Kumekuwa na jambo la ajabu sana humu ndani la kuitana au kutambulishana kama wanaume wa Dar, hebu bila kuchanganya mada na mada nyingine (please Mods) naomba tupate uelewa wa hao watu.
Kwa uelewa wangu mimi na kuhusu shutuma wanazorushiwa kuwa hawawezi kwenda round zaid ya moja, ni waoga, wengi wanamiliki mali za kurithi, wengi wameathiriwa na chips mayai. Naomba kuulizia haya yafuatayo au kueleza yafuatayo
- ili kuweza kujua uwezo wa mtu ku-perfrom niu lazima either huyo mtu awe amekushirikisha kwa namna yoyote ile iwayo, umelala nae, ni ndugu yako au wewe ni daktari kwahio unajua mapungufu ya huyo mtu
- uwe una ushahidi wa kutosha tena uwe umefanya utafiti wa kutosha kufikia hitimisho hilo, na tafiti nzuri ni zile zenye supporting data gunuine
- Dar karibia asilimi 75 au zaidi ni wageni, je hao wanaume wa Dar ni hawa wageni au ni wale Migrants?
- Tunaposema hawajui mapenzi, tunarejelea kitu gani hasa?
- Tunapodai kuwa wengi wanamiliki mali za kurithi, tunataka kuuaminisha nini ulimwengu wa Tanzania? kwamba wazazi ambao wako nje ya Dar hawana kitu cha kuwaachia watoto wao?
No, nadhani hizi mada nyingine tujifunze kuwaheshimu wengine. Vinginevyo tunalea matabaka yasiyo ya msingi.