansi ya siasa anapoonekana kutotambua kuwa kuna taifa kwanza kabla ya mkusanyiko huo wa watu wachache wanaojiita chama cha siasa. Bila taifa, chama cha siasa hakiwezi kuwepo. Wasomi wetu tunawatarajia katika ukada wao wajipambanue kwa hilo. Mwalimu alionya kuwa mataifa ya Kiafrika bado machanga sana na kwamba kitu kidogo tu kinaweza kuwagawa wananchi na kusambaratisha taifa. Kwamba katika michezo yetu yote ya siasa tuhakikishe taifa linabaki bila nyufa za kujitakia. Mchakato wa katiba mpya umesbabisha ufa kiasi kwamba hata viongozi wetu wa dini wameshindwa kunyamaza. Baada ya kuona hivyo busara nyingi zilihitajika ili kunusuru nchi hasa kwa vile kuna uchaguzi mkuu mbele yetu. Msomi asiyeona kwamba ipo haja ya wanasiasa wetu kuangalia upya misimo yao ili kutuepusha na na uhasama wa kisiasa, kwa hakika anayo matatizo makubwa sana. Hao ndio wasomi wanaowashauri watawala wetu? Mungu atusaidie sana.