Hivi haiwezekani kuwa na alama za ufaulu za aina moja?

Hassan Mambosasa

JF-Expert Member
Aug 2, 2014
3,350
4,485
Habari zenu, hebu rejeeni kichwa cha uzi hapo juu. Naamini mpo vyema kiafya, hata mimi nipo hivyohivyo na shukrani zote kwa Muumba.

Kilichonifanya nikafungua uzi huu, ni kuhusu huu mfumo wa ufaulu ambao umewekwa na baraza la mitihani hapa nchini. Ambao umekuwa wa kutoeleweka kabisa, ili utumike kwa vizazi vyote vitakavyopitia hatua za kielimu hapa nchini.

Siku hizi huu mfumo wa upangaji wa madaraja na alama za ufaulu umekuwa kama rangi ya kinyonga, Kila kukicha ni wenye kubadilika hovyohovyo, mara mwaka huu watumie huu. Uje mwingine itumike vingine, hadi inakuwa haieleweki.

Mfano, unakuta hawa kidato cha pili wametumia mtindo wa DIVISION mwaka fulani, mara unakuja mwingine wanatumia GPA, mara wastani na hata ule wa DISTINCTION. Hata kidato cha nne haya yanatokea pia, si huko chini tu.

Hivi baiwezekani zile alama za kizamani zikaendelea kutumika kama mwanzo, ila kufanyike maboresho tu kuendana na teknolojia ya sasa ilivyo?

Kushuka kwa thamani ya elimu hapa nchini, hadi mtu akifaulu kidato cha nne anaonekana kama kavuka mtihani wa kujipima wa darasa la nne. Hakutokani na huku kubadilika kwa hii mifumo?

Sasa hivi imekuwa kama ni mchezo yaani, akija kiongozi huyu atabadilisha na kuweka hivi. Mara mwingine aweke vile, ilimradi aonekane naye alipita kwenye uongozi na kufanya kitu. Pasipo kukumbuka wanatuharibia elimu na kutyletea mkanganyiko kwenye vyeti tu.

1579006754887.jpeg
 

Attachments

  • AJIRALEO.COM_MFUMO_WA_KUTUNUKU_MATOKEO_2016.pdf
    320.1 KB · Views: 2
Ilikuwa mwaka 2013 ilikuwa mpaka division five ya 45 na mwaka 2014 ndio kulikuwa na nasuala ya GPA, 2015 mfumo ulitumika wa GPA mda wa masomo but matokeo yakaja kwa division.

But now, hizo Mambo haziko ni division ndio instumika from 2016.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ilikuwa mwaka 2013 ilikuwa mpaka division five ya 45 na mwaka 2014 ndio kulikuwa na nasuala ya GPA, 2015 mfumo ulitumika wa GPA mda wa masomo but matokeo yakaja kwa division.

But now, hizo Mambo haziko ni division ndio instumika from 2016.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ila angalia alama za ufaulu pia, zinavyobadilika kama kinyonga
 
kikwete alikua anaelekea kuua kabisa elimu yetu..yule mzee hovyo sana.
 
Back
Top Bottom