Nilikaona kameanzisha tabia ya kuniangaliaangalia, nami nikageuka kuwa mwangaliaji pia.
Nikiwa mgahawani siku moja kakapita nikakakaribisha chai, kakachukua vitafunwa tu kakaenda.....ile kutokataa ikanisogeza kidogo kihisia (km unavyojua tena wanaume).
Siku nyingine nikakutana nacho na nikamwambia anione baadae, kakaitikia....tena kwakuwa kulikuwa na watu karibu, kakaitikia kidogo kidogo na kwa ufundi fulani ili wasisikie.
HAKUTOKEA! nasema hivi, HAKUTOKEA!!
Kwa jinsi ninavyojiheshimu hapa mtaani na kuheshimika, na pia kutokana na asili ya soni niliyonayo, nimeshindwa kabisa kumvaa na nimetafsiri km hiyo ni 'HAPANA' yake. Na mimi kiukweli huwa naheshimu sana 'hapana' za kina dada......kupigiwa kelele za 'nimekwambia sikutaki huelewi.....jitu zima hovyoooo?!!!' mpaka majirani wanishangae ni kitu sikiwezi kabisa.
Kilichonifanya niulize swali hilo katika title,
1. Siku hizi amejenga tabia zisizoeleweka; anaweza kubadili njia tukionana kwa mbali (ili tusikutane), lakini hunisalimia kwa kunistua nikiwa sijamuona (na hunisalimia kwa confidence ya hali ya juu).......hii ananifanya nishindwe kumuelewa anatakaje haswa! Hata tukiwa kwenye kusanyiko, akiona tumekutanisha macho basi haraka huhama eneo hilo ili nikiangalia tena nisimuone....hili linanifanya nijisikie vibaya na kujaribu kwa kila namna kutoangalia tu upande anaokuwa yeye.
2. Kila ninapoongea nae, basi siku hiyo lazima kuwe na vicheko vya kina dada sehemu fulani ninayopita.....yaani siku hiyo nikipita hapo (na ni lazima nipite) lazima kuwe na vicheko vya haja ambavyoo, kwa kutumia uzoefu wangu, najua kabisa kuwa vinanielekea mimi.
3. Nimeshangaa juzi kati kaja kuniaga safari yake (hili lilinishangaza kidogo), nilimtakia kila la kheri na kumuongezea kanauli kidogo.....hakuikataa, aliipokea na kushukuru. Aliporudi alikuja kunipa taarifa na kuendelea na maisha yake.
4. Kukiwa na kazi ya jamii (pamoja), maana tunaishi kijiji kimoja, basi atafanya kila namna awe katika kundi ambalo nipo.....hili nimelichunguza vya kutosha na lipo hivyo.
Wazoefu wa hivi vibinti hebu toeni uzoefu wenu katika hili hapo......kuna nini?!!