Hivi gazeti la Daily News nalo lilifungiwa?

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
89,981
2,000
Mara baada ya Rais Samia kuchukua madaraka, gazeti la serikali, Daily News, lilichapisha tangazo kutoka STAMICO, la kumpongeza Rais huyo mpya.

Zaidi ya kumpongeza, tangazo hilo hilo pia lilitoa masikitiko ya kufiwa/ kufa kwa Rais Samia Suluhu Hasan!

Lilikuwa tangazo la hovyo kweli. Sijui hata lilipitaje kwenye mchujo wa uhariri.

Daily News lilifungiwa?

D2496D0C-16B0-4411-ABCD-DDF5C7D87C8B.jpeg

Leo serikali imelifungia gazeti la Uhuru kwa kile kinachodaiwa ni kumzulia Rais maneno ambayo hakusema katika mahojiano yake na Salim Kikeke wa BBC!

Maajabu ya mwaka haya!

Kwa nini ninajiwa na hisia za kutilia shaka ufungiwaji huo wa gazeti la Uhuru?

Kati ya kuzuliwa maneno ambayo mtu hajasema na kuzuliwa kifo, kipi kilicho kibaya kukizidi chenzake?

Isije kuwa CCM wanatuchezea akili. Isije kuwa wametengeneza tukio la kujichukulia hatua ili huko mbeleni tukio hilo lije kutumika kama rejea ya kuhalalisha kuwabana mbavu wale wote wanaoonekana kuleta chokochoko.

Twaweza kuambiwa ‘serikali ya CCM haina upendeleo. Hata vyombo vyake vya habari huwa inavifungia’.

Kuna kitu ndani kabisa ya mifupa yangu kinachonambia ‘Ngabu, stuka! Maigizo tu hayo ya kutengeneza mazingira ya kuja kuhalalishia yajayo huko mbeleni’.

Tujiulize: Hivi kwa mfano hilo gazeti la Uhuru lingemzushia mmoja wa viongozi wa upinzani, tuseme lingemzushia Tundu Lissu kifo [kama yeye alivyomzushia yule mlinzi wa Magufuli], serikali ingelifungia kweli? CCM nao wangesitisha uchapaji wake kweli?

Sidhani!!!!
 
Kavirondo

JF-Expert Member
May 2, 2020
426
1,000
Hiyo ya DailyNews inaonekana zaidi ni makosa ya uhariri na si kudhamiria..
Hii ya Uhuru ni habari nyingine.."Wamemlisha Maneno Mama"..kwa mujibu wa wenye Chama

Sent from my SM-A405FN using JamiiForums mobile app
 
Kavirondo

JF-Expert Member
May 2, 2020
426
1,000
Habari nzima ya Uhuru iko wapi? Umeisoma? Wametumia/ wameweka alama za kunukuu?
Kichwa cha habari Uhuru ni Nukuu Tosha..
..Na kama kweli katika mahojiano na BBC hakutamka hicho kitu,basi Wao kama Chama wana haki ya kuwachukulia hatua kwa mujibu wa miongozo waliojiwekea..
2877974_FB_IMG_16286913241432301.jpg

Sent from my SM-A405FN using JamiiForums mobile app
 
chivala

JF-Expert Member
Apr 13, 2021
769
1,000
Wasiwasi wangu naona kufungiwa gazeti la UHURU kwa siku 14 ni bosheni tu, sababu hawa walikua wakiyafungia magazeti, vituo va redio na television miezi 6 na, iweje leo uhuru iwe siku 14?
 
Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
89,981
2,000
Kama ni msomaji wa magazeti ya kibongo "Kiswahili Sanifu" ni msamiati mgumu sana.
Pengine haikidhi Sifa za nukuu..Lakini hicho kichwa ni nukuu na ndio maana limetumika neno "kumlisha maneno"

Sent from my SM-A405FN using JamiiForums mobile app
Hicho kichwa cha habari si nukuu. Nukuu ina alama zake zinazomjulisha msomaji kuwa anachokisoma ni nukuu ya maneno ya anayezungumziwa.

Alama za uandishi zina maana zake.

Kwa mfano, ukiwa unauliza swali kwa maandishi halafu usiweke alama ya kuuliza, hicho ulichokiandika kitakuwa si swali.
 
Ibambasi

JF-Expert Member
Jul 25, 2007
8,978
2,000
Mara baada ya Rais Samia kuchukua madaraka, gazeti la serikali, Daily News, lilichapisha tangazo kutoka STAMICO, la kumpongeza Rais huyo mpya.

Zaidi ya kumpongeza, tangazo hilo hilo pia lilitoa masikitiko ya kufiwa/ kufa kwa Rais Samia Suluhu Hasan!

Lilikuwa tangazo la hovyo kweli. Sijui hata lilipitaje kwenye mchujo wa uhariri.

Daily News lilifungiwa?

Leo serikali imelifungia gazeti la Uhuru kwa kile kinachodaiwa ni kumzulia Rais maneno ambayo hakusema katika mahojiano yake na Salim Kikeke wa BBC!

Maajabu ya mwaka haya!

Kwa nini ninajiwa na hisia za kutilia shaka ufungiwaji huo wa gazeti la Uhuru?

Kati ya kuzuliwa maneno ambayo mtu hajasema na kuzuliwa kifo, kipi kilicho kibaya kukizidi chenzake?

Isije kuwa CCM wanatuchezea akili. Isije kuwa wametengeneza tukio la kujichukulia hatua ili huko mbeleni tukio hilo lije kutumika kama rejea ya kuhalalisha kuwabana mbavu wale wote wanaoonekana kuleta chokochoko.

Twaweza kuambiwa ‘serikali ya CCM haina upendeleo. Hata vyombo vyake vya habari huwa inavifungia’.

Kuna kitu ndani kabisa ya mifupa yangu kinachonambia ‘Ngabu, stuka! Maigizo tu hayo ya kutengeneza mazingira ya kuja kuhalalishia yajayo huko mbeleni’.

Tujiulize: Hivi kwa mfano hilo gazeti la Uhuru lingemzushia mmoja wa viongozi wa upinzani, tuseme lingemzushia Tundu Lissu kifo [kama yeye alivyomzushia yule mlinzi wa Magufuli], serikali ingelifungia kweli? CCM nao wangesitisha uchapaji wake kweli?

Sidhani!!!!
Ni vigumu sana kuamini kuwa Uhuru wangeweza kufanya Hilo "kosa" kwa namna yoyote ile. Pili tazama tu jinsi hatua zingekuwa haraka hivi. Inaleta maswali mengi
 
IDEGENDA

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
4,128
2,000
Hii habari ni ya kipumbavu sana, sioni kama kuna haja ya watu kukoseshwa kazi kisa hii habari.

Samia nae akibariki huu ujinga ntamshangaa sana!
.
Labda kama kuna kitu wame target.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom