Sadaka ya kweli

Sadaka ya kweli

Papillon 1906

Senior Member
Joined
Jun 19, 2025
Posts
128
Reaction score
431
Je, umewahi kujiuliza kwa nini watu wengi wanatoa sadaka kwa miaka mingi lakini maisha yao bado yamekwama kwenye umaskini, hofu, na madeni?

Wengi wanaelewa sadaka ni kama biashara ya kubadilishana na Mungu au Universe kwamba "Nitoe kiasi hiki, nipate hiki." Lakini ukweli ni kwamba Universe haifanyi kazi kwa hesabu za kiasi, bali inafanya kazi kwa Frequency na Nishati (Vibration)

*Sadaka ya Kweli ni Nini?

Sadaka si pesa tu. Ni uhamisho wa nishati kutoka kwako kwenda kwa mwingine kwa nia ya kuongeza thamani ,,inaweza ikawa:
Pesa au chakula, Maarifa, ujuzi, au muda wako, Upendo, faraja, au kumsaidia mtu kuinuka na kujitegemea

*Je, Sadaka Lazima Itolewe Sehemu Fulani?

Hapana! Universe haiangalii jina la mahali ulipopeleka sadaka (iwe kanisani, msikitini). Sadaka yenye nguvu zaidi ni ile inayoongeza uwezo wa maisha ya mtu mwingine. Kumsomesha mtoto, kununua dawa, au kusaidia mjane ni sadaka yenye nguvu kwa sababu inazalisha nishati ya ukuaji.

*Siri ya Feeling: Unatakiwa Ujisikieje Baada ya Kutoa?

Hapa ndipo kwenye siri kuu ya sadaka,,dakika tano baada ya kutoa ndizo zinazoamua hatima ya sadaka yako, ukitoa halafu ukaanza kuwaza, "Mbona nimetoa nyingi? Sasa nitakula nini?" hapo tayari umeshafuta vibration ya utoaji.
Unapotoka kutoa ukiwa na hisia ya "Nina vya kutosha, nimefurahi kuwa sehemu ya suluhisho," hapo ndipo unapotuma signal ya Uwingi (Abundance) kwa Universe.

*Je, KUJIMALIZA (Kutoa hela ya Chakula au Kodi) ni Sawa?

Sheria ya Universe haisemi "Jimalize kwanza ndipo upewe." Badala yake, inasema: "Jijaze kwanza ndipo utoe." Mtu anapotoa pesa ya kula au ya kodi kwa imani ya muujiza wa kesho, mara nyingi anakuwa anafanya hivyo akiwa amejawa na hofu, wasiwasi, na msongo wa mawazo. Katika lugha ya nishati, hapo unatoa sadaka ya hofu. Universe haisikii kiasi ulichotoa,, inasikia sauti ya ndani inayosema, "Sina," "Nimebakiza kidogo," au "Ninaogopa." Kwa kufanya hivyo, unathibitisha hali ya upungufu ndani yako, na ndiyo maana watu wengi wanaotoa kwa njia hii huishia kuzama zaidi kwenye madeni na maumivu. Sadaka ya kweli inatakiwa ikupe amani, siyo kukuacha ukiwa kwenye hatari ya maisha au njaa. Kumbuka, huwezi kumimina maji kutoka kwenye kikombe ambacho ni kitupu!

*Kutoa Ukiwa Unasubiri Malipo/kulipwa

Kuna kosa kubwa ambalo watu wengi wanalifanya,,Kutoa sadaka huku wakiwa na saa mkononi wakisubiri muda wa kulipwa uweze kuwadia. Ukitoa sadaka huku ukihoji, "Mbona siku mbili zimepita sijapata muujiza?" au "Mbona nimefanya hivi lakini bado maisha hayajabadilika?", unaonyesha kuwa utoaji wako ulikuwa ni biashara na siyo sadaka. Katika sheria za Universe, hofu na mashaka huwa zinasitisha mzunguko wa nishati. Unapokuwa na mawazo ya kuhesabu faida, unazuia wingi usije kwako kwa sababu unajionyesha kuwa huna imani na mchakato wa ulimwengu. Sadaka ya kweli ni ile inayotolewa bila masharti na bila kutegemea malipo ya haraka. Ukitoa kwa moyo mweupe, unaiachia Universe ifanye kazi yake kwa muda wake sahihi, na ndipo matokeo ya kweli yanapojitokeza.

*Je, Kutoa kwa Kujionyesha (Kujitangaza) ni Sahihi?

Katika sheria za Universe, nia yani intention ndiyo kila kitu. Ukitoa ili uonekane na watu , unatoa nishati ya kutafuta sifa badala ya nishati ya kupenda. Universe haijibu kitendo, inajibu hali ya ndani. Ukitoa kwa ajili ya sifa, utavuna sifa za muda mfupi, lakini nishati ya ndani ya umaskini au upungufu itabaki ile ile.

Sadaka siyo mchezo wa kiasi, ni mchezo wa fahamu. Kabla ya kutoa,hebu jiulize,, Natoa kwa upendo au kwa hofu ya kukosa baraka?
Utoaji wa kweli unapaswa kutoka kwenye kikombe kilichojaa, siyo kikombe kilicho tupu. Unapotoa ukiwa na hisia ya "Ninavyo vingi" unafungulia milango ya Universe kukuletea zaidi.

Mwandishi:Nguvu ya universe

sadaka_omru_uzatir_mi_sadakanin_faziletleri_nelerdir_ramazanda_sadaka_vermek_1649174220_6203.jpg
 
Back
Top Bottom