Nizalie kwanza kisha nitakuoa

jastertz

JF-Expert Member
Jul 4, 2020
392
743
Siku hizi kumekuwa na wimbi kubwa la singo mama, wanawake ambao wapenzi wao wamewazalisha kisha wamewaacha, wengine wana mtoto mmoja, wawili mpaka watatu. Lakini pia siku hizi kumekuwa na vijana wengi ambao kimsingi walipaswa kuwa kwenye ndoa wawe na watoto kadhaa, ila wapo mtaani tu na wengi wao wana watoto ambao wamezaa na wanawake kisha wamewaacha.

Vijana wengi wakikaa kijiweni hoja yao ni kuhusu ugumu wa maisha, wengi wana hofu ya kuhudumia familia, wanaogopa kuitwa mume, wanaogopa kubeba majukumu, wanafarijiana kwamba muhimu wapate mtoto mmoja au wawili watakaowasaidia uzeeni lakini kuoa hapana. Kwenye maongezi yao wanasema wanawake wa siku hizi nao hawatulii kwenye ndoa, hawaheshimu ndoa na hata wakiolewa pia wengi wao wanakuwa na michepuko.

Habari mbaya ni kwamba wanawake wengi wa siku hizi wamekuwa warahisi mnoo, wanathamini pesa kuliko magonjwa, kuliko mimba za nje ya ndoa, hawaoni tena kama zinaa ni dhambi. Vijana wengi wanaitumia hiyo chansi wanawazalisha kisha wanawaacha na mbaya zaidi ni kwamba hata baada ya kutia hizo mimba hawazihudumii. ajabu ni kwamba wapo wanawake wanaoifurahia hali hiyo lakini wanawake wengi zaidi wameishia kujutia.

Unaambiwa na mpenzi wako nizalie kwanza mtoto ndio nikuoe, nijue kama una kizazi au laah, nijue mtoto wangu anafananaje, na wewe mwanamke bila kutafakari unakubali ukijua unapendwa, hata wanaojaribu kukataa wanapigwa na fungu la pesa wanakuwa walaini wanaacha milango wazi mimba inaingia. wengine wanatishwa kuachika endapo watakataa, basi mambo yakijipa mwanaume huyoo anakimbia zake, hakuoi na ndio inakuwa imeisha hiyo.

Mwarobaini wa hili tatizo ni mwanamke kujitambua, kujithamini, kuepukana na tamaa, kumjua Mungu, kutambua kama zinaa ni chukizo kwa Mungu. Wewe sio sehemu ya majaribio, wanawake wengi wanatia huruma, unakuta nyumba ina wapangaji sita, wapangaji watatu ni singo mama, ijue thamani yako, kaa ukijua kabisa ni chukizo kufanya zinaa lakini pia ni chukizo kuzaa nje ya ndoa, ni aibu, ni fedheha pia, jitambue jipe thamani.
 
Asante kwa ushauri kaka.
 
Back
Top Bottom