Hahahaaa, jamaa halitaki Wapambe. Anakupa za usoni moja kwa moja.
CC:
FirstLady1
Nimekaa Geita Tangu mwaka 2000 mwezi wa Pili,nimeshiriki uchaguzi wa mwaka huo,katika jimbo la Geita akapatikana Mbunge anaitwa Ernest Mabina,kwenye Jimbo la Busanda alipatikana Mbunge anaitwa Faustine Rwilomba Kabuzi (Marehemu),na Jimbo la Nyang'hwale alikuwepo James Musalika.
Wabunge hawa walifanya kazi kubwa sana ya kujaribu kuijenga Geita,lakini walikuwa wakibebwa sana na Marehemu Kabuzi ambaye hadi leo hii bado anakumbukwa kutokana na juhudi zake katika kuwapelekea wananchi wa Jimbo lake maendeleo pamoja na Wilaya yote ya Geita wakati huo kabla haijapata Mkoa,lakini Pia Mabina alikuwa akijitahidi sana ingawa yeye ni mtu wa Ground hakuwa na maneno mengi sana mitaani,kuongea sana alikuwa hajui isipokuwa alikuwa mtekelezaji,nadhani hii huenda ilisababishwa kwake na shughuli yake za Usalama wa Taifa,kwa sababu mara nyingi ni watu wakimya sana mfano mwingine ni Mbunge wa jimbo la Mbogwe Augustine Masele,naye mkimya mkimya lakini mambo yake chinichini sana.
Wabunge hawa wote walirudi kwenye uchaguzi wa mwaka 2005 kwa kishindo lakini kwa bahati mbaya Kabuzi akafariki Dunia mwaka 2007,wakati wao walikuwa wakiitwa 'UTATU MTAKATIFU' hadi Bungeni na walikuwa wasumbufu,hata hivyo huyu Mbunge wa sasa Max alijitahidi sana kumsumbua Mabina wakati huo na hasa kwenye uchaguzi wa mwaka 2005 lakini alishindwa vibaya,wakati huo maxalikuwa na hela za Pamba kwa sababu alikuwa akifanya kazi kwenye kampuni moja inaitwa Copcot ambayo ilikuwa ya shemeji yake mzungu ambayo pia iko huko Kampala.
kutokana na pesa hizo aliamua kupanda nyasi kwenye eneo la hospitali ya wilaya ya Geita,pamoja na pembezoni mwa barabara ya Geita mjini ukielekea Mwanza kama mita 400 hivi pamoja na kujenga Public Toilet inayotumika hadi sasa ila kwa kulipia,hapo watu wakaona kwamba yeye ni mwanamaendeleo wakamshauri kugombea ubunge kwamba ataleta maendeleo kwa wakazi wa Jimbo la Geita,lakini mwaka 2005 akashindwa na alimfanyia visa kweli kweli aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo Mabina.
Miongoni mwa mambo hayo ni pamoja na kuwanywesha vijana viroba na kwenda kumzomea Mabina kwenye mikutano yake ya hadhara yote na hasa mjini Geita(kwenye uwanja wa Kalangalala),lakini huko vijijini alikuwa akishindwa wanamtoa mbio,hali hiyo iliwashawishi hata viongozi wa ngazi ya Mkoa na Taifa wa CCM na kumuona Mabina kama mtu anayewaharibia chama na ilipofika uchaguzi wa mwaka 2010 akashinda lakini kwa kutumia mchezo mchafu sana wa kununua kadi 3500 na kuzisambaza kwa watu wake ambao walikuja kumpigia kura,ingawa mbinu hiyo pia ilikuwa imetengenezwa na CHADEMA wakijua kwamba akishinda yeye na kupita kwenye kura za maoni ndani ya ccm itakuja kuwa rahisi sana kumshinda kwenye uchaguzi mkuu.
Ndicho kilichotokea alishinda na baada ya hapo upepo ukageuka,alishambuliwa na almanusra CHADEMA ishinde jimbo hilo kama sio wizi wa kura kwenye baadhi ya maeneo lakini pia kuna uzembe CHADEMA walifanya nadhani ni kutokana na kutokuwa wazoefu wa uchaguzi na hasa Rogers mgombea wa chadema na kundi lake wakazidiwa ujanja kidogo,chadema alipata sapoti kubwa sana kutoka hadi kwa wanaccm wenyewe ambao walikuwa wakiamini kwamba huyo Max hafai kubwa Mbunge.
kwa hiyo hayo yanayotokea sasa hivi ni halali kwa wakazi wa Geita ili wajifunze wakiambiwa wawe wanasikia na sio kushabikia kila mtu,jamaa sasa hivi linatembea na viroba tu kwenye mifuko ya koti na suruali,halina time na mtu na halijawahi hata kufanya mkutano mmoja wa hadhara iwe ni kuwashukuru wananchi ama kuzungumzia shughuli za maendeleo,labda kama anadandia ile ya wakubwa ambao nao siku hizi wanamkataa kwenye mikutano yao wanamwambia ajifiche kwa sababu anazomewa LIVE yani ile yenyewe,na nasikia kwamba hagombei tena ndio maana ameamua kutumia pesa zake vizuri.
Kuna mengi sana ya kuelezea juu ya huyu Mbunge wa Geita lakini ndio hivyo tena nitawachosha.hafai jimbo liko wazi.