Utaratibu wa kulazimisha mtoto wa kwanza kuanza kufunga ndoa kwanza kisha ndio wafuate wadogo zake

Chief Wingia

JF-Expert Member
Jul 12, 2013
2,451
4,369
Habari zenu wana MMU nawasalimu

Nianze kwa kusema ndoa ni rizki, ndoa ni bahati, ndoa ni baraka sasa kuna mila na desturi za ndoa ambazo ni za kishamba katika jamii zetu ambazo bado tunazikumbatia bila maana yoyote.

Ipo hivi mwanzoni mwa mwaka huu kuna rafiki yangu wa karibu alidhamiria kuaga ukapela hivyo basi akajitoa kimasomaso kuchumbia binti katika familia flani na mchakato ukaanza chapchap Mungu si Athuman barua ya uchumba ikakubaliwa kisha tarehe ya kikao/siku ya kupeleka mahari ikapangwa.

Mungu ni mkubwa siku iliwadia na mara baada ya zoezi la kupokea mahari kuisha basi bana utata ukaanzia pale tulipo wapa tarehe tulio kusudia kuja kuoa ili kama kuna la kujadili tuwekane sawa kabisa maana tulihitaji kuondoka na tarehe rasmi ya siku ya ndoa.

Nakumbuka wanafamilia wa binti walianza kuongea kwa minong'ono kisha babu alianzisha hoja na malumbano ya hoja yakanzia hapo.

Upande wa binti wakadai kuwa haiwezekani mdogo mtu aolewe kabla ya dada yake eti ni dharau, aisee tulijitahidi kuwaelimisha kadri ya uwezo wetu kuwa ndoa ni rizki inayopangwa na Mungu hivyo sisi wanadam hatuwezi kuisitishaa ndoa ya binti yao mdogo eti kisa dada yake bado hajaolewa wakati dada mtu hata kuchumbiwa tu haijulikani atachumbiwa lini lakini wapi familia ya yule bint ilishikilia msimamo wake hadi ikatubidi tuondoke bila jibu la maana na kuahidi kurudi siku nyingine

Ikapita kama mwezi hivi tukaomba kikao kingine nakumbuka kwenye kikao hicho tulishirikisha na viongozi wa dini lakini wapi familia ya binti ilisimamia msimamo wake na kuweka wazi kuwa hadi mkubwa aolewe ndio mdogo nae ataolewa

Ila safari hii hatukuondoka mpaka tulipo kubaliana na tukawapa miezi 4 kama bint yao mkubwa atakua hajachumbiwa basi ndoa ya binti yao mdogo itafanyika na kama atakua amechumbiwa basi tutakuwa radhi kusubiria.

Sasa ile miezi imeshatimia na panapo majaaliwa siku ya kesho tunarudi tena huko ukweni ili kufahamu ni ipi hatma ya ndoa hii tarajiwa maana kwa taarifa tulizonazo hadi wakati huu yule binti yao mkubwa bado hajachumbiwa

Waungwana nakaribisha ushauri wenye kujenga katika hili.

Ahsanteni
 
Hiyo alishakosea tokea mwanzo. Ilitakiwa apambanie kupendwa na huyo binti mdogo. Yeye mwenyewe alifuata mila kupeleka barua kuomba uchumba. Imekula kwake. Angekuwa anapendana teari na msichana, kikwazo kisingekuwepo kwa sababu haoi familia, ila anaoa msichana.

Ila alishaanza kuhusisha familia. Sasa inakula kwake


Habari zenu wana MMU nawasalimu

Nianze kwa kusema ndoa ni rizki, ndoa ni bahati, ndoa ni baraka sasa kuna mila na desturi za ndoa ambazo ni zakishamba katika jamii zetu ambazo bado tunazikumbatia bila maana yoyote.

Ipo hivi mwanzoni mwa mwaka huu kuna rafiki yangu wa karibu alidhamiria kuaga ukapela hivyo ]
 
Hiyo alishakosea tokea mwanzo. Ilitakiwa apambanie kupendwa na huyo binti mdogo. Yeye mwenyewe alifuata mila kupeleka barua kuomba uchumba. Imekula kwake. Angekuwa anapendana teari na msichana, kikwazo kisingekuwepo kwa sababu haoi familia, ila anaoa msichana.

Ila alishaanza kuhusisha familia. Sasa inakula kwake

Hivi unadhani ni zile ndo za nmemuona nmemuona hawa wachumba wote ni watu wanao fahamiana
 
Lazima mkubwa aolewe kwanza hujui tu maana yake wazee wanajua miiko,kumbuka hata kwenye bible Raheli alipendwa Ila siku ya harusi yake akawekwa dada yake badala yake ili aolewe kwanza ndio afate, I think huu usasa tunao iga una walakini.
Umeongea point
Haiwezekani dada yako awe nyumbani eti wewe uondoke kabla yake
Huko ni kumdharirisha.
 
Lazima mkubwa aolewe kwanza hujui tu maana yake wazee wanajua miiko,kumbuka hata kwenye bible Raheli alipendwa Ila siku ya harusi yake akawekwa dada yake badala yake ili aolewe kwanza ndio afate, I think huu usasa tunao iga una walakini.
Miiko ndo nn sasa ushenzi mtupu , hayana maana yeyote , wangekutana na mm nahisi hata hiyo ndoa ningeghairi kabisa , kwan inaonekana hao watakua na mambo ya kiswahili ambayo yanaweza yakawa hata na athari kwenye familia yangu na kizazi changu , upuuzi tu
 
Back
Top Bottom