Hivi huwa inakuwaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi huwa inakuwaje?

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Manyanza, Oct 26, 2011.

 1. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #1
  Oct 26, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  wadau huwa mimi nashindwa kuelewa utakuta mtu anaenda kutoa PESA kwenye ATM. Akishamaliza anaanza kuzihesabu. Hivi hata kama akizukuta zimepungua/ ongezeka atafanya nini wakati huo Bank inakuwa imeshafungwa.
  Na huwa inakera zaidi maeneo ya mikoani yaani umesimama kwenye foleni halafu kila anayeingia anakuwa anafanya kamchezo hako bila kuzingatia kuna foleni kubwa inasubiri huduma.
  Sijaelewa na huwa najiuliza bila majibu mtu kuanza kuhesabu pesa baada ya kutoa kwenye ATM.
  Naomba wenzangu kama mna mawazo tofauti.
   
 2. N

  Navoyne JF-Expert Member

  #2
  Oct 26, 2011
  Joined: Dec 12, 2010
  Messages: 871
  Likes Received: 193
  Trophy Points: 60
  utandawazi wito ..........wanaogopa dhuluma wengi risiti hawaifadhi.
   
 3. A

  Ave Ave Maria JF-Expert Member

  #3
  Oct 26, 2011
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 10,757
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 0
  Hivi machine inaweza kutoa pesa chini/juu ya kiasi ulichoandika? Lol.....nimeona niulize mwaya, ila mi sijawahi shuhudia!
   
 4. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #4
  Oct 26, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  huwa mimi nashangaa sana, kama mtu ume command kutoa laki moja iweje ukishatoa uanze tenaa kuzihesabu?
   
 5. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #5
  Oct 26, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kwenye ATM zetu za bongo hua inatokea watu wanapata chini ya kiasi walichotaka kitoke kutokana na makosa ya kupanga pesa. Yani kama sh. 5000 ikiwekwa kwenye tray la sh.10000 lazima kuna mtu atapunjwa mashine itakapotoa ile 5000 kama 10000....kwahiyo binafsi siwezi kulaumu mtu akihesabu vijisenti vyake just to make sure hajapigwa changa la macho. Bongo si ATM wala watu usanii kila mahali....
   
 6. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #6
  Oct 26, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Ukiingia kwenye chumba cha ATM kuna tangazo linasomeka 'HESABU FEDHA ZAKO KABLA HUJAONDOKA'. Kwahiyo waliloliweka ni wajinga?
   
 7. L

  LAT JF-Expert Member

  #7
  Oct 26, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  hivi unaweza uka justify vipi kwamba pesa yako imepungua au imeongezeka once umeshaitoa kwenye mashine na ATM receipt inaonyesha imetoa fedha taslimu

  ukikuta zimepungua utamhakikishiaje afisa wa benki kwamba pesa zimepungua kwa ATM na si janja yako

  siyo rahisi kihivyo mkuu
   
 8. Meritta

  Meritta JF-Expert Member

  #8
  Oct 26, 2011
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 1,304
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  bongo usanii hadi kwenye atm du
   
 9. chapaa

  chapaa JF-Expert Member

  #9
  Oct 26, 2011
  Joined: Feb 19, 2008
  Messages: 2,355
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  nimesha shuhudia mtu kaomba hela ikamuhesabia na pesa haikutoka ikatoa risiti kuthibitisha kwamba pesa kesha chukua,mtu atakaye fuata hapo au hata baada ya watu kazaa akapewa pesa zaidi ya ile ailiyoomba
   
 10. A

  Ave Ave Maria JF-Expert Member

  #10
  Oct 26, 2011
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 10,757
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 0
  Gosh!!! Kama benki imeshafungwa sasa hapo sijui ndo inakuwaje!!
   
 11. chapaa

  chapaa JF-Expert Member

  #11
  Oct 27, 2011
  Joined: Feb 19, 2008
  Messages: 2,355
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  ukienda siku za kazi huwa wanacheki sabab kuna taarifa huwa zina baki kama kweli hela ilitoka au la kama haikutoka baada ya 24hrs ile hela huwa inarudi kwenye akaunt automatically,kwa yule aliye chukua zaidi ya kiwango ailchokuwa anahitaji maana atm ilitoa accidentally huwa inakuwa deducted kwenye ac yake
   
 12. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #12
  Oct 27, 2011
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Watu na wahesabu coz ilishawahi kunitokea nimekomand laki ikatoka elfu 50 na risiti iasoma nimetoa laki,ilinisumbua sana kufatilia kwenye tawi nililofungulia account ndio wakanirudishia,ni vizuri kuhesabu mashine nyingi zina mawenge na zinakosea.
   
 13. harakat

  harakat JF-Expert Member

  #13
  Oct 27, 2011
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 2,908
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  utahesabia mbele ya safari kwani mara nyingi inakua too late...............
   
 14. v

  valid statement JF-Expert Member

  #14
  Oct 27, 2011
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 2,737
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  mkuu kuhesabu mbona kitu cha kawaida icho.
  Si unahakikisha tu, kwani mashine unadhani haikosei?
   
 15. feis buku

  feis buku JF-Expert Member

  #15
  Oct 27, 2011
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 2,371
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Pesa yangu jamani,kuhakiki muhimu!!
   
 16. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #16
  Oct 27, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkuu sure unachoongea kuna siku niliingia kwenye hizi Umoja Switch. badala ya 50,000 ilitoka 30,000.
  na receipt ilikuwa inaonyesha nime withdraw 50,000. nili complain mpaka kwa Meneja lakini wapi.
  na msimamo wao ulikuwa pale pale. receipt inaonyesha elfu 50 wewe unasema elfu 30, hawakunielewa nikakubali kula hasara maana ilikuwa hamna evidence yoyote.
   
 17. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #17
  Oct 27, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  hadi kwenye ATM?? au pale dirishani?
   
Loading...