Hivi Harmonize ni mwanajeshi wa kikosi gani hadi avae nguo za jeshi, anaogopwa?

Nimeshangaa sana kuona msanii huyu anazunguka akiwa amejiachia na mavazi ya kijeshi wakati Raia wa kawaida wasiokua maarufu wakivaa wanaambulia kipigo na pengine kesi za uhujumu uchumi....
Ukiomba kibali kwa kazi fulani inayofahamika inakubalika, huwezi tumia mavazi haya bila kibali utachezea vitasa
 
Sijui kwa nini nimekumbuka ile kauli ya faru Ndugai kuwa serikali iongeze kodi kwenye vifurushi vya internet
 
Kama ni real Uniform za TPDF nadhani Hoja yako itakuwa na Mashiko na kuhitaji Mjadala zaidi ila kama ni just camouflage Uniform haina tatizo sana na hasa kwa Msanii kama Yeye ambaye huenda anazitumia Kiusanii tu.
Kasome tena ile sheria. Yaani hata nguo zinazofanana na za jeshi hairuhusiwi.
 
Kasome tena ile sheria. Yaani hata nguo zinazofanana na za jeshi hairuhusiwi.
Nawe pia Kasome Kanuni za Kisanii na Wasanii hasa pale wawapo Kazini ( hasa Kimaigizo ) yao nadhani unaweza Kuelewa zaidi. Mimi si Team Harmonize na simkumbali ila katika hili naona tunataka kutengeneza taswira ya Kisiasa na Chuki zetu ya Vyama kuwa anapendelewa kwakuwa tu anakubalika na Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli na Chama chake cha CCM.
 
Kawakamate wauzajj kwanza mbona mtukamate wavaaji halafu ukute ni rangi tu havifanani.

Vijana wenye pasaka mbili huko jeshini mnaona kama vile nchi yenu

Machinga wanauza kwa ajili ya makamanda na sio kwa ajili ya raia.Pasaka mbili sio tatizo, raia wa kawaida kuvaa mavazi ya kijeshi sio vizuri kwasababu unaweza kuyatumia kufanya matukio ya kuvunja sheria za nchi huku raia wakidhani wewe ni askari.
 
Nawashangaaga sana yaani wanatukamata wavaaji

Kwanini wasianze kuwakamata wauzaji maana wao wanaziuza deile yaani
Walishwahi kunj tagert bar
Nikwaambia nakaa kwa kanali Alli wakaniacha
Ukirudisha kumbukumbu nyuma, kisa cha kuzuia nguo, zinazofanana na za jeshi kuvaliwa ni kila mtu, na miaka ujambazi ulishamili sana, huku waharifu wakitumia mavazi ya jeshi, au yanayofanana nayo.
Yakiwemo ya polisi pia.

Sasa wanaofanyiwa uharifu, wakiulizwa majambazi walivalia kijeshi. hivyo serikali ikapiga marufuku, nguo zinazofanana na majeshi yetu kuvaliwa huku majumbani.

ila sasa Dunia inasonga mbele begi na nguo zinazo fanana na jeshi ziko tele mitumbani na madukani, wanahusika wanachotakiwa ni kuona vazi lilovalia siyo la kitanzania.
 
Hizo alizo vaa ndio za kijeshi? 😂 😂 😂 😂... The wonders of Afrika shall never cease to amaze me.
 
Vazi la kijeshi ni iwe imedhibitishwa kuwa na nembo/serial code au batch number ya serikali kwa upande wa ndani wa nguo yenyewe. Hilo tu ndio kosa. Lakini haya mengine, mbona mchina tu, yaani ni kupiga luku tu 😂 😂 😂
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom